Tuesday, December 15, 2009

MTIBWA YAPATA KICHAPO TUSKER

MABINGWA WATETEZI MTIBWA SUGAR WAANZA VIBAYA KAMPENI ZAO TUSKER
Klabu ya Mtibwa Sugar kutoka Turiani Manungu Mkoani Morogoro muji kasoro Bahari imeanza vibaya harakati zake za kutetea ubingwa wake wa Tusker. Wakata Miwa wa Manungu wameanza mawindo yao kwa kupata kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa Mabingwa wa Kenya, Sofapaka. Magoli ya wageni yamefungwa na John Onami (28), Muyoti Nicholaus (61) na Hogo Nzoka (80). Goli la kufuatia machozi la Mtibwa limefungwa na Obadia Mungusa (84). Kindumbwe ndumbwe kuendelea kesho katika ya Mafunzo (Tz) dhidi ya Tusker (Kenya).

No comments:

Post a Comment