Monday, December 21, 2009

CUF WADAI MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI

MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI HAYAKUSHIRIKISHA WADAU.

CUF – Chama cha Wananchi hatukuridhishwa na maamuzi ya kutoshirikishwa vyama vya siasa, pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kuonyesha haja ya kufanya marekebisho katika sheria ya Uchaguzi, sura 343 na sheria ya uchaguzi wa serikali za Mitaa sura ya 292 kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya Habari wiki hii.

Muswada huo unakusudia kuondoa mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika chaguzi zilizopita kwa lengo la kuiwezesha Tume kuendesha chaguzi kwa ufanisi.

CUF – Chama cha Wananchi tumesikitishwa na hatua hii iliyochukuliwa kwa kuandaliwa muswada pasipo kuwashirikisha wadau wakuu wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa vilivyosajiliwa kwa misingi halali .

CUF – Tunaamini kuwa nchi yenye serikali adilifu ni ile inayofanya maamuzi yake kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na utawala bora kwa kushirikisha walengwa na wadau ili kupata mawazo bora yatakayoboresha jambo husika kuliko kuwaamulia kwa utashi na matakwa ya waliopewa madaraka, kwani maamuzi hayo yanaweza yasiwe na tija wala siyo suluhisho la tatizo husika.

No comments:

Post a Comment