Tuesday, December 29, 2009

MAMBO YA CUF KWA SERIKALI HAYO!!

SERIKALI IWE NA HURUMA NA MATUMIZI MABAYA YA KODI ZA WALALAHOI.

CUF – Chama cha Wananchi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Beno Ndulu kwa kutumia zaidi ya Tshs bilioni 1 za walipa kodi kujengea nyumba yake na kutamka kuwa ni jambo dogo.

CUF – Tunaungana na Watanzania wengine wote wenye uchungu, waliotoa vilio vyao juu ya ufujaji huu wa mapesa hali Taifa letu likikabiliwa na tatizo la njaa, upungufu wa madawa katika Zahanati, ukosefu wa vifaaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule zetu za sekondari hususani hizi za kata.

CUF – Chama cha wananchi tunaimani serikali yenye viongozi makini ni ile inayotoa vipaumbele vyenye maslahi na Taifa kwa sasa na baadaye, kwani uapoboresha elimu unajenga msingi mzuri wa kuzalisha wataalamu wengi bora wa baadae ambapo utakuwa na wenye uwezo wa Ugavana wengi, Wahandisi wengi na Madaktari wakutosha .

CUF - Tunawatanabaisha Watanzania kuwa makini na kuzinduka na viongozi wa serikali ya Mapinduzi kwani wapo kwa ajili ya maslahi yao na familia zao, na hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuwajibisha nyingine kwani kila mamlaka imeoza, hivyo ni jukumu lao wananchi kuhakikisha serikali iliyopo madarakani hairudi tena katika uchaguzi ujao wa 2010.

MATOKEO YA LIGI KUU ENGLAND!!!

Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba akifunga goli la kusawazisha kwa timu yake
Wachezaji wa Tottenham Hotspurs wakishangilia goli lao la pili dhidi ya West Ham United
Carlos Tevez wa Man City akifunga goli la tatu katika mchezo dhidi ya Hull City
Cameron Jerome wa BirminghamCity akifunga goli dhidi ya Stoke City
Wachezaji wa Blackburn Rovers wakimpongeza Al Hadj Diouf mara baada ya kuisawazishia timu hiyo dhidi ya Sunderland

Barclays Premier League
Wolverhampton 0-3 Man City

THAMAHANINI JAMANI!!!!

Mambo vp wadau? Me mzima lakini niombe radhi kutokana na kuwepo kwa kwikwi pamoja na kigugumizi cha Internet yangu lakini mambo sasa swadakta!! Huree

Sunday, December 27, 2009

YANGA BINGWA TUSKER

YANGA 2-1 SOFAPAKA
Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Tusker baada ya kuifunga Sofapaka ya Kenya kwa magoli 2-1. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uga wa Uhuru maarufu kama Shamba la Bibi. Magoli ya Yanga yamefungwa na Boniface Ambani (84) na Mrisho Ngassa (89). Hongera wazee wa Jangwani kwa ushindi. Mwali amebaki tena nyumbani kwa mwaka mwingine.

Saturday, December 26, 2009

CHELSEA YABANWA MBAVU

DAKIKA 90 ZA MCHEZO BIRMINGHAM 0-0 CHELSEA
Vinara wa Ligi Kuu nchini England Chelsea wamebanwa mbavu mara baada ya kulazimishwa sare tasa na Birmingham City. City itabidi wajilaumu wenyewe kutokana na kukose nafasi nyingi. Picha zaidi na matokeo mengine baadaya kama si kesho. Me mwenyewe naangalia mechi saa hii.

SIMBA 2-1 TUSKER

WEKUNDU WAAMBULIA NAFASI YA TATU KWENYE TUSKER
Vinara wa Ligi Nchini Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika Mashindano ya Tusker mara baada ya kuifunga Tusker ya Kenya kwa magoli 2-1. Magoli ya Mnyama Mkali kuliko wote Mwituni yamefungwa na Mohamed Kijuso (89) na Ramadhani Chombo Redondo (95). Mchezo umechezwa kwa dakika 120. Kwa ushindi huo Wekundu wanaondoka na kitita cha Milioni 20. Hongera Mnyama. Kesho kazi katika ya Yanga (Tz) na Sofapaka (Kenya) fainali Uwanja wa Taifa.

Friday, December 25, 2009

ANGALIA TASWIRA HIZI!!

PICHA ZA WALIOKUWA VIONGOZI WA JUU WA TAIFA HILI KATIKA SERIKALI ZA AWAMU YA TATU NA YA NNE
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa
Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne Edward Ngoyay Lowassa
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tatu Basil Pesambili Mramba

Hivi ukiziona Taswira za Viongozi hawa unakumbuka nini kwa haraka haraka katika Uongozi wao? Viongozi hawa wametumika taifa hili katika serikali ya awamu ya tatu pamoja.

MNYAMA KUSAKA MSHINDI WA TATU

WEKUNDU WA MSIMBAZI KUSHUKA DIMBANI DHIDI YA TUSKER LEO
Vinara wa Ligi Kuu nchini Simba leo wanatarajiwa kushuka dimbani kuumana na Tusker katika mchezo wa kulinda heshima wakati wakisaka nafasi ya mshindi wa tatu. Simba ambao waliondolewa kwenye Nusu fainali na Watani zao wa Jadi Yanga itakuwa pia inasaka Milioni 20.

MABINGWA WA U.S OPEN WAKIPOZI KWA PICHA

HAWA NDIYO WALIOONDOKA NA MATAJI YA U.S. OPEN KWA MWAKA HUU WA 2009
Roger Federer akiwa na Serena William mara baada ya kutwaa mataji yao ya U.S Open mwezi August mwaka huu. Picha hii ilipigwa katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

SALAMA ZA X-MASS NA MWAKA MPYA KUTOKA CUF

TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA XMAS NA KHERI ZA MWAKA MPYA

CUF - Chama cha Wananchi tunawatakiwa watanzania wote sikukuu njema na kheri za mwaka mpya wa 2010.

Uwe ni mwaka wenye maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa Taifa letu na maisha yetu ya sasa pamoja na ya kizazi kijacho kwa kuchagua viongozi waadilifu wenye nia njema na nchi yao wanaoweza kulitumika Taifa kwa faida ya wote kwa kufuata misingi sahihi ya utawala bora na demokrasia na kuhakikisha pato la nchi linatumika kwa faida ya wote.

HAKI SAWA KWA WOTE

PACQUIAO KUMBURUZA KORTINI MAYWEATHER

KASHFA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA HUENDA IKASABABISHA MABONDIA HAWA WAKAFIKISHANA KORTINI.Bondia Manny Pacquiao ametangaza nia yake ya kumburuta kortini mwanamasumbwi Floyd Mayweather Jr, Baba yake Mayweather Sr na Promota wake kutokana na kumuhusisha na utumiaji wa dawa za kulevya. Mabondia hao ambao ilibidi wapigane mwezi March kabla ya kuzuka mizengwe wameanza vita ya kutupiana maneno ambayo imewafikisha hapo walipo.

BEI YA WESE UMEIONA??

HAYA KAZI KWAKO HIYO NDIYO BEI YA MAFUTA KAMA HUWEZI KUMUDU FUNGIA GARI LAKO NDANI
Kwa hali hii huko tunakokwenda siku moja magari yatapungua tu barabarani na kutuepusha na kadhia ya foleni kwani kila siku bei ya Mafuta inazidi kupaa. Haya we!!!

PAPA APIGWA MWELEKA KWENYE MKESHA

PAPA BENEDICTO WA KUMI NA SITA AANGUSHWA NA MWANAMKE BAADA YA MISA YA X-MASS
Papa Benedicto wa Kumi na Sita amepigwa mweleka huko Vatican wakati wa Misa ya Mkesha wa X-Mass na mwanamke mmoja. Papa alirukiwa na mwanamke huyo ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Thursday, December 24, 2009

SALAMA ZA X-MASS KUTOKA KWA RAIS KIKWETE

MUENDELEZO WA SALAMU ZA X-MASS KATIKA MAADHIMISHO YAKE
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mama Salma Kikwete, wanatoa Salamu za Heri na Fanaka za Sikukuu ya Krismas kwa Watanzania wote.

Mheshimiwa Rais pamoja na Mama Kikwete wanawatakia Watanzania wote sikukuu salama, yenye furaha, amani na utulivu. Aidha, anawaomba madereva, hususani wa magari ya abiria kuwa waangalifu zaidi wanapokuwa kazini barabara katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismas na ile ya Mwaka Mpya.

Na katika kuadhimisha Sikukuu hiyo, Rais Kikwete, kama ilivyo jadi, ametoa mkono maalum wa heri kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa zawadi ya kuwawezesha nao kusherehekea sikukuu hiyo kwa furaha, kama walivyo watoto wengine wa Tanzania.

Mbali na kutoa zawadi kwa watoto hao yatima, Mheshimiwa Rais pia ametoa zawadi ya namna hiyo kwa Wazee, waliopo katika nyumba maalum za wazee.

Watakaonufaika na zawadi hiyo ya Mheshimiwa Rais, ambayo ni vyakula ni walioko katika vituo 28 vya mikoa minane ya Tanzania Bara.

Vituo hivyo ni saba vya Mkoa wa Dar es Salaam, vyote vilivyoandikishwa rasmi katika Mikoa ya Dodoma, Kigoma, Mwanza, Tabora na Tanga, na kituo kimoja kimoja katika mikoa ya Iringa na Arusha.

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, vitanufaika vituo vine: Nyumba ya Wazee ya Sebleni iliyoko Unguja, na Nyumba ya Wazee ya Limbani, Pemba na vituo viwili vya watoto yatima vya Mabaoni na Istikama vilivyoko Pemba.

Kwa mara nyingine, Mheshimiwa Rais Kikwete, na mkewe Mama Salma Kikwete wanawatakia Watanzania wote Sikukuu yenye Heri ya Krismas.

MSIMBAZI HOI TUSKER

YANGA 2-1 SIMBA
Mabingwa Watetezi wa Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Tusker mara baada ya kumbanjua Mnyama mkali kuliko wote mwituni Simba kwa Magoli 2-1. Magoli ya Yanga yamefungwa na Jerryson Tegete (68) huku la pili likifungwa na Shamte Ally (117). Goli la Simba lilifungwa na Hillary Echesa (80). Yanga kucheza fainali na Sofapaka wakati Simba wanasaka nafasi ya tatu na Tusker.

MERRY CHRISTMAS WANABLOGU WOTE!!!

JAMANI NOELI NJEMA LAKINI KUWENI MAKINI
Wanablogu me hata nyumbani hakuna Pilau kwa hiyo nawaishia kuwatakia kila la kheri katika Sikukuu ya Noeli kwani Yesu Kristo ndiyo anazaliwa hivyo. Kuweni makini na mpunguze nguvu wajameni.

NIMETIMIZA AHADI!!!!

JAMANI NILIAHIDI KUWAWEKEA TASWIRA ZA GARI LA MLIMANI TV NA RADIO
Gari la Mlimani Tv na Rdio likionekana katika Taswira tofauti tofauti lilivyo sasa mara baada ya kufanyika majambozz katika kuliweka katika muonekano wa kupendeza zaidi.

Wednesday, December 23, 2009

WATAALAM WAPO WENGI.!!

UNAAMBIWA KILA MTU NA FANI YAKE BWANA.
Kama unasumbuliwa na tatizo la Mchwa dawa ndiyo hii. Sasa unasubiri nini kumsaka huyu jamaa ili akusaidie. Tangazo hili lilinivutia ndiyo maana nikaamua kuliweka ili nawe ulione.

MABONDIA WA KWELI!!!

LINI NA SISI TUTAUKUWA NA MABONDIA MFANO WA HAWA ILI TUSHINDE MATAJI MAKUBWA

Mabondi Manny Panquiao (Shoto) na Floyd Mayweather Jr's (Kulia) waki katika picha ya pamoja. Mabingwa hawa wasiopigika wanatarajiwa kuzichapa mwezi March iwapo hakutaibuka longolongo ambalo limeanza kusikika.

SOFAPAKA YATINGA FAINALI TUSKER

SOFAPAKA 4-0 TUSKER
Mabingwa wa Kabumbu nchini Kenya, Klabu ya Sofapaka imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Tusker baada ya kuifyatua Tusker kwa jumla ya magoli manne kwa buyu. Sofapaka kwa sasa inasubiri mshindi kati ya watani wa jadi Simba na Yanga ili acheze naye fainali ya kuska mwali wa Tusker Mwaka huu. Simba na Yanga wanatarajiwa kusaka nafasi moja ya Fainali kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

MICHAEL SCHUMACHER AREJEA FORMULA 1

SCHUMACHER ASAINI MKATABA WA KUREJEA FORMULA 1 NA KAMPUNI YA MERCEDES
Dereva wa magari yaendeayo kasi na bingwa wa kihistoria wa michuano ya Formula 1 Michael Schumacher amesaini mkataba wa kurejea katika kinyang'anyiro hicho mwakani akiwa na kampuni ya Mercedes. Swali je jamaa atarejea na makali yake yale ambayo tulikuwa tunayafahamu?

CUF WATAKA VITENDO NA SI MANENO MATUPU

JAJI LEWIS MAKAME TUNATAKA TUONE MKITEMBEA KWENYE KAULI ZENU NA SIYO PROPAGANDA.
CUF – Chama cha Wananchi tumepokea kwa tahadhari kubwa maonyo aliyoyatoa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame kwa Maafisa wa Polisi nchini juu ya Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba 2010.

Jaji Lewis makame aliwaonya Maafisa hao wa Polisi kuwa ni makosa kujihusisha na Siasa kwani watakuwa wanakiuka Katiba ya Nchi lakini pia wao kama askari wajibu wao mkubwa ni kutetea, kulinda na kudumisha amani na wanapaswa kuwa makini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao hivyo wahakikishe uchaguzi unakuwa wa haki na amani.

CUF – Tumeipokea kwa tahadhari kubwa kauli hii na tena inatutia mashaka kwani Jaji Lewis Makame akiwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa alitakiwa kuwa mkweli kwa kukemea yale yote yaliyofanywa na askari Polisi hapa nchini katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita.

Jeshi la Polisi limekuwa likijihusisha kikamilifu na siasa na uchaguzi kwa kuegemea upande wa Chama cha Mapinduzi hasa katika maeneo ambayo yamekusudiwa Chama hicho kushinda kwa hali yoyote, ambapo imebidi askari kukimbia na masanduku ya kupigia kura yakiwa na kura ndani.


Hali hiyo ilijitokeza katika chaguzi za Serikali za mitaa zilizoranyika Oktoba mwaka huu katika mtaa wa Zombokoni Manispaa ya Temeke, Mtaa wa Muungano na Kagera katika Manispaa ya Kinondoni..

Hivyo kama haitoshi matukio kama hayo yalijitokeza katika chaguzi za 2005 na 2000 katika uchaguzi wa Zanzibar, lakini pia jeshi la Polisi limediriki kuwatisha wapiga kura siku moja kabla ya siku ya upigaji kura ambapo mwaka 2005 aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo nchini Omari Mahita akionyeshwa katika televisheni mbalimbali nchini akiwa ameshikilia visu vyenye mipini ya rangi ya bendera za CUF alidai wamekamata kontena nzima ya visu na majamvia yaliyotarajiwa kutumiwa na Chama chetu katika uchaguzi huo.

Tukio jengine la kusikitisha ni lile lilofanyika siku moja kabla ya uchaguzi wa 2000 katika mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni kwa chama cha CUF pale Jangwani Dar es Salaam ambapo kwa makusudi jeshi la Polisi liliamua kuwapiga mabomu ya machozi na kutishia kwa riasi za moto wananchi waliokuwa wanatoka mkutanoni.


CUF – Chama cha Wananchi tunasisitiza kuwa tunaipokea kwa tahadhari kubwa kauli za Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame, halikadhalika tunamtahadharisha Mkuu wa jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema kutofuata nyayo za Mkuu wa jeshi hilo aliyemtangulia ambaye aliligeuza jina jeshi hilo na kuliita ngunguri ili kukabiliana na kauli mbiu ya Chama cha Siasa cha CUF cha kuwataka wanachama wake kuwa ngangari.

MADAGASCAR HALI SI SHWARI!!!!!

HALI YA USALAMA NCHINI MADAGASCAR SI YA KURIDHISHA KUTOKANA NA WAANDAMANAJI KUFANYA GHASIA

Rais Andry Rajoelina ambaye ameingia madarakani kwa msaada wa jeshi la Madagascar
Wanajeshi wa Madagascar wakiwa imara kuzima maandamano yanayofanywa na wananchi wakipinga kupunguzwa kwao kazini. Taarifa zinaeleza kuwa wengi wa waliofukuzwa kazi ni wafuasi wa kambi ya Upinzani inayoongozwa na Rais wa zamani Marc Ravalomanana.

Tuesday, December 22, 2009

X-MASS IMEKARIBIA MABANGO NDIYO HAYA.

BANGO LIKIHAMASISHA USICHEZE MBALI SIKU YA MKESHA WA X-MASS. KAZI KWAKO
Ama kweli siku zimebaki mbili na kila sehemu kuna mabango ambayo yanahasisha watu wajitokeze na kustarehe katika kumbi mbalimbali. Starehe hizi chonde chonde ziendane na tahadhari ili mwisho wa siku furaha isijegeuka kilio.

UNAUJUA MTI WA X-MASS WEWE??

UMEUONA MTI WA X-MASS YAANI HUU NI MAALUM KWA SIKUKUU HII TU.
Mti huu kwa wale ambao haumjawahi kuuona ni maalum kwa X-mass. Kipindi cha kukaribia X-mass ndipo unachanua vizuri na kuonekana katika mandhari nzuri. Si unajua siku mbili zimesalia kabla ya X-mass nina maana kabla ya pilau haijaanza kunukia kwenye nyumba zetu.

BARIDI LAZIDI KULETA BALAA UROPA

WATU 90 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA BARAFU BARANI ULAYA
Idadi ya vifo inaonekana kuongezekaBarani Ulaya kufuatia kuongezeka kwa baridi kali na kusababisha barafu kuanguka huku nchi nyingine kiwango cha joto kikiwa -40. Kumekuwa na ajali nyingi za barani huku safari za ndege na treni zikiahirishwa kuhofia hali ya usalama.

MANDHARI YA ENEO LA MAKUMBUSHO

TASWIRA HIZI ZIMECHUKULIWA KWA NYAKATI TOFAUTI YAANI MOJA ASUBUHI NA NYINGINE USIKU
Mandhari ya eneo la Makumbusho mapema asubuhi majira ya saa kumi na mbili.

Taswira hii imechukuliwa usiku majira ya saa mbili katika eneo la Makumbusho

ZANZIBAR GIZANI MPAKA MWAKANI

MIUNGURUMO YA JENERETA MAPAKA MWAKANI ZANZIBAR
Taarifa kutoka Kisiwani Zanzibar zimethibitisha kuwa umeme ambao ilibidi uwake leo umeshindikana na sasa huenda hali ya stima ikatengamaa hapo mwakani. Habari ambazo zimethibitishwa na Waziri mwenye dhamana ya Umeme Zanzibar imeeleza kuwa kifaa ambacho kilikuwa kinashughulikiwa katika kijiji cha Fumba kimeharibika tena na kinatakiwa kipelekwe Afrika Kusini ili kichongwe. Na kutokana na hiki kuwa kipindi cha sikukuu ya X-mass mafundi wamepumzika. Kwa hiyo ni lazima kifaa hicho kitapelekwa mwakani kwa ukarabati kabla ya kuletwa kwa majaribio.

JAMBAZI LAKAMATWA

JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA LIKIWA KAZINI

Polisi Mkoani RUVUMA wamemkamata mtu mmoja aitwaye JOSEPH LUSINDE ambaye amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kutokana na kutoroka adhabu ya kifungo cha miaka 74 Jela kutokana na kupatikana na hatia ya mashitaka manne tofauti, yanayohusiana na Uuaji, Ubakaji na Wizi.

JOSEPH LUSINDE mwenye umri wa miaka 30, MKazi wa MAKAMBAKO mkoani IRINGA amekamatwa katika kituo kidogo cha basi cha MSAMALA hapa Mjini SONGEA majira ya saa 11 alfajiri akiwa katika harakati za kusafirisha mali za wizi alizoziiba kutoka kwa wakazi wa manispaa ya SONGEA.

Mtu huyu anayehusishwa na matukio lukuki ya uhalifu, inadaiwa alishahukumiwa na mahakama ya wilaya ya Songea kutumikia miaka 14 kwa kosa la uvunjaji na wizi, kisha akahukumiwa miaka 30 Jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na pia alihukumiwa miaka mingine 30 Jela baada ya kupatikana na hatia ya Mauaji huko MAKAMBAKO Mkoani IRINGA.

Kwa Maelezo ya Kamanda KAMUHANDA Mtu huyu alifanikiwa kutoroka adhabu hizi kwa kuwa kwanza alikuwa nje kwa dhamana na akiwa katika dhamana alitenda makosa mengine na kuhukumiwa pasipo yeye mwenyewe kuwapo mahakamani.

Kama waswahili walivyosema za mwizi Arobaini, na Arobaini za JOSEPH LUSINDE zikamfikia Desemba 21 mwaka huu saa 11 alfajiri, alipobambwa na vifaa vya ndani kama Luninga, Deck, Radio na Nguo ambavyo aliiba kwa nyakati tofauti katika nyumba za wakazi wa hapa Mjini SONGEA.

Kamanda KAMUHANDA anasema baadhi ya vitu hivyo vimeanza kutambuliwa na walioibiwa baadhi yao wakiwa ni ABENEGO SAKAFU na DOMINICA HAULE ambao waliripoti polisi hivi karibuni baada ya kuvunjiwa nyumba zao na kuibiwa.

Katika hali ambayo sio ya kawaida Mke wa JOSEPH LUSINDE aitwaye ZARAFI ZARAMALENGA amekamatwa na Polisi wa kituo kikuu cha hapa SONGEA wakati akimpelekea mmewe Chakula aina ya Pilau.

Polisi wamemkamata ZARAFI baada ya kubaini kuwa ndani ya chakula hicho alificha Hirizi kwa lengo la kumfikishia mmewe. Alipohojiwa juu ya Hirizi hizo amejitetea kuwa ni kinga.

Nimemuuliza kamanda wa Polisi Mkoani Hapa MICHAEL KAMUHANDA kukamatwa kwa JOSEPH LUSINDE kwaweza kuwa mwisho wa Mtandao wa uvunjaji nyumba za watu na wizi Wakati Polisi wa hapa RUVUMA wakiahidi kujiimarisha hapa Mkoani katika kudhibiti uhalifu, bado taarifa zinaonesha ipo kazi kubwa ya kushugulikia mtandao wa waharifu walio nje ya Mkoa huu ambao wamekuwa wakihusiana na waharifu wa hapa ndani.

Kama itakumbukwa vyema mwezi uliopita Mtu mmoja aliyewatapeli walimu zaidi ya shilingi milioni 5 Mkazi wa Kilimanjaro alishirikiana na wenzake kadhaa wa hapa Ruvuma, na katika kipindi hicho hicho Mtu mwingine akateka motto wa miaka minne na kasha kumrejesha baada ya kutekelezewa madai ya kupewa shilingi milioni 2 (Habari kwa hisani ya Mdau Gerson Msigwa)

Monday, December 21, 2009

HUYU NDIYE KAPTENI MOUSA DIDAS CAMARA

KIONGOZI ALIYENUSURIKA KIFO MARA BAADA YA MLINZI WAKE KUMPIGA RISASI

Kapteni Mousa Didas Camara ni Kiongozi wa Serikali ya Kijeshi ya Guinea ambayo iliingia madarakani kwa kufanya Mapinduzi wasioyomwaga damu. Kwa sasa Kapteni Camara anapatiwa matibabu nchini Morocco mara baada ya kusurika kifo kufuatia kupigwa risasi na mlinzi wake Luteni Abubacar Toumba Diakite.

WINTER UROPA NOMA.

KUANGUKA KWA SNOW KATIKA NCHI NYINGI ZA BARA LA ULAYA KUMESABABISHA WATU WENGI KUKWAMA MAJUMBANI.

Hii ni moja ya picha inayoonesha hali si shwari huko Barani Uropa kwani kila sehemu barabara hazipitiki kutokana na kujaa barafu. Safari za ndege na treni zimeahirishwa na hata mechi za ligi nazo zimepigwa stop.

ANGALIA MLIMANI TV, SIKILIZA MLIMANI RADIO

HIZI NI NEMBO ZINAZOWAKILISHA MLIMANI TV NA RADIO SAMBAMBA NA KAULIMBIU YAO YA ELIMU KWANZA
Hapa ni sina cha kusema bali nilitaka kukuonesha kwa ukweli nembo hizi zilivyo kwa yule ambaye hazifahamu. Hivi ni vyombo vya habari zinavyomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam chini ya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC).

PONGEZI ZA RAIS KIKWETE KWA ANNA ABDALLAH

PONGEZI BAADA YA KUPATA NISHANI KUTOKA BONDENI.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi Mama Anna Abdallah kwa kutunukiwa Nishani ya heshima na Serikali ya Afrika ya Kusini.

“Tuzo hiyo ni chachu na changamoto kwa viongozi na utendaji wao wawapo katika nafasi za kutumikia wananchi na pia ni ishara kubwa ya kuutambua mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika ya Kusini na Watu wake” Rais amesema.

Mama Anna Abdallah alipewa Tuzo ya Order of the Grand Companions of O.R Tambo, Silver na Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini.

Rais Kikwete amesema Mama Abdallah ameiwakilisha nchi na watu wake vyema na hivyo kuleta heshima kwa Taifa kwa ujumla.

CUF WADAI MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI

MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI HAYAKUSHIRIKISHA WADAU.

CUF – Chama cha Wananchi hatukuridhishwa na maamuzi ya kutoshirikishwa vyama vya siasa, pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kuonyesha haja ya kufanya marekebisho katika sheria ya Uchaguzi, sura 343 na sheria ya uchaguzi wa serikali za Mitaa sura ya 292 kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya Habari wiki hii.

Muswada huo unakusudia kuondoa mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza katika chaguzi zilizopita kwa lengo la kuiwezesha Tume kuendesha chaguzi kwa ufanisi.

CUF – Chama cha Wananchi tumesikitishwa na hatua hii iliyochukuliwa kwa kuandaliwa muswada pasipo kuwashirikisha wadau wakuu wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa vilivyosajiliwa kwa misingi halali .

CUF – Tunaamini kuwa nchi yenye serikali adilifu ni ile inayofanya maamuzi yake kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na utawala bora kwa kushirikisha walengwa na wadau ili kupata mawazo bora yatakayoboresha jambo husika kuliko kuwaamulia kwa utashi na matakwa ya waliopewa madaraka, kwani maamuzi hayo yanaweza yasiwe na tija wala siyo suluhisho la tatizo husika.

MESSI MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA DUNIA

LIONEL MESSI AKIKABIDHIWA TUZO YA UCHEZAJI BORA WA MWAKA WA DUNIA NA RAIS WA FIFA SEPP BLATTER

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina Lionel Messi amefanikiwa kutwaa tuzo ya uchezaji bora ya mwaka na kumshinda Cristiano Ronaldo. Messi ambaye ametwaa tuzo ya uchezaji bora wa Ulaya amepata kura 1,073, Ronaldo ameambulia 352, Xavi Hanandez za kwake 196, Ricardo Kaka amepata 190 na Andrea Iniesta amefunga tano bora kwa kura 134.

Sunday, December 20, 2009

SHAMBA LA MJINI UMELIONA?

MAZAO YOTE YANAPATIKANA KUANZIA MBOGA ZA MAJANI HADI MATUNDA.
Mjini kuna maeneo watu wanaishi kama kijijini kwetu kwani wanalima vizuri na mazo yao yanastawi vizuri. Mandhari kama hii ni nadra sana kuikuta mjini lakini kuna maeneo watu wanalima tena kila aina ya mboga utaikuta humu. Umekiona kisamvu hicho?

MAFUTA YA TRANSFOMA SIKU HIZI SIO DILI NINI?

TANESCO UMEPATA DAWA YA WEZI WA MAFUTA YA TRANSFOMA NINI?
Afadhali siku hizi kilio cha kuibwa kwa mafuta ya Trasfoma kimepungua kitu ambacho kimesaidia kuondokana na tatizo la watu kukaa giza kwa muda. Hivi Tanesco wamepata dawa ya kuzuia wizi huu au mafuta hayo si dili tena kwa sasa? Kama dawa imepatikana itakuwa kheri ili zoezi lisiwe la zima moto.

SAA KUMI NA MOJA NA NUSU ASUBUHI JIJINI

HIVI NDIVYO JIJI LA DARA ES SALAAM LINAVYOKIMBILIA WAKATI WA MAWIO.

Taswira hizi nimezinasa asubuhi wakati nawahi daladala nielekee job. Hapa ni Mabibo Mwisho sehemu ambayo kituo cha daladala kilipo. Magari hayo yanayoonekana kando ni wale wenzangu wenye usafiri halafu hawana sehemu za kulaza.

VIKWANGUA ANGA VYAONGEZEKA

MANDHARI YA MAENEO MBALIMBALI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA SASA INATAWALIWA NA VIKWANGUA ANGA
Ghorofa hili linapatikana Kituo cha Makumbusho pembeni ya lile la Dermo House kama ambavyo linaonekana chini.
Ghorofa la Dermo House linavyoonekana mapema asubuhi na sasa limeanza kuungwa mkono kutokana na kuibuka majengo mengine kama uyoga.

CHELSEA YAAMBULIA SARE

LIGI KUU NCHINI ENGLAND YAFIKA MAHALI PATAMU

Kiungo wa Chelsea Frank Lampard akipongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la kusawazisha katika mchezo wa ligi dhidi ya West Ham United. Matokeo mpaka dakika tisini zinamalizika yalikuwa 1-1.

MATOKEO BARCLAYS PREMIER LEAGUE - ENGLAND

KITIMUTIMU CHA LIGI KUU NCHINI ENGLAND KATIKA PICHA
MATOKEO YA MICHEZO YA BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Arsenal 3-0 Hull
Aston Villa 1-0 Stoke
Blackburn 0-2 Tottenham
Fulham 3-0 Man Utd
Man City 4-3 Sunderland
Portsmouth 2-0 Liverpool