Tuesday, June 22, 2010

WAKULIMA WA KAHAWA MBINGA WALILIA FIDIA ZAO!!!

Wakulima wa kahawa walio katika Umoja wa wakulima wa Kahawa Spesheli (KILICAFE) wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma wamedai kuwa mpaka sasa hawajapata malipo yoyote yatokanayo na fidia iliyotangazwa na serikali kwa wakulima wa kahawa ambao waliopatwa na hasara ya kuanguka kwa bei ya kahawa katika Soko la kimataifa.

Wakulima hao ambao hoja yao imewasilishwa na mwenyekiti wa Bodi ya Wakulima wa kahawa Spesheli KILICAFE Philemoni Haule katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Umoja huo.

Hoja hiyo imetolewa kwa kuzingatia maelezo ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 21 na milioni 900 kwa ajili ya kuwafidia wakulima walioathirika na anguko la bei ya kahawa katika soko la kimataifa.

Pembezoni mwa mkutano huo Mwenyekiti Haule amesema anguko la bei ya kahawa lilitokea mwaka jana limesababisha madhara makubwa kwa wakulima wake ambao baadhi wamenyang’anywa dhamana zao kutoka kwa taasisi za fedha walikokopa pembejeo na wengine wamepoteza uaminifu na waliokuwa wakifanya nao biashara.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa imelazimu ununuzi wa kahawa uminye mirija katika msimu huu ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutisha Uhai wa Mkakati Mzima wa KILICAFE wa kuwasaidia wakulima

Wakulima wa kahawa walio katika Umoja wa wakulima wa Kahawa Spesheli (KILICAFE) wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma wamedai kuwa mpaka sasa hawajapata malipo yoyote yatokanayo na fidia iliyotangazwa na serikali kwa wakulima wa kahawa ambao waliopatwa na hasara ya kuanguka kwa bei ya kahawa katika Soko la kimataifa.

Wakulima hao ambao hoja yao imewasilishwa na mwenyekiti wa Bodi ya Wakulima wa kahawa Spesheli KILICAFE Philemoni Haule katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Umoja huo.

Hoja hiyo imetolewa kwa kuzingatia maelezo ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 21 na milioni 900 kwa ajili ya kuwafidia wakulima walioathirika na anguko la bei ya kahawa katika soko la kimataifa.

Pembezoni mwa mkutano huo Mwenyekiti Haule amesema anguko la bei ya kahawa lilitokea mwaka jana limesababisha madhara makubwa kwa wakulima wake ambao baadhi wamenyang’anywa dhamana zao kutoka kwa taasisi za fedha walikokopa pembejeo na wengine wamepoteza uaminifu na waliokuwa wakifanya nao biashara.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa imelazimu ununuzi wa kahawa uminye mirija katika msimu huu ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutisha Uhai wa Mkakati Mzima wa KILICAFE wa kuwasaidia wakulima kupata Bei nzuri za kahawa na kuendeleza zao hilo

Wakati Malipo ya fidia ya wakulima wa kahawa yaliyoahidiwa na serikali yakiwa kizungumkuti, Mkurugenzi wa Mtendaji wa KILICAFE Geofrey Mwangulumbi ametamba kupata mafanikio makubwa tangu ianze kuwahudumia wakulima wa kahawa, ambao walioanza katika vikundi kumi na sasa vipo vikundi 217 vyenye wakulima 12,149.

Anasema KILICAFE imejihakikishia kupata kahawa bora kutoka kwa wakulima hao kwa kuwa imewawezesha mitambo ya kumenyea kahawa 116 na imejenga maghala ya uhakika hali iliyowezesha kuinua ubora wa kahawa ya wakulima wake kutoka daraja la kumi hadi daraja la nne.

Wakulima wa Mbinga Mkoani Ruvuma ndio wanufaika wakubwa wa harakati za KILICAFE kuinua mapato ya kahawa kutokana na kuzalisha kahawa nyingi kwa kiwango cha hadi kufikia tani 9700 kwa msimu mmoja, na ni wilaya hii yenye vikundi 159 kati ya vikundi vyote 217 vya KILICAFE Nchi nzima    kupata Bei nzuri za kahawa na kuendeleza zao hilo

Wakati Malipo ya fidia ya wakulima wa kahawa yaliyoahidiwa na serikali yakiwa kizungumkuti, Mkurugenzi wa Mtendaji wa KILICAFE Geofrey Mwangulumbi ametamba kupata mafanikio makubwa tangu ianze kuwahudumia wakulima wa kahawa, ambao walioanza katika vikundi kumi na sasa vipo vikundi 217 vyenye wakulima 12,149.

Anasema KILICAFE imejihakikishia kupata kahawa bora kutoka kwa wakulima hao kwa kuwa imewawezesha mitambo ya kumenyea kahawa 116 na imejenga maghala ya uhakika hali iliyowezesha kuinua ubora wa kahawa ya wakulima wake kutoka daraja la kumi hadi daraja la nne.

Wakulima wa Mbinga Mkoani Ruvuma ndio wanufaika wakubwa wa harakati za KILICAFE kuinua mapato ya kahawa kutokana na kuzalisha kahawa nyingi kwa kiwango cha hadi kufikia tani 9700 kwa msimu mmoja, na ni wilaya hii yenye vikundi 159 kati ya vikundi vyote 217 vya KILICAFE Nchi nzima. (Habari kwa hisani ya Gerson Msigwa)  

No comments:

Post a Comment