Thursday, December 17, 2009

CUF NAO WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA GAMA

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZIMEENDELEA KUTOLEWA KUFUATIA KIFO CHA LAWRENCE GAMA
CUF – Chama cha Wananchi kimepokea taarifa ya kifo cha Dokta Lawrence Gama kwa masikitiko makubwa.

Marehemu Dokta Lawrence Gama alikuwa ni mzalendo ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Serikalini na za Chama cha Mapinduzi, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Marehemu alikuwa Kada muhimu wa Chama cha Mapinduzi.

CUF – Chama cha Wananchi kinampa pole Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, familia ya marehemu, wanachama wa CCM na wananchi wote kwa ujumla.
Mungu ilaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment