Wednesday, January 6, 2010

UTEUZI WA RAIS MKURABITA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Mheshimiwa Anna Makinda, Mbunge na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya MKURABITA kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa Jumatano, Januari 6, 2010, Ikulu, Dar Es Salaam, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, George Yambesi, imesema kuwa uteuzi huo ulianza Desemba 24, mwaka jana, 2009.

Taarifa hiyo ya Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Yambesi pia imesema kuwa Mheshimiwa Rais amewateua wajumbe 11 wa Kamati Tendaji hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Walioteuliwa ni Bwana Peter A Ilomo (kutoka Ofisi ya Rais, Ikulu), Bibi Monica Mwamunyange (kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi), Dkt. Donath R. Olomi (kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam), Bibi Anna Mdemu (kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Bwana Desystant S Massawe (kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara) na Bwana Casmir Kyuki (kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali).

Wengine walioteuliwa, kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Bwana Joseph John Ndunguru (kutoka Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba), Bwana Severini Kahitwa (kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI), na Mhandisi Ladislaus Salema (kutoka MKURABITA)

Taarifa hiyo pia imewataja wateuliwa wengine kuwa ni Bwana Joseph A Meza (kutoka Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar), na Bwana Mohamed A Mohamed (kutoka Wizara ya Maji, Miundombinu, Nishati na Ardhi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar).

No comments:

Post a Comment