Monday, December 14, 2009

CUF YAWATETEA WALIMU

SERIKALI IFANYE UCHUNGUZI YAKINIFU JUU YA MADAI YA MAFAO YA WALIMU

CUF – Chama cha Wananchi tumeshitushwa na taarifa za baadhi ya walimu kudai kuwa majalada aliyopewa Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CGA) yalikuwa na kasoro zilizosababishwa na watendeaji ndani ya Wizara.

Baadhi ya walimu hao wanadai nyaraka zilikuwepo isipokuwa upo uzembe katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutokana na watendaji kupoteza nyaraka na hatimaye mzigo kubebeshwa walimu.

Walimu hao wamemuomba Waziri wa Elimu na Mufunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe achunguze kwa kina rufaa za walimu atakazopelekewa na akubali kufuatilia kwa makini watendaji wake.

CUF – Chama cha Wananchi tunaunga mkono madai hayo ya kuidai Serikali ifanye uchunguzi yakinifu ili haki iweze kutendeka, kwani itambulike kuwa walimu ni nguvu kazi muhimu kwa Taifa, ambapo wanapaswa kujaliwa haki zao na kuthaminiwa mchango wao mkubwa wanaoutoa wa kulea na kuwafunza nguvu kazi ya baadae ya Taifa letu.

CUF – Tunakiasa Chama cha Mapinduzi na Serikali yake kiache kuwatumia vibaya baadhi ya walimu wanaoteuliwa kusimamia ukarani na usimamizi mdogo wakati wa uchaguzi katika kuhujumu na kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

CUF – Tunawasihi walimu kutambua wazi kuwa viongozi wa Serikali iliyopo madarakani ambao wamechaguliwa na wananchi, wapo kwa ajili ya maslahi yao pamoja na vizazi vyao, hivyo shime walimu kuungana na Chama cha CUF, chenye nguvu ambacho ni mbadala, kuhakikisha viongozi hao hawarudi madarakani na kukiweka chama hicho kitakacho jali maslahi, stahiki na haki ya kila mtanzania.

No comments:

Post a Comment