Thursday, June 24, 2010

HENRY KUKUTANA NA SARKOZY!!


Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Les Blues Thierry Henry anatarajiwa kukutana na Rais wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy kwa ajili ya kueleza sababu za wao kuondoshwa mapema katika Mchuano wa Kombe la Dunia unaoendelea nchini Afrika Kusini. Maelewano ndani ya Kambi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa yalitoweka baada ya kufukuzwa kwa Mshambuliaji Nicolas Anelka baada ya kumrushia maneno makali Raymond Domenech!!

No comments:

Post a Comment