Thursday, January 14, 2010

PINDA AWASHUKIA WABUNGE VING'ANG'ANIZI


Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda amewashukia wabunge king'ang'anizi ambao wapo Bungeni kwa miaka lukuki na kukataa kung'atuka.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari vya habari nchini na kugusia mambo mbalimbali ambayo yanaikabili nchi.

Waziri Mkuu Pinda amesema wakati umefika kwa Wabunge ambao wamekaa kwa muda mrefu madarakani kuwapisha wengine kwani wapo wengi wenye uwezo wa kuongoza.

Kama hiyo haitoshi Waziri Mkuu Pinda amesema Tanzania imejaa watu walioelimika na ambao wanaweza kuwa wabunge mahiri.

Lakini wahariri nao walitaka kujua kama na yeye Waziri Mkuu muda wake wa kuondoka madarakani haujafika ndipo alipojibu kuwa yeye angali bado hajafikia ukongwe ambao unalalamikiwa na wengi.

Waziri Mkuu Pinda akamalizia kwa kuwataka Wabunge kuiga mfano wa Marehemu Mzee Mfaume Kawawa "Simba Wa Vita" ambaye aling'atuka madarakani akiwa bado na umri mdogo.

No comments:

Post a Comment