Wednesday, January 6, 2010

WATUHUMIWA WA UJAMBAZI SONGEA WAKAMATWA

Jeshi la Polisi Mkoani RUVUMA linawashikilia watu kumi wanatuhumiwa kuhusika katika tukio la kuwavamia askari wawili waliokuwa wakitoka lindoni na kuwapora bunduki mbili aina ya SMG na Risasi Sitini Jana Alfajiri.

Wakati huo huo hali ya askari Mmoja PC Rajab aliyepigwa na kitu kizito kichwani bado ni mbaya na tayari Helkopta ya Jeshi la Polisi imemchukua kutoka Hospitali ya Mkoa Mjini Songea na Kumuhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu zaidi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Songea Dr PETER KIULA amesema uchunguzi wa awali umeonesha PC Rajab amepata madhara katika fuvu la kichwa na kusababisha kuminyika kwa ubongo na kuganda kwa damu

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA amesema Pamoja na kukamatwa kwa watu kumi ambao wanaendelea kuhojiwa na Polisi, Msako Mkali unaendelea katika maeneo mbalimbali ili kuwapata watuhumiwa wengine pamoja na Bunduki mbili na Risasi 60 ambazo hazijakamatwa.

Tukio hili limeendelea kuleta hali ya wasiwasi kwa wakazi wa manispaa ya SONGEA ambao wanahofia Bunduki na risasi zilizoporwa kutoka mikononi mwa Polisi kutumika kuwadhuru. (Habari kwa Hisani ya Gerson Msigwa)

No comments:

Post a Comment