Thursday, January 14, 2010

MAHAKAMA YA KISUTU YAWAACHIA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WA NBC UBUNGO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachiwa huru watuhumiwa tisa wa ujambazi kati ya kumi na moja ambao walikuwa wanashikiliwa kwa kuhusika katika wizi wa shilingi milioni 168 katika Benki ya NBC Tawi la Ubungo. Hakimu Beragia Kadai ndiye ambaye amewaachia watuhumiwa hao kwa madai ya ushahidi kutojitosheleza.

Wakati watuhumiwa hao tisa wakiachiwa huru na Hakimu Kadai mmoja Rashid Eliakimu maarufu kama Rama Mdogo yeye amekutwa na hatia na kupewa kifungo cha miaka 30.

Mmoja wa watuhumiwa hao wa kesi hiyo walipoteza maisha wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa.

Watuhumiwa hao ambao walihusika katika kesi ya ujambazi wa mwaka 2006 walipovamia NBC Tawi la Ubungo na mwanamke mmoja akafunga barabara akiwa na bunduki kabla ya kufanikiwa kuchukua milioni 168

No comments:

Post a Comment