Thursday, January 14, 2010

CUF YATAKA UCHUNGUZI ZAIDI CHUO KIKUU HURIA

CUF – Chama cha Wananchi kimesikitishwa na taarifa za tuhuma za Wahadhiri wa nne na mtaalamu wa Kompyuta wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) za kuharibu matokeo ya mitihani kwa nia ya kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.

CUF – Tunatambua kuwa elimu ya juu kwa Taifa lolote ni muhimu kwa sababu inalenga katika kuwaandaa wataalamu mbalimbali kuja kukabidhiwa majukumu mazito kwenye jamii yetu. Kutokana na serikali ya CCM kutotathimini elimu kwa ujumla Tanzania tumekuwa na udhaifu mkubwa katika udhibiti wa mitihani kuanzia elimu ya msingi hadi ya juu na kushindwa kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

CUF – Tunaitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina kwa miaka yote katika chuo hicho na vingine nchini, pia wote waliohusika na tuhuma wafanyiwe uchunguzi wa kina mwenendo katika elimu zao ili kuweza kujua chanzo na kulipatia ufumbuzi na kuweza kuchukua hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine na kuweza kuepusha kupata wataalamu vihiyo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment