Wednesday, June 30, 2010

FEDERER AONDOLEWA WIMBLEDON!!


Bingwa mara sita wa taji la Wimbledon Roger Federer ameondolewa kwenye kinyang'anyiro baada ya kufungwa na Tomas Berdych kwa seti3-1 kwa matokeo ya 6-4 3-6 6-1 6-4. Ndiyo hivyo mkongwe ameiabishwa na kijana mdogo kwenye fani!!!

MAN CITY YAKUBALIANA NA DAVID SILVA!!!


Klabu ya Manchester City imefanya mazungumzo na Valencia kwa ajili ya kumnasa Mshambuliaji wake David Silva kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Tayari masuala yote yameshakamilika na kilichosalia ni kwa mchezaji huyo kupimwa afya yake tu!!!

KAMPENI ZAZIDI KUSHIKA KASI KWA WABUNGE!!!

Mbunge wa Mbinga Magharibi, mkoa wa Ruvuma, Kapteni John Komba amewaomba wananchi wa jimbo lake kumfilisi fedha zote kwa ajili kutatua matatizo yao na kwamba hateteleki na wagombea wanaojitokeza kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.

Kapteni Komba ameyasema hayo huku akijihakikishia kwa asilimia 100 kwamba amefanikiwa kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu, maji, afya, miundombinu ya barabara na mengineyo.

Akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali katika jimbo hilo hivi karibuni ambalo kwa sasa limepewa jina la wilaya ya Ziwa Nyasa, Kepten Komba amewaambia wananchi hao kuwa bado ana kiu ya kutaka kuendelea kuwasaidia.

Amesema kuwa mafanikio makubwa waliyoyapata hadi sasa yanatokana na jitihada zake binafsi na kwamba ana kiu ya kuendelea kuwasaidia huku akijinadi kuwa Mungu hakukosea kuwapa chaguo lake.

Hata hivyo amesema wanasiasa wanaojitokeza kugombea nafasi hiyo katika jimbo la Mbinga Magharibi hawana nguvu ya kushindana naye kwani wananchi bado wana imani naye kutokana na kufanikiwa kuleta mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi cha miaka mitano.

Aidha, amewaasa wapiga kura wake kuwaogopa kama ukoma wanasiasa wanaotaka madaraka kwa kigezo cha kutumia ukabila kwani wamepitwa na wakati hivyo wametakiwa kuchagua kiongozi makini ambaye ana uwezo wa kuleta maendeleo mbalimbali pamoja na kupiga vita umaskini.

Amewataka wananchi wakati wa kupiga kura utakapofika wamchague tena ili aweze kumalizia kazi ambazo alikuwa amezianzisha katika harakati za kuwasaidia kuondokana na kero zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

Jumla ya wagombea Wanne ndiyo waliojitokeza kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Mbinga magharibi hadi sasa akiwemo Bw. Stanley Vumu, Bw. Alex Shauri na wengine waliotambulika kwa majina ya Bw. Haule na Bw. Mangwea. (Habari na Mdau Emmanuel Msigwa)

WAFANYABIASHARA WALIA NA TRA SONGEA!!!

WAFANYABIASHARA mbalimbali katika Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, wamesema watamwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kulalamikia kitendo cha serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwalazimisha kulipa kodi kubwa inayosababisha biashara zao kufa.

Aidha, wamesema watamwandikia Rais Kikwete kuikataa sheria mpya ya ukusanyaji kodi kupitia mfumo mpya wa kudhibiti mapato kwa kutumia mashine maalumu ya Electronics kwa madai hauna manufaa kwa wananchi na umelenga kushibisha matumbo ya wachache.

Wafanyabiashara hao wameyasema hayo jana wakati wa mkutano ulioandaliwa na TRA mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwafahamisha wafanyabiashara juu ya mfumo mpya wa kudhibiti mapato kwa kutumia mashine hizo.

Wamesema wamechoshwa na vitendo vya serikali kupitia mamlaka hiyo kwa kuwachezea rafu mara kwa mara katika kutimiza malengo yao ya kukusanya kodi kwani wamekuwa wakiwakadiria kodi kubwa bila kuangalia hali ya biashara zao ina nguvu kiasi gani.

Wamesema wamefikia hatua hiyo kutokana na TRA mkoani humo kudai kuwa wanatekeleza sheria na maagizo yaliyotolewa na serikali hivyo hata kama mkoa umepangiwa kodi kubwa ni lazima ipigane kufa na kupona ili kutimiza lengo lao.

John Rupia amesema amesena kama serikali ndiyo inayotumika kuwanyonya wananchi wake basi watamwamndikia barua Rais Kikwete kulalamikia suala hilo wakidai kuwa unasababisha biashara zao kufa kutokana na kulipa kodi kubwa.

Aidha, kwa upande wa mashine hizo Bw. Rupia amesema zimeletwa kwa ajili ya kushibisha matumbo ya wachache kwa madai kuwa upo uwezekano wa kuuziwa bei kubwa hata kama bei yake ni ndogo.

Ameeleza kuwa wana wasiwasi na mtiririko wa kuuziwa mashine hizo kwani unaonesha wazi kuwa una mianya ya kuwanufaisha baadhi ya watu huku wakitilia mashaka makampuni yaliyopewa kazi ya kusambaza mashine hizo kwa wafanyabiashara.

Kwa mujibu wa Ofisa wa TRA mkoa wa Ruvuma kitengo cha utoaji elimu kwa mlipa kodi, Msetti Jackson, mashine hizo zinauzwa kuanzia milioni Moja hadi Tano na kwamba makampuni yaliyopewa tenda ya kusambaza mashine hizo yapo Sita tu.

Amesema makampuni hayo yatasambaza na kutoa elimu kwa wauzaji wa maduka yaliyosajiriwa na VAT namna ya kuzitumia huku akitaja sifa lukuki za mashine hizo katika kudhibiti mapato ikiwemo ya utunzaji wa kumbukumbu kwa miaka Mitano na kwamba imeunganishwa mtandao moja kwa moja na TRA. (Habari na Emmanuel Msigwa)

Tuesday, June 29, 2010

MASHABIKI WAPENDEZA!!!




Mashabiki wakiendelea kuzishangilia timu zao kwenye kinyang'anyiro cha Woza 2010 kinachoendelea nchini Afrika Kusini kwa sasa!!!

WOZA 2010 - SPAIN NA PARAGUAY ZAFUZU ROBO FAINAL!!!











Timu ya Taifa ya Spain ilikuwa timu ya mwisho kuweza kufuzu katika hatua ya Robo fainal baada ya kuifunga Ureno kwa goli moja kwa nunge wakati mpambano wa mapema ukishuhudia Paraguay ikiiondosha Japan kwa mikwaju ya penalty baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare tasa. Timu hizi mbili yaani Spain na Paraguay zinatarajia kuumana kwenye hatua ya Robo fainal!!!

BARABARA YA SONGEA NAMTUMBO YAIVA SASA!




Mkurugenzi wa Miradi ya Usafirishaji Kitengo cha Miradi ya Millennia Wizara ya Fedha na Uchumi Salum Sasillo (Kulia) akimkabidhi David Curtarello kutoka kampuni ya Sogea Satom Tanzania mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 67 kwa kiwango cha lami kutoka Songea hadi Namtumbo mbele ya wananchi wa kijiji cha Lumecha wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika baada ya miezi 27 na kutumia zaidi ya bilioni 70.(Taarifa kutoka kwa mdau Emmanuel Msigwa)

BLATTER AOMBA RADHI KWA MADUDU YA WAAMUZI!!!



Rais wa Shirikisho la Kabumbu Duniani FIFA Sepp Blatter ameziomba radhi England na Mexico kwa makosa ambayo yametokea kwenye Kombe la Dunia. Blatter amekiri goli la Frank Lampard lilikuwa halali huku pia goli lililofungwa na Carlos Tevez akikiri ilikuwa ni offside!!!

HENRY NA TOURE KUONDOKA BARCELONA!!


Timu ya Barcelona imethibitisha kuondoka kwa wachezaji wake wawili. Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ufaransa Thierry Henry pamoja na Kiungo wa Kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure. Wakati Henry akielezwa yupo njiani kujiunga na Major League Soccer ya nchini Marekani mwenzake Toure anakwenda kuungana na ndugu yake katika Klabu ya Manchester City!!!

Monday, June 28, 2010

MASHABIKI WAKIJINADI MITAANI!!!





Mashabiki wa Timu za Taifa wakiwa wamejipamba kwa rangi za bendera za nchi zao ikiwa ni ishara ya uzalendo walionao wakati timu zao zinashuka dimbani!!!

FEDERER, NADAL NA MURRAY WATINGA ROBO FAINAL!!!





Roger Federer ametinga robo fainal baada ya kumfunga Jurgen Melzer kwa 6-3, 6-2 na 6-2 huku Rafael Nadal akifuzu baada ya kumfungaPaul-Henri Mathieu kwa 6-4, 6-2 na 6-2 wakati Andy Murray akimshinda Sam Querrey kwa 7-5, 6-3 na 6-4!!!!

SERENA ATINGA ROBO BAADA YA KUMUONDOSHA SHARAPOVA!!



Bingwa Mtetezi wa Taji la Wimbledon upande wa Wanawake Serena Williams amefanikiwa kuvuka kizuizi chake cha kwanza baada ya kumuondosha Maria Sharapova na kutinga hatua ya Robo fainal kwa ushindi wa 7-6 na 6-4!!

BRAZIL, HOLLAND KWENYE ROBO FAINAL!!!












Timu ya Taifa ya Brazil Samba Kings imefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainal baada ya kuichakaza Chile kwa magoli matatu kwa buyu huku mapema Holland ikikata tiketi baada ya kuiondosha Slovakia kwa kichapo cha magoli mawili kwa moja!!

NDOTO ZA ENGLAND ZILIPOPOTEA BAADA YA GOLI LAO KUKATALIWA!!




Tayari Timu ya Taifa ya England imeanza kupigia debe teknolojia ya kuamua magoli yenye utata baada ya kujikuta ikinyimwa goli lao halali dhidi ya Ujerumani. England walikataliwa goli lao ambalo huenda lingekuwa la kusawazisha kwa timu hiyo baada ya Frank Lampard kupiga mkwaju uliovuka goli lakini waamuzi wakashindwa kulikubali. Baada ya pigo hilo wameanza kampeni za kutaka kutumika teknolijia katika kuamua magoli yenye utata!!!

Sunday, June 27, 2010

HEKA HEKA ZA KOMBE LA DUNIA!!!


Vijana wa Songea wakihaha kuhakikisha hawapitwi na mitanange ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Afrika Kusini. Kwa sasa imefikia hatua ya mtoano huku timu nne zikiwa zimefuzu katika hatua ya Robo fainal. Picha hii imenaswa na mdau Emmanuel Msigwa akiwa kwenye harakati zake huko Songea!!!

STENDI YA SONGEA IKIWA KATIKA HALI MBAYA!!!



Hii ndiyo hali halisi ya Stendi Kuu ya Mabasi ya Songea ilivyo. Kwa ujumla hali yake inatisha kwani mazingira yake ni mabaya sana huku hata barabara zinazoingia hapo zikiwa katika hali mbaya. (Picha kwa Hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)

WILAYA MPYA YA ZIWA NYASA MKOANI RUVUMA!!!






Matukio mbalimbali Mkoani Ruvuma wakati harakati za Wilaya mpya ya Ziwa Nyasa Mkoani Ruvuma ambapo Mbunge wa Mbinga Kapteni Mstaafu John Komba alikuwepo kwenye shughuli hiyo!!! (Picha kwa Hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)