SERIKALI IWE NA HURUMA NA MATUMIZI MABAYA YA KODI ZA WALALAHOI.
CUF – Chama cha Wananchi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Gavana wa Benki Kuu
CUF – Tunaungana na Watanzania wengine wote wenye uchungu, waliotoa vilio vyao juu ya ufujaji huu wa mapesa hali Taifa letu likikabiliwa na tatizo la njaa, upungufu wa madawa katika Zahanati, ukosefu wa vifaaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule zetu za sekondari hususani hizi za kata.
CUF – Chama cha wananchi tunaimani serikali yenye viongozi makini ni ile inayotoa vipaumbele vyenye maslahi na Taifa kwa sasa na baadaye, kwani uapoboresha elimu unajenga msingi mzuri wa kuzalisha wataalamu wengi bora wa baadae ambapo utakuwa na wenye uwezo wa Ugavana wengi, Wahandisi wengi na Madaktari wakutosha .
CUF - Tunawatanabaisha Watanzania kuwa makini na kuzinduka na viongozi wa serikali ya Mapinduzi kwani wapo kwa ajili ya maslahi yao na familia zao, na hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuwajibisha nyingine kwani kila mamlaka imeoza, hivyo ni jukumu lao wananchi kuhakikisha serikali iliyopo madarakani hairudi tena katika uchaguzi ujao wa 2010.