Monday, January 18, 2010

RAIS KIKWETE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA!!!

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Jumatatu, Januari 18, 2010, amewapatia wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, gari la wagonjwa, ili kupunguza shida ya usafiri wa wagonjwa katika eneo hilo.

Katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Mheshimiwa Kikwete amekabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mbozi, Bwana Levison Jeremiah Chilewa.

Mheshimiwa Kikwete aliwaahidi wananchi wa Kamsamba gari hilo wakati alipotembelea eneo hilo mwishoni mwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment