Thursday, May 6, 2010

MAZISHI YA RAIS YAR'ADUA!!!!






Wakuu wa Jeshi la Nigeria wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu Rais Alhaj Umar Yar'Adua ambaye amezikwa katika eneo la Katsina nchini humo!! Mwili huo ulisafirishwa kwa ndege baada ya watu kupata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi huyo!!!

RAIS GOODLUCK JONATHAN AKIAPISHWA!!


Rais mpya wa Nigeria Goodluck Jonathan akiapishwa rasmi kushika madaraka ya kuliongoza taifa hilo kufuatia kifo cha Rais Umar Yar'Adua!!

RAIS MPYA WA NIGERIA GOODLUCK JONATHAN!!!


Rais mpya wa Nigeria ameapishwa rasmi saa kadhaa kabla ya kuzikwa kwa Alhaj Umar Yar'Adua. Kaimu Rais wa Taifa hilo Jonathan Goodluck ameapishwa kuchukua nafasi ya marehemu Yar'Adua!!!

CUF YATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA NIGERIA!!

CUF- Chama Cha Wananchi, tumepokea kwa masikitiko makubwa habari za msiba wa Rais wa Nigeria Umar Yar'Adua hivyo tunatoa pole kwa Wananchi wa Nigeria.

Rais Umar Yar' Adua alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Wanaigeria wanafikia malengo yao ya Maendeleo na kuwa na Amani ya Kudumu katika nchi yao. Pia alihakikisha anayafanyia kazi mambo matatu muhimu kwa Wanaigeria ambayo ni kushughulikia Rushwa na Ufisadi uliokithiri nchini humo, pili kuhakikisha Nigeria inakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi itakayo tenda haki kwa watu wote na jambo la tatu ni kuhakikisha Nigeria inakuwa na amani ya kudumu kwa kukubaliana na Waasi hasa katika maeneo ya mafuta.

CUF - Pamoja na kumtakia kila la kheri Rais mpya aliyeapishwa Goodluck Jonathan ambaye alikuwa ni Makamo wa Rais, lakini pia ni matarajio yetu kuwa atahakikisha anaifanyia kazi na kuiendeleza mipango na malengo mazuri aliyoyaacha Marehemu Umar Yar' Adua, na kuhakikisha anaondoa ubaguzi wa aina yoyote na kuleta umoja na mshikamano kwa Wanigeria.

CUF- tunatarajia kuwa Wanaigeria watakuwa na utulivu wa hali ya juu katika kipindi hiki cha majonzi hasa kwa kuzingatia Nigeria ni nchi yenye watu wengi Barani Afrika hivyo kuwa ni mojawapo ya Nchi yenye Uchumi ulio juu ikilinganishwa na baadhi ya nchi nyingine.

Mungu amlaze mahali pema peponi Marehemu Umar Yar' Adua, Amin!!

RAIS YAR'ADUA AFARIKI DUNIA!!!


Rais wa Nigeria Alhaj Umar Yar'Adua amefariki na kuzikwa kijijini kwake baada ya kuwa mgonjwa kwa muda wa miezi karibu saba! Kiongozi huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 59 alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo na Ini! Mwenyezimungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!

ODINGA ATEMA CHECHE!!!

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema ili Bara la Afrika lipate maendelea lazima liepuke utegemezi kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Waziri Mkuu Odinga amesema imefika wakati kwa Bara la Afrika kuanzisha vitegauchumi vyake kwa kutegemea rasilimali zilizopo barani humu.

Aidha Waziri Mkuu Odinga amesema licha ya changamoto ya miundombinu katika bara la Afrika bado inayonafasi ya kutengeneza miundombinu ili kujiletea maendeleo ya haraka.

Amesema moja ya nyenzo muhimu katika maendeleo ni miundombinu ambapo wawekezaji wengi wamekuwa wakiogopa kuwekeza katika Bara la Afrika kwa kuhofia ubovu wa miundombinu.

"Tukiwekeza kwenye miundombinu ya barabara,umeme,reli,mawasiliano tutakuwa tumepiga hatua kubwa kimaendeleo kwani hakuna mwekezaji anayewekeza kwenye miundombinu mibovu."

Odinga amesema kwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru wa bara la Afrika nchi nyingi hazijapiga hatua ya maendeleo kutokana na uongozi mbovu na kusema kuwa kwa sasa demokrasia inachukiua mkondo wake.

Ametolea mfano wa Kenya katika suala la demokrasia kuimarika amesema nchi yake imekuwa mfano wa kuigwa kwa kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na amesema kuanzia siku 90 katiba hiyo mpya itakuwa imekamilika na kutawanywa kwa wananchi.

"Hivi sasa demokrasia katika nchi nyingi za Afrika ni nzuri japo kwa mfano Kenya marekebisho ya katiba yatakamilika siku tisini kuanzia leo na kutawanya kwa wananchi".

Wednesday, May 5, 2010

SILVA AITAMANI MAN UTD!!!!


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Spain ambaye anasukuma gozi katika Klabu ya Valencia David Silva ameweka bayana anaitamani Klabu ya Manchester United na kama itaweza kumudu dau lake hawezi kukataa kujiunga nao! Mshambuliaji huyo amesema ni wazi duniani kwa sasa kila mchezaji anatamani kucheza Ligi ya England na hasa Klabu kama Manchester United!!!!

WENGER BADO YUPO YUPO SAANAAA!!!!


Kocha Mkuu wa Klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesaini mkataba ambao utamuwezesha kuendelea kukinoa kikosi hicho kilichosheheni Ndama hadi mwaka 2013. Wenger ambaye amekuwa akilaumiwa kutokana na kuendekeza sera yake ya kutumia wachezaji chipukizi atakuwa na jukumu la kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa ambao umekuwa historia kwa miaka zaidi ya mitatu sasa!!!!

CUF WAMGEUKIA WAZIRI GHASIA!!!!

CUF – Chama cha Wananchi tumeshangazwa na kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia katika moja ya chombo cha habari nchini, kuwa chama chetu ndio chanzo cha kushawishi “Sakata lililoandaliwa la Mgomo wa Wafanyakazi nchini”.

Akizungumza na chombo hicho cha habari, ambacho jina lake tunalo alisema kuwa Chama cha CUF ndio chanzo cha uchochezi kwa Wafanyakazi kupitia taasisi yao ya TUCTA kupanga mgomo ambao Rais Jakaya Kikwete ameshautolea Tamko kuwa ameupiga marufuku, atakegoma atafukuzwa kazi, na atakaeandamana kukiona cha moto.

CUF – Chama cha Wananchi tunamuelimisha Waziri Hawa Ghasia kuwa Chama chetu ni cha siasa na kipo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wote Tanzania na kukemea vitendo vyovyote vya udhalilishaji, ukiukaji wa haki za binadamu, ubakaji wa demokrasia nchini, ubadhirifu, ufisadi na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani na uchochezi nchini.

CUF – Tunawatanabahisha Watanzania kuwa makini na Viongozi wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwamba wapo kwa ajili ya maslahi yao na kulindana, badala ya kuwatumikia wananchi waliowachagua wakiwemo Wakulima, Wafanyabiashara na Wafanyakazi.

MADIWANI WAGEUKA MBOGO!!!

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wameilalamikia kamati ya idara ya mipango miji katika Manispaa hiyo kwa kushindwa kusimamia kazi zake vizuri.

Madiwani hao wametoa lawama hizo huku wakilitaka pia baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kutoa tamko rasmi la kumuondoa mkuu wa Idara ya Mipango miji katika manispaa hiyo, Christian Mkude na kumtafuta mtu mwingine wa kushika nafasi hiyo kwa madai kuwa aliyopo sasa anashindwa kufanya kazi yake ipasavyo.

Hatua hiyo imefikiwa jana na Madiwani hao katika baraza lao la madiwani mara baada ya kumtaka Mwenyekiti wa kamati ya idara ya mipango miji, Christian Matembo kutoa maelezo ya kushindwa kusimamia vyema mpango wa ujengaji wa barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea kufanyika mjini hapa.

Madiwani hao wamedai kuwa barabara zinazoendelea kujengwa mjini hapa kwa kiwango cha lami zipo katika kiwango duni licha ya kutumika fedha nyingi hali ambayo imepelekea kuwepo kwa malalamiko mengi ya wananchi kuhusu barabara hizo.

Golden Sanga Diwani wa Kata ya Bombambili Mjini ameishia kuishutumu kamati pamoja na idara hiyo ya mipango miji kwa kushindwa kusimamia kazi yake ipasavyo huku akiwatupia lawama moja kwa moja watalaamu kwa madai kuwa kazi wanayoifanya haikidhi mahitaji.

Amesema watalaamu wameshindwa kufanya kazi yao kwa ufanisi hali ambayo imesababisha pia barabara zingine mifereji kujengwa juu na barabara ipo chini hali ambayo inasababisha wakati wa mvua maji kupita juu ya barabara badala ya kwenye mifereji.

Akitoa hoja za kujitetea Mwenyekiti wa Kamati ya Idara ya Mipango Miji, Matembo amedai kuwa wanashindwa kufanya kazi yao vizuri kutokana na Mkuu wa Idara hiyo Bwana Mkude kutoshiriki katika mikutano ya baraza hilo la madiwani hivyo kushindwa kushauriana na kufikia muafaka.

Bwana Matembo amesema kila mkutano unapofika mkuu huyo wa idara ya mipango miji amekuwa akimtuma mwakilishi hivyo akaliomba baraza hilo kutamka rasmi kumtafuta mtu mwingine wa kushika nafasi hiyo.

Awali Mhandisi wa Manispaa ya SONGEA, Maximillian Kabairuka amekiri kuwepo kwa mapungufu katika kusimamia miradi hiyo ya barabara huku akilihakikishia baraza hilo kuwa barabara zinazojengwa ni bora na kwamba zitatumika bila kuharibika kwa muda wa zaidi ya miaka 10 hadi 15.

Akifunga baraza hilo la Madiwani, Meya wa Manispaa ya Songea, Gerald Ndimbo amesema baraza hilo linaagiza kuwa barabara hizo zifanyiwe marekebisho ya haraka hadi ifikapo Juni mwaka huu ili ziwe katika kiwango kinachotakiwa vinginevyo itamyang’anya kazi mkandarasi na kumchukulia hatua zaidi.( Habari kwa Hisani ya Emmanuel Msingwa)

Tuesday, May 4, 2010

TORRES KUKOSA MECHI ZA MWANZO ZA WORLD CUP!!!



Mshambuliaji wa Kimataifa wa Spain ambaye anasukuma gozi katika Klabu ya Liverpool Fernando Torres El Nino yupo mashakani iwapo ataweza kucheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia. Torres ambaye amefanyiwa operesheni imeelezwa kuwa uwezekano wa yeye kucheza ni mdogo sasa!!

KIKOSI CHA ALGERIA CHA WORLD CUP!!!


Goalkeepers: Lounes Gaouaoui (ASO Chlef), Faouzi Chaouchi (Entente Setif), Mohamed Lamine Zemmamouche (MC Alger), M'bohi Rais Ouheb (Slavia Sofia, Bulgaria)

Defenders: Abdelkader Laifaoui (Entente Setif), Madjid Bougherra (Rangers, Scotland), Carl Medjani (Ajaccio, France), Rafik Halliche (Nacional Madeira, Portugal), Anther Yahia (Bochum, Germany), Habib Belaid (Boulogne-sur-Mer, France), Nadir Belhadj (Portsmouth, England), Djamel Mesbah (Lecce, Italy)

Midfielders: Hassan Yebda (Portsmouth, England), Medhi Lacen (Racing Santander, Spain), Yazid Mansouri (Lorient, France), Adlene Guedioura (on loan at Wolverhampton, England from Charleroi, Belgium), Riad Boudebouz (Sochaux, France), Djamel Abdoun (Nantes, France), Fouad Kadir (Valenciennes, France), Mourad Meghni (Lazio, Italy), Karim Ziani (Wolfsburg, Germany), Karim Matmour (Borussia Moenchengladbach, Germany)

Strikers: Abdelkader Ghezzal (Siena, Italy), Rafik Djebbour (AEK Athens, Greece), Rafik Saifi (Istres, France)

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA WAZEE!!!

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA
DAR ES SALAAM, TAREHE 3 MEI 2010

Mhe. Makamu wa Rais,
Mhe. Waziri Mkuu,
Waheshimiwa Mawaziri,
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,
Mstahiki Meya,
Viongozi wa Serikali,
Wazee wangu,
Ndugu Wananchi,

Nianze kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuniandalia fursa ya kukutana na Wazee wa Dar es Salaam. Nawashukuru wazee wangu kwa kuitikia wito wangu huu wa kukutana nanyi na nimefarijika sana kwa mahudhurio yenu makubwa. Asanteni sana.

Nimewaiteni wazee wangu nizungumze nanyi mambo mawili na kupitia kwenu nizungumze na wananchi wote wa Tanzania. Jambo la kwanza, linahusu mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu masuala ya uchumi utakaofanyika hapa Dar es Salaam kuanzia keshokutwa tarehe 5 Mei mpaka tarehe 7 Mei. Mkutano huo ulioandaliwa na shirika moja la kimataifa lijukanalo kama World Economic Forum, lenye makao yake makuu nchini Uswisi, unafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 20 ya mikutano hiyo kufanyika Barani Afrika. Pia ni mara ya kwanza kwa mikutano hiyo kufanyika nje ya Cape Town, Afrika Kusini.

Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu,

Hii ni heshima kubwa sana ambayo taifa letu limepewa. Ni kielelezo cha imani kubwa waliyokuwa nayo kwetu, wenzetu kwingineko duniani, kwani zilikuwepo nchi nyingine zilizotaka kuwa wenyeji wa mkutano huu lakini wakaiteua Tanzania. Ni jambo la fahari kwetu lakini ni jambo ambalo pia lina wajibu mkubwa kwetu. Wajibu wenyewe si mwingine bali ni ule wa kuwapokea vizuri na kuwa wakarimu kwa wageni wetu kama ilivyo desturi yetu na sifa yetu Watanzania. Lazima tuhakikishe kuwa wageni wetu wanaondoka nchini wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na sisi watu wake.
Ndugu Wananchi,

Mwitikio wa watu kushiriki katika mkutano huu wa Dar es Salaam umekuwa mkubwa sana hata kuwashangaza waandaaji. Wanasema wameshaandaa mikutano hii kwa zaidi ya miaka 50 sasa, lakini hawajapata mwitikio kama huu wa mkutano wa Tanzania. Walikuwa na lengo la kupata washiriki 750, lakini mpaka tarehe 29 Aprili, 2010 washiriki 959 walikuwa wamethibitisha kushiriki na wengine kadhaa wamekosa nafasi. Haya yote ni kielelezo cha kukubalika na kuheshimika kwa nchi yetu kimataifa.

Ndugu Wananchi;

Tunatarajia kupokea Wakuu wa Nchi na Serikali wapatao, 11 na Mawaziri 23 wa kutoka nchi mbalimbali duniani. Aidha, wajumbe kutoka mashirika makubwa ya kimataifa, kama Umoja wa Kimataifa, Benki ya Dunia, WTO n.k. Kuna washiriki kutoka makampuni makubwa, ya kati na madogo ya kimataia na watu binafsi wakiwemo watu mashuhuri duniani. Washiriki wa mkutano huu kwa ujumla wao wanatoka katika mataifa 85 duniani. Katika mikutano hii hufanyika mikutano ya Viongozi Vijana wanaoongozwa na Mwana wa Mfalme wa Norway, Prince Magnus Haakon. Mkutano huo nao umevunja rekodi ya ushiriki, awali walitegemea washiriki 200 lakini washiriki waliothibitisha mpaka sasa ni 350. Kwa sababu ya ugeni mkubwa kiasi hiki, kutatokea usumbufu wa magari kusimamishwa ili kuruhusu misafara ya wageni wetu kupita. Naomba ndugu zangu muelewe hilo na kuwa wavumilivu. Natanguliza kuwataka radhi kwa usumbufu mtakaoupata katika siku tatu za mkutano huu.

Agenda kubwa ya mkutano wa mwaka huu ni kuangalia jinsi ya kurekebisha na kukuza uchumi wa nchi za Afrika baada ya kutikiswa na hali mbaya ya uchumi duniani. Masuala yatakayoongelewa ni pamoja na jinsi ya kuongeza uwekezaji; kukuza uzalishaji na tija kwenye kilimo; uwekezaji kwenye viwanda na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za kilimo; kuendeleza sekta binafsi ili iweze kuchangia kwenye ukuzaji wa uchumi; kuboresha miundombinu; kuendeleza elimu n.k.

Kwa ujumla mkutano huu ambao miaka ya nyuma umekuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini una faida kwa nchi yetu. Faida kubwa ni kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake duniani na hivyo kuwafanya wawekezaji na watalii watambue uwepo wetu. Wapo watakaoijua Tanzania kwa kufika na kujionea wenyewe na wapo watakaoijua nchi yetu kupitia vyombo vya habari ambavyo vitawakilishwa kwa wingi sana. Faida itakayopatikana haraka sana wakati na baada ya mkutano huu ni mahoteli na vyombo vya uchukuzi na maduka nchini kupata kipato kutokana na wageni watakaohudhuria mkutano huu kutumia huduma hizo. Naambiwa karibu wageni wetu wote wa nje watatembelea mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar baada ya mkutano.


Ndugu Wazee na Viongozi,

Jambo la pili linahusu TUCTA na mgomo. Sikupenda kulizingumzia suala hili, lakini nimelazimika kuzungumza baada ya kuwasikiliza viongozi wa TUCTA wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi hivi majuzi. Nimewasikia wakirudia kuwashawishi wafanyakazi kugomo kuanzia tarehe 5 Mei, 2010 kwa sababu ati sisi katika Serikali hatusikii wala hatujali maslahi ya wafanyakazi.

Katika hotuba yangu niliyoitoa mwishoni mwa mwezi Machi, 2010, nilielezea kwa kirefu jinsi gani Serikali inavyowathamini na kuwajali wafanyakazi. Nilitaja na kufafanua kwa kina hatua mbalimbali ambazo Serikali imechukua na inazoendelea kuchukua katika kuboresha maslahi ya mfanyakazi. Nilisema kuwa madai ya viongozi wa TUCTA kuwa Serikali hii siyo sikivu na haiwajali wafanyakazi si kweli kwani mema yote tuliyoyafanya kwa wafanyakazi hayangefanyika kama sisi hatusikii wala kujali.

Kadhalika nimeelezea dhamira yetu ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi katika bajeti ijayo. Ukweli ni kwamba tangu tuingie madarakani, tumeongeza kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 62.5 kutoka shilingi 65,000 hadi kufikia shilingi 104,000 hivi sasa.

Nilielezea pia mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali kuendeleza maslahi ya wafanyakazi wa sekta binafsi. Taliziunda Bodi nane za kisekta ambazo hazikuwepo kabla ili ziweze kushughulikia kupanga viwango vya mishahara ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi. Kwa ajili hiyo, wafanyakazi wa sekta binafsi wameanza kunufaika kwa mishahara kupanda tangu wale wa mashambani na majumbani mpaka viwandani na kwingineko. Hivi majuzi tena kumetolewa nyongeza nyingine, wapo ambao wametoka kwenye shilingi 45,000 mpaka shilingi 80,000 au hata 150,000, wapo waliotoka kwenye mshahara wa shilingi 48,000 kwa mwezi hadi shilingi 350,000 kwa mwezi mwaka 2009. Bodi hizi zinafikia maamuzi haya kwa kuzingatia uwezo wa sekta binafsi kumudu gharama hizo.

Ndugu Wananchi;

Jambo kubwa nililowaomba viongozi wa TUCTA ni kwamba, katika hotuba ya Machi, 2010 niliwasihi viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kutumia njia ya mazungumzo kwa sababu ilikuwa bado haijatumika na kushindikana. Aidha, nilikumbusha kuwa hata kama watagoma mwishowe watalazimika kurudi mezani kuzungumza, ndipo wapate wanayoyataka. Niliwatahadharisha pia kwamba ni bora kuzungumza sasa kuliko kufanya hivyo baada ya mgomo kwani hujui katika kipindi cha mgomo mambo yatakuwaje. Inawezekana hata mazingira ya kuzungumza yakawa mabaya.

Wazee Wangu;

Napenda kueleza furaha yangu na shukrani zangu kuwa maombi yangu yalikubaliwa na pande zetu tatu zimekuwa zinazungumza tangu wakati ule kwa mujibu wa sheria ya Mahusiano Kazini na Sheria ya Taasisi Kazi. Napenda kusema pia kuwa, mazungumzo yamekwenda vizuri, yapo mambo yaliyokamilika na yapo yanayoendelea kuzungumzwa na naamini nayo yatakamilika. Nadhani mnashangaa kuelezea furaha na kusema yapo mambo yaliyokamilika na kuonesha matumaini kuwa yaliyobakia nayo yatakamailika. Hii ni sahihi kabisa .

Naomba nifafanue kidogo. Tarehe 6 Aprili, 2010 kulifanyika kikao cha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambapo TUCTA iliwasilisha rasmi hoja zao zinazowafanya waitishe mgomo wa wafanyakazi wote nchi nzima kuanzia tarehe 5 Mei, 2010. Hoja hizo ziliwasilishwa na kuzungumzwa na kuamuliwa ipasavyo.

a. Madai kuwa Bodi za Kisekta zilikuwa zimemaliza muda wake yalifutwa na TUCTA baada ya kugundua kuwa walikosea tarehe.
b. Kuhusu madai ya kuchelewa kutangazwa kima cha chini nalo halikuwa tatizo la Serikali bali ni LESCO kupata mamlaka ya Bunge.
c. LESCO kutokukutana kwa sababu ya mazungumzo kuchelewa kumalizika ndani ya siku 60, hivyo kibali cha Bunge kilihitajika ambacho kilipatikana Februari, 2010. Kinachosubiriwa sasa ni tarehe ya mazungumzo kupangwa.
d. Ripoti ya Tume ya Ntukamazina kupewa TUCTA; wakaambiwa Tume aliunda Rais imshauri yeye kama wanahitaji ripoti wakamuombe yeye.
e. Kima cha chini kiwe shilingi 315,000/=; wakaambiwa lizungumzwe kwenye baraza husika.
f. Kodi kuwa kubwa mno; wapeleke kwenye Mamlala husika.
g. Ukokotoaji wa malipo ya uzeeni uhuishwe ili ufanane katika mifuko yote. Waliambiwa ili nalo likazungumzwe.

Tarehe 14 Aprili, 2010, LESCO ilikutana kujadili taarifa ya CMA na kuelekeza ipasavyo. Matokeo ya uamuzi wa LESCO ni:-
a. Kukubali mapendekezo ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi na kuelekeza Waziri wa Kazi atangaze kabla ya tarehe 30 Aprili, 2010; Waziri akafanya hivyo, lakini cha ajabu mara baada ya Waziri kutangaza, TUCTA wakamshutumu Waziri Kapuya na kudai hiyo ni danganya toto. Lakini wakati wanafanya hivyo, maamuzi hayo yamefanywa katika vikao ambavyo TUCTA wameshiriki kwa ukamilifu. Waziri si mjumbe wa vikao vyote hivyo, bali yeye ndiye mtanganzaji.
b. Ikaafiki uamuzi wa CMA kuwa suala la kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa umma lipelekwe kwenye Baraza la Majadiliano la Pamoja la Utumishi wa Umma kuzungumzwa.

Tarehe 27 Aprili, 2010, kikao cha Baraza hilo kikaitishwa na mazungumzo kuendelea tena tarehe 30 Aprili, 2010. Baada ya kikao cha tarehe 30 Aprili, 2010 walikubaliana wakutane tena tarehe 8 Mei, 2010. Jambo la kustaajabisha, tarehe 1 Mei, wale wale waliokubaliana wakutane tarehe 8 mwezi Mei, wanatoa siku mbili kwa wenzao kutoa majibu na isipofanyika hivyo tarehe 5 mwezi Mei wafanyakazi wote wagome.

Lingine la ajabu ni la viongozi wa TUCTA kuendelea kudai hadharani kima cha chini cha shilingi 315,000/= , wakati siku ya kwanza ya mazungumzo walielezwa ugumu wake, nao wakakubali na kupendekeza kiwango kingine cha chini, ambacho nacho Serikali iliona hakitekelezeki. Hivyo tarehe 30 Aprili, viongozi wa TUCTA wakapendekeza kiwango kipya cha chini zaidi. Upande wa Serikali nao walipendekeza kiwango wanachoamini kuwa mapato yetu yanaweza kumudu. Licha ya mwenendo mzuri wa mazungumzo, bado hakujawa na muafaka kati ya kiwango kipya cha chini walichopendekeza viongozi wa TUCTA na kiwango kilichopendekezwa na Serikali. Kutokana na hali hiyo walikubaliana wakutane tarehe 8 Mei, 2010 kuendelea na mazungumzo.

Ndugu Wananchi;

Iweje tena tarehe 1 Mei, 2010 mtu yule yule anageuka na kuzungumzia kima kile kila cha mwanzo wa mazungumzo na iamuliwe ndani ya siku mbili? Tunayo kila sababu ya kuhoji dhamira zao, wana nia njema kweli wenzetu hawa? Wana hili hili au wana lao jambo lingine?

Kima cha Shilingi 315,000/=

Kima cha chini cha shilingi 315,000/= hakitekelezeki kwa sababu Serikali haitakuwa nazo pesa hizo. Kwa kima hicho, Serikali itatakiwa kutumia shilingi bilioni 6,852.93 kwa mishahara peke yake wakati mapato yanayotarajiwa katika bajeti ijayo ni shilingi bilioni 5,773.1, ambazo zinapaswa kutumika kwa mishahara pamoja na shughuli zingine za kuendesha Serikali na maendeleo. Hivyo basi, italazimika kukopa shilingi bilioni 1,233.52 zaidi ili zitosheleze mahitaji ya mishahara peke yake. Hii haiwezekani kwa sababu Serikali itakuwa haifanyi shughuli nyingine ila kulipa mishahara. Tutakuwa ni watu wa ajabu sana. Huko tutakapokwenda kukopa watatushangaa na tutaonekana kichekezo. Na viongozi wa TUCTA tumewaambia hivyo.

Hata kama ningetaka kuwafurahisha akina mzee Mgaya, kwa jambo hili haiwezekani. Na, kama wanavyodai kwamba watampigia kura kiongozi na chama atakayewapa fedha hizo, kura hizo sisi tunahesabu tumeshazikosa. Ni afadhali kuzikosa kura za akina Mgaya kuliko kuwaumiza wananchi walio wengi kwa kutumia fedha zote za nchi kuwapa akina Mgaya wagawane na kuwakosesha wananchi huduma muhimu. Jambo hili sitalifanya.

Hatutafanya hivyo, kwa vile fedha za Serikali ni za Watanzania wote milioni 40 na siyo kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi 350,000 tu. Ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote kwa ajili ya maendeleo yao. Kuwalipa mishahara wanayodai viongozi wa TUCTA inamaanisha kwamba serikali isitishe kutoa huduma yoyote ile kwa wananchi; madawa hospitalini yasiwepo, ruzuku za mbegu, mbolea na madawa ya kuulia wadudu visiwepo, ujenzi wa majosho, barabara, zahanati, mashule, maji na umemenk usitishwe, shuguli za ulinzi na usalama wa raia pia zisimamishwe. Na wafanyakazi wenyewe wakifika maofisini mwao watakuwa ni watu wa kupiga gumzo tu bila kufanya kazi yoyote kwa sababu hakutakuwapo fedha za kununulia vitendea kazi. Hii haiwezekani. Hii ni sawa na kusema serikali iwe imekufa. Hakuna serikali inaweza kufanya hivyo. Hata hao ambao wanawapigia debe hivi sasa kama wangebahatika kuwa madarakani wasingeweza na hawataweza kamwe kukubali miujiza hii.

Wazee Wangu, Wananchi Wenzangu;

Naomba muelewe ugumu tulionao katika mazungumzo na viongozi wa TUCTA. Hawataki kuwaambia wafanyakazi na wanachama wao ukweli. Viongozi hawa hawana muamana, kwenye majadiliano wanakubaliana jambo moja, wakitoka nje wanasema jingine. Viongozi hawa wanakosa moja ya nguzo muhimu ya uongozi bora. Nguzo ya uongozi bora ni kuwaambia watu unaowaongoza ukweli hata kwa yale mambo wasiyopenda kuyasikia. Hawana sababu ya kuacha kuwaeleza wanachama wao ukweli. Tayari viongozi hao wamekubaliana na Serikali kukutana tarehe 8 Mei. Hawana sababu tena ya kuipa Serikali siku mbili kutekeleza mambo yale yale yaliyopangwa kujadiliwa baina yao na Serikali tarehe 8 Mei.

Uhalali wa Mgomo

Ndugu Wananchi;

Mgomo unaoshinikizhwa na viongozi wa TUCTA ni batili na kinyume cha sheria. Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Employment and Labour Relations Act,) No. 6 ya 2004 inaainisha pamoja na mambo mengine utaratibu wa kutatua mizozo na migogoro kazini na haki za mwajiri na mwajiriwa. Utaratibu wa mgomo ulioainishwa katika sheria hiyo, unazingatia maslahi ya wafanyakazi, waajiri pamoja na wananchi. Unatambua umuhimu wa kufanya majadiliano na unasisitiza kwamba huduma muhimu hazipaswi kuathirika kutokana na migomo. Aidha, imetamka kuwapo kiwango fulani cha huduma wakati wa mgomo. Uratatibu huo unaelekeza kwamba mgomo wenyewe utekelezwe kwa kiwango ambacho kitasaidia kutatua tatizo mahsusi lililopo kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mambo ya msingi ya kuzingatia ni kwamba kabla mfanyakazi hajagoma, au mwajiri hajaamua kufunga eneo la kazi (lock out) kuwe na majadiliano yatakayofanyika kwa nia njema kati ya mwajiri na mwajiriwa na kwamba majadiliano hayo yawe yameshindwa kutoa suluhisho. Kamishna wa Kazi awe amearifiwa hiyo. Wafanyakazi wasilazimishwe kugoma, badala yake wao wenyewe wawe wameamua kwa ridhaa yao kwa kura, kushiriki katika mgomo.

Bahati mbaya sana mgomo huu uliotangazwa na Chama cha Wafanyakazi siyo halali kabisa. Umeitishwa wakati ambao majadiliano bado yanaendelea. Hawaonyeshi kuwa na nia njema katika majadiliano kwani mambo yanayokubalika kwenye majadiliano ni tofauti na yale wanayowaambia wafanyakazi wao. Pili, wanawalazimisha wafanyakazi wote kushiriki katika mgomo, hata wale ambao sheria inasema kwamba huduma zao ni muhimu hivyo hawatakiwi kugoma. Tatu mgomo wenyewe hauna muda. Nne, viongozi wamejitwalia mamlaka ya kisheria kutangaza mgomo bila kuzihusisha mamlaka za kazi jambo ambalo kwa kweli siyo zuri wala la kistaarabu. Kutokana na kushindwa kutekeleza masharti haya ya Sheria ya Ajira na mahusiano kazini mgomo huu ni kuvunja Sheria za nchi, ni haramu. Hatuwezi kukubali jeuri ya watu wanaovunja sheria za nchi.

Ndugu Wananchi;

Nimalize kwa kutoa ushauri wangu kwa wafanyakazi wa Serikali, wafanyakazi wa sekta binafsi na viongozi wa TUCTA. Kwa wafanyakazi wa Serikali hakuna sababu ya msingi kugoma kwa madai yasiyotekelezeka ya kulipwa kima cha chini cha shilingi 315,000/=. Kwa vile mazungumzo baina ya Serikali na TUCTA bado yanaendelea, hakuna sababu za msingi za kugoma. Kwa vile ni dhahiri kuwa siyo halali. Atakayegoma atakuwa amekiuka taratibu na kanuni za ajira na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu na kanuni za utumishi Serikalini. Na yule ambaye atakwenda kazini lakini ataacha kufanya kazi atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Kwa wafanyakazi wa sekta binafsi, tumeunda Bodi za kisekta zimeshafanya kazi yake na Waziri wa Kazi ameshatangaza tuzo stahiki kisheria. Tangazo la TUCTA nyie mgome ili mlipwe shilingi 315,000/= linavunja sheria. Msiwasikilize. Mtapoteza ajira zenu na Mgaya hamtamwona. Ndugu zangu mshahara unategemea uwezo wa mwajiri kulipa, usidai kiasi ambacho hawezi kukulipa. Bodi ya Kisekta ndiyo muamuzi kwa mujibu wa sheria. Madai mengine yote nje ya utaratibu huu ni batili.
Changamoto kwa viongozi wa TUCTA, ni kuwa wakweli kwa watu wanaowaongoza na wawe tayari kusema hata yale mambo magumu ambayo wafuasi wao hawapendi kuyasikia.

Ahsanteni Sana kwa Kunisikiliza!
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

MANUMBA AGEUKIA MASUALA YA MAZINGIRA!!!

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini, Robert Manumba amesema kwamba udhibiti mkubwa wa kisheria unahitajika kutoka vyombo husika katika kupambana na vitendo vya uharibifu wa mazingira.

Kauli hiyo ilitolewa na Manumba jana wakati akizundua ripoti ya utafiti wa uharibifu wa mazingira Tanzania katika warsha ya siku moja uliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Tunahitaji udhibiti mkubwa wa sheria kutoka vyombo husika mfano polisi Takukuru katika kuhakikisha watu wanaovunja sheria za zinazodhibiti utunzaji wa mazingira kuhakikisha kuwa wanakamatwa na kuhukumiwa, ikiwemo upepelezi na uendeshaji mzuri wa kesi,” alisema Manumba.

Mkurungezi huyo amesema hayo baada ya utafiti huo kubaini kwamba vyombo vya kisheria vina upungufu wa uwezo wa kutambua, kuchunguza na kuendesha kesi zinazohusiana makosa ya mazingira.

Manumba ameongeza sekta zinazohusika kupambana na vitendo vya uharibifu wa mazingira, ambavyo ni vyombo vya kisheria,sekta binafsi na jamii zinapaswa kuweka kipaumbele utamaduni wa uratibu na ushirikiano ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.

Ameongeza kwamba binadamu wanapaswa kuyalinda mazingira kwa kuwa ndio yanayowafanya waishi.

Akizungumzia kuhusu warsha hiyo ambayo imeshirikisha wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha DarSalaam(USDM),taasisi zisizo za kiserikali , Ushirikiano wa Polisi Duniani Tawi la Nairobi, wizara za mazingira na idara za serikali alisema itasaidia kutoa mapendekezo na mikakati ya udhibiti wa suala hilo.

Naye Dk. Wilson Kipkore kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama,(ISS) alisema utafiti huo umefanyika katika nchi za Tanzania, Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan, Ehtiopia na Schely, ambapo kila nchi ina ripoti yake, umebaini kuwa ukuaji wa idadi ya watu ni changamoto kubwa katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni mabadiliko ya hali ya juu ya teknolojia mfano utumiaji wa machine zenye nguvu kubwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na vitendo mbalimbali vya binadamu kama vile uchomaji misitu.

Ameshauri serikali kutoa kuelekeza rasimali za kutosha,ikiwemo rasilimali watu ili kuweza kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Utafiti huo kwa sasa umefanyika kwa muda wa miaka miwili, lakini unatakiwa kukamilishwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

TANGAZO LA TIGO MATATANI!!!

Wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara wameitaka Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo kusitisha matumizi ya tangazo linalomuonesha mtu anayejisaidia vichakani wakati wa safari ya kwenda Songea wakidai tangazo hilo linaudharirisha Mkoa wa Ruvuma.

Wajumbe hao, wameilaumu kampuni ya tigo kwa kutengenza tangazo lisiloeleza hali halisi kwa kuwa eneo lililowekewa kibao cha Songea halipo Mkoani Ruvuma, wala basi lilitumika halitoi huduma Mkoani Ruvuma.

Pamoja na kuitaka kampuni ya Tigo kusitisha matumizi ya Tangazo hilo, wajumbe hao waliokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa Dr Christin Ishengoma wametishia kudai fidia kutoka kampuni ya Tigo endapo itaendelea kulitumia tangazo hilo katika vyombo vya habari vya Luninga.

Tangazo la Kampuni ya simu ya tigo linalolalamikiwa, linaonesha kilometa 250 kabla kufika SONGEA mtu mmoja anaingia vichakani kwa ajili ya kujisaidia, na kisha anaachwa na baada ya kulisimamisha basi hilo kwa kutumia simu.

Aidha wajumbe wa Bodi ya barabara Mkoani Ruvuma wameridhia mpango wa wakala wa barabara Mkoani humo, wa kujenga vituo viwili vya vyoo kati ya Njombe na Songea kwa ajili ya kujisaidia abiria wanaosafiri kutoka na kuingia Mkoani Ruvuma.

Monday, May 3, 2010

MAMBO YA ARDHI!!

Wataalamu wa udongo wa kituo cha Utafiti UYOLE wamebaini kuwa ardhi ya Mkoa wa RUVUMA inakabiliwa na tatizo la upungufu wa madini ya Salfa hali inayochangia kuzorota kwa ustawi wa mazao hususani mahindi.

Matokeo ya Uchunguzi wa ardhi ya Mkoa wa RUVUMA yanakuja ikiwa ni miaka kumi tangu Mkoa huo upige marufuku matumizi ya Mbolea aina ya SA ambayo ina kiasi kikubwa cha madini ya salfa.

Athari za ardhi ya Mkoa wa Ruvuma kupungukiwa madini ya Salfa zimeathiri zaidi uzalishaji wa Zao la Mahindi, ambapo sasa wakulima wanashindwa kufikia rekodi ya kuzalisha magunia 25 hadi 30 ya mahindi, hali iliyowalazimu wataalamu kutoka kituo cha Utafiti wa Udongo Uyole kuendesha utifiti shirikishi katika vijiji vitatu vya wilaya ya Mbinga Mkoani Humo.

Afisa kilimo wa Mkoa wa RUVUMA amekiri kuwepo malalamiko ya wakulima juu ya kupigwa marufuku matumizi ya Mbolea ya SA, lakini akajitetea kuwa Mkoa ulishaagiza wilaya zipime ardhi upya na kutoa ushauri, agizo ambalo utekelezaji wake unasuasua

Pamoja ardhi ya Ruvuma kupungukiwa madini ya Salfa, Utifiti wa Uyole pia umebaini kuwa kuna upungufu wa Madini ya Nitrogen, Phosphoras, na Calcium (Habari kwa Hisani ya Gerson Msigwa)

WAAFRIKA AMBAO WANATAMBA INTER MILAN!!




Hawa ni wachezaji ambao wanambeba Jose Antonio Mourinho katika Klabu ya Inter Milan ambayo inausaka Ubingwa wa Italy pamoja na Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya. Wachezaji hawa ni Mshambuliaji wa Kimataifa wa Cameroon Samuel Etoo Fils,Kiungo wa Kimataifa wa Ghana (Black Stars) Sulley Ally Muntari na Kiungo wa Kenya McDonald Mariga.

Sunday, May 2, 2010

UBINGWA ENGLAND BADOOO!!!



Chelsea wakati ikiifunga kwa urahisi Liverpool kwa magoli 2-0, Manchester United nayo yashinda kwa 1-0 mbele ya Sunderland. Haya yetu macho na masikio tu!!!

Saturday, May 1, 2010

SOUTH KOREA WATAJA KIKOSI CHA WORLD CUP!!!

Kim Young-Kwang (Ulsan), Lee Woon-Jae (Suwon), Jung Sung-Ryong (Seongnam); Kang Min-Soo (Suwon), Kwak Tae-Hwi (Kyoto), Kim Dong-Jin (Ulsan), Kim Hyung-Il (Pohang), Oh Beom-Seok (Ulsan), Lee Young-Pyo (Al Hilal), Lee Jung-Soo (Kashima Antlers), Hwang Jae-Won (Pohang), Cho Won-Hee (Suwon Bluewings - on loan from Wigan), Cha Du-Ri (SC Freiburg), Cho Yong-Hyung (Jeju); Koo Ja-Cheol (Jeju), Ki Sung-Yong (Celtic), Kim Bo-Kyung (Oita), Kim Nam-Il (Tom Tomsk), Shin Hung-Min (Pohang), Kim Jae-Sung (Pohang), Kim Jung-Woo (Gwangju), Lee Chung-Yong (Bolton), Kim Chi-Woo (Seoul), Park Ji-Sung (Manchester United); Park Ju-Young (AS Monaco), Ahn Jung-Hwan (Dalian Shide), Lee Seung-Ryul (Seoul), Yeom Ki-Hun (Suwon), Lee Keun-Ho (Jubilo Iwata), Lee Dong-Guk (Jeonbuk)

KIKOSI CHA BAFANA BAFANA WORLD CUP!!!

Goal Keepers: Itumeleng Khune (Kaizer Chiefs), Shu-Aib Walters (Maritzburg United), Rowen Fernandez (Arminia Bielefeld, Germany), Moeneeb Joseph (Orlando Pirates).

Defenders: Matthew Booth (Mamelodi Sundowns), Siboniso Gaxa (Mamelodi Sundowns), Innocent Mdledle (Mamelodi Sundowns), Bongani Khumalo (Supersport United), Tsepo Masilela (Maccabi Haifa, Israel), Aaron Mokoena (Portsmouth, England), Bryce Moon (PAOK, Greece), Anele Ngcongca (Racing Genk, Belgium), Siyabonga Sangweni (Golden Arrows Lucas Thwala (Orlando Pirates).

Midfielders: Surprise Moriri (Mamelodi Sundowns), Franklin Cale (Mamelodi Sundowns), Lance Davids (Ajax Cape Town), Kagisho Dikgacoi (Fulham, England), Andile Jali (Orlando Pirates), Teko Modise (Orlando Pirates), Reneilwe Letsholonyane (Kaizer Chiefs), Siphiwe Tshabalala (Kaizer Chiefs), Thanduyise Khuboni (Golden Arrows), (Steven Pienaar (Everton, England), Macbeth Sibaya (Rubin Kazan, Russia).

Strikers: Benni McCarthy (West Ham United, England), Katlego Mphela (Mamelodi Sundowns), Siyabonga Nomvete (Moroka Swallows), Bernard Parker (FC Twente, Holland).

WAKULIMA TUNDURU WALILIA SOKO!!

WAKULIMA wa Halmashauri ya wilaya ya TUNDURU, Mkoa wa RUVUMA, wameiomba serikali wilayani humo kuhakikisha inawafungulia maghulio kwa ajili ya kuuzia mazao yao ili kuepukana na wafanyabiashara matapeli ambao huwanyonya.

Wamesema kumeibuka wimbi kubwa la wafanyabiashara matapeli ambao huzunguka vijijini kuwarubuni wakulima na kisha kuununua mazao yao kwa bei ya chini tofauti na jasho wanalotumia katika kilimo chao.

Wakulima hao wamelazimika kutoa kilio chao hicho kwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA , Bi CHRISTINE ISHENGOMA, wakati akiwakabidhi wakulima hao trekta ndogo za kulimia 62 zenye thamani ya zaidi ya milioni 360.

Bi ISHENGOMA amekabidhi trekta hizo kwa wakulima hao tayari kwa shughuli za kilimo ikiwa ni mkakati wa halmashauri hiyo kuondokana na kilimo cha jembe la mkono kutoka asilimia 0.8 sasa hadi kufikia ailimia 15 ifikapo Juni 2011 ili kuongeza tija ya uzalishaji mazao na kukuza kipato chao.

Pamoja na kuwatoa hofu wakulima hao kuondoa mashaka kuhusu uhakika wa kuuza mazao yao , Bi ISHENGOMA amewataka wakulima wilayani humo kuhakikisha wanazitumia trekta hizo katika shughuli za kilimo pekee na siyo kubebea abiria.

Amesema trekta hizo zitasaidia katika kuongeza tija ya uzalishaji mazao na kwamba mkoa huo katika kipindi cha mwaka 2009/2010 imevuna mazao ya chakula na biashara tani 983,883 sawa na asilimia 93.6 ya matarajio ya kuzalisha mazao tani 1,506,520.

Awali kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya TUNDURU, Bi MARY DING’HOI amesema gharama ya trekta moja dukani ni milioni 6.5 lakini halmashauri inamchangia mkulima asilimia 80 na hivyo mkulima anapaswa kuchangia asilimia 20 iluyobakia ambayo ni sawa na sh. milioni 1.3.

Amebainisha kuwa msimu huu wameagiza trekta 64 na kwamba zingine 75 zimeshapata mzabuni wa kuzifikisha hadi Tunduru tayari kwa kugawiwa kwa wakulima. ( Habari kwa Hisani ya Emmanuel Msigwa)

Friday, April 23, 2010

LIVERPOOL YALALA WAKATI FULHAM IKILAZIMISHA SARE UEFA!!




Michezo miwili ya nusu fainali ya Mchuano wa Ligi ya Europa imepigwa na kushuhudia Atletico Madrid wakiwalaza Vijogoo vya Jiji Klabu ya Liverpool wakati Fulham wakipata sare tasa ya ugenini dhidi ya Hamburg!!!

Tuesday, April 20, 2010

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO SONGEA!!!











Nyumba moja yateketea kwa Moto Songea eneo la Mfaranyaki huku chanzo chake kikiwa bado hakijathibitishwa ( Picha kwa Hisani ya Emmanuel Msigwa)

SERIKALI YA AWAMU YA NNE NA ELIMU!!!

Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kuwezesha asilimia 96 ya watoto wenye umri wa kwenda shule kuwa darasani kutoka asilimia 35 miaka sita iliyopita.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo jioni (19.4.10) Jijini New York katika sherehe ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya kuzindua rasmi Mfuko wa Elimu Tanzania, Tanzania Education Fund.

“Mafanikio yetu ya kwanza yametokana na kuweza kuandikisha watoto kujiunga na elimu ya msingi na kuhakikisha kila mtoto anayetakiwa kuwa shule anakuwa darasani, miaka 6 iliyopita asilimia 35 ya watoto Tanzania ambao walitakiwa kuwa darasani walikuwa mitaani au wapo katika ajira”. Amewaambia waalikwa waliohudhuria chakula hicho cha jioni “sasa hivi ninapoongea nanyi, tumefanikiwa kuandikisha watoto shuleni kwa asilimia 96 na tumedhamiria kuwapeleka wote shuleni” Rais amesema.

Mfuko wa Elimu Tanzania, ni Shirika lisilo la Kiserikali(NGO) lililoanzishwa na marafiki wa Tanzania wa Kimarekani kwa kushirikiana na Serikali yaTanzania.

Kwa miaka minne sasa Serikali ya Awamu ya Nne imeweka kithara na kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha sekta ya elimu hapa nchini inaboreshwa na kuimarishwa. Kwa kuzingatia kithara hizo, bajeti ya sekta ya elimu imekuwa ikiongoza kwa ukubwa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa malengo ya msingi ya Awamu ya Nne yanafanikiwa.

Malengo haya ya msingi ni “Kuhakikisha watoto wa kike na wa kiume nchini Tanzania anapata elimu bora kuanzia elimu ya msingi, sekondari na hadi elimu ya juu” Rais amewaeleza marafiki wa Tanzania waliohudhuria chakula hicho.

Rais ameelezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa ambapo mwaka 2000, Tanzania ilikuwa na shule za sekondari 927 na hadi kufikia mwaka 2009 shule hizo zimeongezeka kwa asilimia mia nne na kufikia idadi ya shule 4,102. Hivyo hivyo kiwango cha uandikishaji wanafunzi katika shule hizi za sekondari kimeongezeka kutoka 261,896 hadi kufikia milioni 1.46 katika kipindi hicho hicho.

Mafanikio mengine ni kwamba kati ya mwaka 2006 na 2009, jumla ya shule za sekondari 2,377 zimejengwa na hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 524,325 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi milioni 1.6.

Hata hivyo Rais Kikwete amesema mafanikio yote haya yameleta changamoto mpya ambazo ni uhaba wa walimu, uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia, uhaba wa vyumba vya maabara na nyumba za walimu.

Rais amewaambia waalikwa kuwa gharama za kutatua changamoto zote hizi zinazidi Dola za Kimarekani Bilioni 1.2 kwa miaka mitano, gharama ambazo kwa nchi maskini kama Tanzania ni mtihani ambao unahitaji ubunifu katika kuzitatua.

“Inahitajika ubunifu na ushirikiano katika kutatua changamoto hizi kutoka kwa marafiki na ndiyo maana tumekusanyika leo hapa”. Rais amewaambia waalikwa akiwemo mfanyibiashara Douglas Pitt ambaye amekuwa akisaidia Tanzania kimya kimya kwa zaidi ya miaka sita.

Katika sherehe hizo kabla ya chakula cha kuzindua mfuko wa Elimu Tanzania, Rais alimtangaza rasmi Bw. Douglas Pitt kuwa Balozi wa hiari wa Tanzania ambaye atakua na kazi ya kuitangaza Tanzania katika highly zake za kibiashara, utalii na elimu.

Bw. Douglas Pitt ni mdogo wake mcheza sinema maarufu wa Marekani Bw. Brad Pitt.

Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani na anaondoka Jijini New York leo tarehe 20April, 2010 kurejea Dar-es-salaam.

VYETI VYA FORM FOUR KUWEKWA PICHA!!!

Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania imeanza kuweka picha katika vyeti vya matokeo ya kidato cha nne na sita ili kudhibiti kutumiwa na watu wasio watainiwa kwa ajili ya kutafuta ajira au nafasi za masomo ya juu.

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza amesema hatua hiyo ya kuweka picha katika vyeti itawawezesha wadau kumtambua mmiliki halali wa cheti.

Aidha Mheshimiwa Maiza alisema zoezi la kuweka vyeti hivyo picha huwekwa kwa kompyuta hivyo picha hizo haziwezi kuondolewa.

Pia amesema zoezi la kuweka picha katika vyeti litaanza na vyeti vya watahini waliofanya Mtihani wa kidato cha nne mwaka 2008 ambavyo vitachapwa mwezi Mei 2010

Naibu Waziri amesema hati ya matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2009 zimetolewa zikiwa na picha

Akijibu swali la nyongeza Waziri Maiza amesema serikali haian taarifa ya kubadilishana vyeti kwa wahusika kwani jambo hilo huwa hufanyika kwa makubaliano maalumu kati ya mwenye cheti na nayetaka kupew cheti hicho.

Hata hivyo Naibu Waziri Mahiza aliongezea kuwa Serikali imewakamata na inaendelea kuwakamata wale wote waliofoji vyeti na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi za kisheria

Ametoa wito rai kwa wananchi wote kuacha mtindo wa kutumia vyeti visivyokuwa vyao kwani kwa kufanya hivyo kunawanyima haki wenye vyeti stahili zao na ni kutenda kosa la jinai.

Monday, April 19, 2010

CUF WALIA NA SHERIA YA WALEMAVU!!!

CUF – Chama cha Wananchi pamoja na kulipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha muswada wa Sheria ya Watu Wenye Ulemavu, tunamsihi Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuharakisha kusaini muswada huo ili iwe sheria, lakini pia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu kuhakikisha kanuni zinaandaliwa mapema kwa ajili ya utekelezaji.

Muswada huo uliopitishwa Bungeni wiki iliyopita, umeridhiwa na Wabunge wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, na moja ya yaliyoridhiwa ni kuwepo kwa baraza la ushari litakalowashirikisha Watu wenye ulemavu na wadau wengine zikiwemo wizara za Serikali.

CUF – Chama cha Wananchi tunakila sababu ya kushinikiza kusainiwa muswada huo pia kuandaliwa kanuni zake haraka iwezekanavyo kama ilivyofanyika kwa muswada wa sheria ya gharama za uchaguzi, ili kuepusha yaliyotokea katika Sera ya Taifa ya Huduma ya Maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu ambayo ilitolewa April 2004 na kuzinduliwa 2007 kwa kudandia maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu duniani ambayo yameandaliwa na watu wenye ulemavu wenyewe.

Hiyo kama haitoshi hadi unaandaliwa muswada wa sheria ya haki za watu wenye ulemavu sera hiyo bado haijaandaliwa mkakati wa utekelezaji, jambo linalotia mashaka, hivyo ni budi maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya kapewa thamani na uzito unaostahili kwa kutambua kwamba masuala ya watu wenye ulemavu yana gusa kila binadamu alie hai kwani inatambulika kuwa “Hujafa Hujaumbika”.

CUF – Halikadhalika tunamtanabaisha Rais Jakaya Kikwete kuwa masuala ya Watu wenye Ulemavu ni mtambuka, na yanahusisha karibuni wizara zote za Serikali, hivyo basi hana budi kulitambua hili na kuhamisha masuala ya Watu wenye ulemavu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili iwe rahisi kusimiwa na kufuatilia utekelezaji wake.

CUF – Tunawahimiza watu wenye ulemavu kuzitumia vyema haki zao na fursa zilizomo katika vyama vya siasa hususan chama mbadala Chama cha Wananchi – CUF, kwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea, na chama kinaahidi kuwa hakuna ubaguzi wowote, tutaheshimu uwezo wa mtu bila ya kujali maumbile yake.

SIMBA YAKABIDHIWA KOMBE!!!


Wachezaji wa Simba wakinyanyua Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo wamekabidhiwa baada ya kuichakaza Yanga kwa magoli 4-3. Hongera Simba kwa Ubingwa!!!

Sunday, April 18, 2010

RAIS KIKWETE ALIVALIA NJUGA SUALA LA AFYA!!!

Changamoto Kubwa inayozikumba nchi zinazoendelea katika utoaji wa huduma za afya ni tatizo kuwa watu wa nchi hizi wanakabiliwa na maradhi mengi na wanaugua mara kwa mara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo wakati alipokuwa anatoa mhadhara juu ya “Changamoto za Utoaji wa Huduma za Afya katika Nchi Zinazoendelea“ katika Chuo Kikuu cha Afya cha Weill Cornel Jijini New York.

“Afrika ina asilimia 11 tu ya idadi ya watu duniani lakini ina asilimia 24 ya mzigo wa maradhi duniani”, Rais amesema na kunukuu takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) ambazo zinaonesha kuwa kati ya vifo 10 vinavyotokea katika nchi tajiri, ni mtu mmoja tu ndiye anayekufa kutokana na magonjwa ya kuambukiza, wakati katika nchi maskini vifo sita kati ya kumi vinatokana na na maradhi ya kuambukiza.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa nchi maskini bado zinakabiliwa na maradhi ambayo yalishatokomezwa katika nchi zilizoendelea na kutoa mfano wa magonjwa kama malaria, kipindupindu, maradhi ya kuhara, typhoid na mengine mengi.

Rais Kikwete amewaeleza wanafunzi, wahadhiri na wageni waalikwa katika mhadhara huo kuwa, changamoto ingine inayozikabili nchi maskini ni uhaba wa wataalamu na huduma za afya ambazo ni pamoja na madawa na vitendea kazi, suala ambalo husababisha uchunguzi na matibabu kuwa magumu.

“Hata hivyo haya yote yanasababishwa na umaskini ambao umesababisha magonjwa makubwa kuwa mzigo na uwezo mdogo wa kukabiliana na maradhi” Rais amefafanua, pato la taifa la nchi zote Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mwaka 2008 lilikuwa dola za Kimarekani Bilioni 987.1, ambayo ni karibu na pato la taifa la nchi ya Korean ya Kusini ambalo lilikua Bilioni 992.0 na chini zaidi kuliko pato la Jiji la New York ambalo lilikua dola Trillion 1.4.

Hata hivyo pamoja na changamoto zote hizo Rais amesema, wananchi wa nchi zinazoendelea hawajakata tamaa na wanajitahidi kwa uwezo wao kuzikabili changamoto hizo na kujitahidi kuishi vyema, kwa kutengeneza sera, mipango na mazingira mazuri kulingana na hali halisi ya nchi zao.

Ameongeza kuwa kati ya jitihada hizo ni nchi hizi kutenga bajeti kubwa kwa ajili ya sekta ya Afya ingawa hata hivyo siyo kubwa sana ya kuweza kutatua matatizo ya sekta nzima ya afya kwa vile nchi hizi hazina uwezo mkubwa.

Ametoa mfano wa Tanzania ambayo ina mpango wa Afya wa miaka kumi ambao unalenga katika kuongeza na kuboresha huduma za afya ambapo serikali imeadhimia kujenga vituo vya Afya Tanzania nchi nzima katika umbali usiozidi km 5 kutoka makazi ya wananchi, kuongeza juhudi za kupambana na maradhi kama malaria, ukimwi, TB na maradhi ya kuambukiza.

Serikali pia inajidhatiti katika kujenga uwezo wa kubaini, kupima na kutibu magonjwa makubwa nchini ili wagonjwa watibiwe nchini, kuongeza idadi na uwezo wa wataalamu.

MCHUANO WA LANGALANGA WASHIKA KASI!!!!


Mchuano wa magari yaendayo kasi duniani maarufu kwa jina la Langalanga umemalizika nchini China na kushuhudia Jenson Button akiikwaa nafasi ya kwanza, huku nafari ya pili ikienda kwa Lewis Hamilton na nafasi ya tatu ikiangukia kwake Nico Rosberg. Mpangilio kwa nafasi kumi za juu ni kama ifuatavyo:
Driver Time
1 J Button 1:46:42.163
2 L Hamilton 1:46:43.693
3 N Rosberg 1:46:51.647
4 F Alonso 1:46:54.032
5 R Kubica 1:47:04.376
6 S Vettel 1:47:15.473
7 V Petrov 1:47:29.763
8 M Webber 1:47:34.335
9 F Massa 1:47:39.959
10 M Schumacher 1:47:43.912

DAKIKA CHACHE ZIMESALIA KABLA YA SIMBA NA YANGA KUUMANA!!!


Uwanja Mkuu wa Taifa ambapo dakika chache zijazo kutapigwa mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ukiwa mchezo wa mwisho katika Msimu huu ambapo tayari Wekundu wa Msimbazi wameshatwaa ubingwa!!!

LIGI KUU NCHINI ENGLAND YAFIKA PATAMU!!!



Michezo mitatu ikiwa imesalia kwa Chelsea na Manchester United kabla ya kumaliza Ligi Kuu Nchini England hatua tamu zaidi imefikia. Baada ya Man Utd kuifunga Man City wenzao Chelsea wamepoteza mchezo wao dhidi ya Tottenham Hotspurs na hivyo kufanya kibarua kuwa kigumu cha nani ataibuka Bingwa msimu huu.

BONGO YAWEZEKANA IKATOKEA KWELI??


Furaha ya Ushindi ambapo Beki wa Manchester United Gary Neville anaonekana akimbusu Paul Scholes ambaye alifunga goli la pekee kwenye mchezo dhidi ya Manchester City na kuweka hai matumaini ya kutwaa Ubingwa!!!

Monday, April 12, 2010

VAN PERSIE AREJEA!!!


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uholanzi ambaye anakipiga katika Klabu ya Arsenal Robin Van Persie anatarajiwa kurejea ugani katika mpambano wa London Derby katika ya Arsenal na Tottenham Hotspurs baada ya kupona matatizo ya mguu ambayo yalikuwa yanamkabili!!

CUF WAANZA MAMBO YAO!!!

CUF – Chama Cha Wanachi kimeshtushwa na kauli ya Mbunge wa Songea Mjini, ambaye ni Naibu wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi ya kuchangia sekta ya elimu kwenye jimbo lake la Songea Mjini zaidi ya shilingi milioni 300. Hayo aliyasema wakati wa kukabidhi majengo ya Sekondari ya kidato cha tano na sita yalioyopo Mkuza katika Manispaa ya Songea aliyojenga kwa juhudi zake binafsi.

Kwa kuzingatia kiwango cha mishahara ya mawaziri hapa Tanzania kauli ya Nchimbi imeleta utata juu ya uhalali wa mchango wake huo wa Tshs milioni 300 kwa kipindi chote ambacho amekuwa Waziri katika Serikali hii ya awamu ya nne.

CUF- Chama Cha Wananchi kinatambua tabia ya viongozi wa CCM kila inapofikia kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wao huanza kufanya kampeni kabla ya wakati na kutumia fedha ambazo hazilingani na vipato vyao halali kwa vipindi vyao vyote vya uongozi.

CUF – Chama Cha Wananchi kinamtaka msajili wa vyma ambae ndie msimamizi mkuu wa sheria za uchaguzi kwa kushirikiana na TAKUKURU kwa mujibu wa kauli yao kwa vyombo vya habari wamfuatilie Dr. Nchimbi kwani licha ya kutoa rushwa lakini pia ni ufisadi mkubwa.

KUMRADHI WADAU!!!

Niwaombe radhi wadau wote wa Blogu hii kuna kigugumizi sugu kilitokea na hivyo kusababisha mambo kushindwa kwenda kama kawaida! Lakini sasa mambo yametengamaa na kila siku nitaendelea kushusha mizigo mizito kazi kwenu!!

Sunday, March 21, 2010

MBINGA WAPATA NEEMA!!!

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF katika Mkoa wa RUVUMA umekiri kukumbana na ugumu katika uongezaji wa idadi ya waajiri na wanachama wa hiari unaosababisha kupunguza makusanyo ya fedha.

Meneja wa NSSF Mkoani humo WAZIRI NDONDE amesema kumekuwa na mwitikio mdogo hasa kwa wananchi wa hiari licha ya juhudi kubwa zinazofanywa kutangaza manufaa ya wananchi kujiunga katika Mifumo ya Hifadhi za Jamii.

Akizungumza katika Hafla ya kihitimisha Juma la NSSF iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa NSSF na Baadhi ya wateja wa Shirika hilo, Bw NDONDE amesema pamoja na kuwepo Changamoto hiyo, katika kipindi cha nusu mwaka zaidi ya shilingi milioni 560 kati ya lengo la shilingi bilioni 1 na milioni 200 zinazotarajiwa kukusanywa Mkoani RUVUMA.

Kuhusu malalamiko ya wanachama wa NSSF kuwa Mfuko huo umekuwa ukitoa mafao kidogo ikilinganishwa na mifuko mingine ya Hifadhi ya Jamii Meneja huyo amesema Serikali inaunda Chombo kitakachodhibiti viwango vya mafao ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Aidha amewaondoa shaka wanachama wa NSSF, kuwa Taarifa za shirika la wafanyakazi la kimataifa ILO zinaonesha kuwa viwango vianvyolipwa na NSSF vitaliwezesha shirika hilo kutoa mafao kwa miaka 50 baadaye ikilinganishwa na mashirika mengine ambayo yanakabiliwa na madeni makubwa (Habari kwa Hisani ya Gerson Msigwa)

Thursday, March 18, 2010

DODOMA WATAKA RAIS KIKWETE ASIPINGWE!!

Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, kimetoa tamko la kutaka Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, awe mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Aidha, katika kumwunga mkono, Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, kimemchangia Mheshimiwa Kikwete shilingi milioni moja, ili kumwezesha kununulia fomu ya kuomba nafasi hiyo.

Tamko hilo lilifikiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Dodoma kilichofanyika mjini Dodoma Februari 18, mwaka huu, 2010, na limekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Kikwete, leo mjini Dar es Salaam na ujumbe wa chama hicho.

Ujumbe wa chama hicho Mkoani Dodoma, umeongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa William Kusila, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Adam Kimbisa na Katibu wa chama hicho mkoani humo, Kapteni (mstaafu) John Barongo.

Tamko hilo linasema kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anastahili kuwa mgombea pekee wa Urais kupitia CCM kwa kuzingatia kazi nzuri na utakelezaji wa Ilani ya Uchaguzi chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanywa katika kipindi cha miaka 2005-2010.

Linaongeza tamko hilo: “Rais Kikwete ameonyesha uwezo mkubwa katika kuwaongoza Watanzania, na kuonyesha umakini mkubwa katika utoaji wa maamuzi mbalimbali bila jazba wala woga, chuki au upendeleo kwa Watanzania.”

Akipokea tamko hilo na pesa hiyo, Mheshimiwa Kikwete ameishukuru Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa kumwunga mkono akiahidi kuendelea kukitumikia chama chake na watanzania wote kwa kadri ya uwezo wake.

TUCTA WAZIDI KUBANWA!!!!

TAMKO LA SERIKALI JUU YA MGOMO WA TUCTA

Haki iliyotajwa hapo juu imeelezwa bayana katika sura ya saba ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004. Kanuni ya utendaji bora na taratibu za kufuatwa katika kutekeleza haki hiyo, imeelekezwa katika sehemu ya nne ya kanuni za utendaji bora toleo la Serikali namba 42 la tarehe 16/02/2007.

Katika sheria iliyotajwa hapo juu kila mfanyakazi anahaki ya kushiriki katika mgomo iwapo kuna mgogoro wa kimaslahi, na kila mwajiri ana haki ya kufungia nje wafanyakazi mahala pa kazi iwapo pana mgogoro wa kimaslahi.

Hata hivyo haki hii imejengewa utaratibu wa kuitekeleza ili kulinda uhai na usalama wa mali, ikiwa ni pamoja na haki za watu wengine ambao pia wana maslahi katika mahusiano hayo. Moja ya mambo yaliyozuiliwa ni kuitisha mgomo unaotokana na malalamiko au haki/ kutotendewa haki.

Kwa kifupi ninachosema ni kwamba mfanyakazi anayohaki ya kugoma kama vile mwajiri alivyo na haki ya kufungia nje mfanyakazi, lakini kwa makundi haya yote mawili ni lazima yazingatie kuwa ipo sheria na zipo kanuni zinazosimamia masuala haya.

Ni muhimu vilevile kufahamu kuwa katika suala la majadiliano baina ya Mwajiri na mfanyakazi wote wanakuwa na haki sawa, hakuna anayeweza kumwamrisha mwenzake, kwa hiyo ni mahala ambapo kila mmoja wao anapaswa kuacha jazba na kuwa na subira. Silaha kubwa ya pande zote mbili ni majadiliano.

KUHUSU TAMKO LA TUCTA LA KUTANGAZA MGOMO TAREHE 5/5/2010
Sisi kama Serikali ni dhahiri tamko hili au kauli hii imetushangaza na pia kiasi Fulani kutusikitisha kwani tunaamini kuwa hali ya mazungumzo ilivyokuwa inaendelea hakukuwa na haja ya kufikia hapo. Kila hoja waliyoieleza Serikali inaifanyia kazi kwa kushirikiana na wao, na wanalijua hilo.

Lakini pamoja na hayo, walipomwandikia barua Kamishna wa Kazi, yenye Ref. TUCTA/AP.15/3/9/2 ya 8/9/2010 kumwarifu juu ya nia yao ya kugoma, sie tulichukua hatua ya kuwajibu na kuwaita Wizarani, ili waje tuzungumze/tujadiliane barua Ref. CAB.360/223/01 ya 11/3/2010 cha kushangaza walikataa na kusema kuwa hawawezi kushiriki katika mazungumzo yoyote kwa sababu wao ni Kamati tu ya Utendaji wakati ambapo azimio la kugoma lilitolewa na Baraza Kuu la TUCTA Ref. TUCTA/P.15/17/5/37 ya 15/3/2010. Kwa bahati nzuri, wakati wanaliandikia barua hiyo ya kukataa kuja tarehe hiyo hiyo waliandika barua LESCO ya kutangaza nia yao ya kugoma ifikapo tarehe 5/5/2010 Ref. TUCTA/M.10/1/2/100 ya 15/3/2010 sababu walizotoa ni kama zifuatazo:-

1. Kutotekeleza mapendekezo ya Tume ya Mishahara ya NTUKAMAZINA ambayo iliteuliwa na Mheshimiwa Rais kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

2. Kutoliangalia swala zima la ukusanyaji wa kodi, hivyo kuwafanya wafanyakazi kuwa eneo kubwa pekee la kulipa kodi za juu wakati wafanyakabiashara wakilipa kodi ndogo na wakati mwingine kukwepa.

3. Wizara ya Kazi kutotangaza maamuzi yake kuhusu mapendekezo ya utafiti uhusuo Vima vya Chini katika sekta binafsi, kinyume na Sheria inavyoagiza.

4. Wizara ya Kazi kushindwa kuunda Bodi mpya za mishahara za Sekta Binafsi tangu zile za zamani zilipomaliza muda wake 1 Aprili 2009.

5. Wizara ya Kazi kushindwa kuitisha vikao vya LESCO ambacho ni chombo cha kuishauri Serikali kuhusu masuala ya wafanyakazi tangu chombo hicho kizinduliwe mwezi Agost 2009 licha ya Rais kuagiza likutane katika kikao chetu cha 4/5/2009 Ikulu Dar es Salaam.

6. Ofisi ya Waziri anayehusika na Menejiment ya Utumishi wa Umma kushindwa kuitisha vikao vya majadiliano yanayohusu maslahi ya Watumishi wa Umma kama sheria ya majadiliano (The Public Service Negotiating Machinery) Act 2003 inavyoagiza.

7. Serikali kutokuwa makini katika kurekebisha malipo dhaifu yatokanayo na Mifuko ya Pensheni ya Wastaafu hivyo kuwafanya Wastaafu wengi kupata mafao duni ya uzeeni.

Kwa kuwa sasa wamefuata mkondo wa sheria unaotakikana kwa kuiandikia LESCO, naamini sasa sheria itachukua mkondo wake katika kutukutanisha pande zote mbili. Sheria inaitaka LESCO kufanya hivyo ndani ya siku 30.

Nina imani hili litafanyika na nina imani pia kuwa ufumbuzi utapatikana kabla ya hiyo tarehe 5/5/2010.

Imesainiwa
Alhaj. Prof. Juma . A. Japuya (Mb)
WAZIRI WA KAZI, AJIRA NA MAENDELEO YA VIJANA

Wednesday, March 17, 2010

CHELSEA YAFA STAMFORD BRIDGE!!


Goli la Mshambuliaji wa Kimataifa wa Cameroon Samuel Etoo Fils limetosha kuwaondosha kwenye Mchuano wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Klabu ya Chelsea. Inter Milan ambayo inanolewa na Jose Antonio Mourinho imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa jumla ya magoli 3-1.

Tuesday, March 16, 2010

LIVERPOOL YAIUA PORTSMOUTH 4-1!!!



Vijogoo vya Jiji Klabu ya Liverpool vimefanikiwa kuweka kibindoni pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Portsmouth maarufu kama Pompey kwa magoli 4-1. Fernando Torres El Nino amesaidia timu yake baada ya kupiga bao mbili!!!

MACHINJONI HAPO (OLD TRAFFORD)!!


Maskani ya Manchester United hayo ambayo yanatambulika kwa jina la Old Trafford Uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu sabini na tisa. Timu zetu za hapa nchini nazo zinachangamoto ya kuhakikisha zinakuwa na viwanja kama hivi kwa ajili ya kuongeza mapato yao!!!

Monday, March 15, 2010

MAN UNITED YARUDI KILELENI, MAN CITY YABANWA TENA!!!



Mashetani Wekundu Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuichakaza Fulham kwa magoli matatu kwa nunge. Magoli ya Man United yamefungwa na Wayne Rooney ambaye amecheka na nyavu mara mbili huku goli la tatu likifungwa na Dimitry Berbatov. Manchester City wenyewe wameambulia sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Sunderland.

BECKHAM HATARINI KUKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA!!!





Kiungo wa kimataifa wa England David Beckham ambaye anakipiga katika Klabu ya AC Milan huenda akakosa mashindano yake ya nne ya Kombe la Dunia kufuatia kuumia katika mchezo dhidi ya Chievo. Beckham alilazimika kutolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia katika mchezo huo ambao AC Milan imevuna uhsindi wa goli moja kwa nunge. Kiungo huyo anatarajiwa kupelekwa Finland kufanyiwa upasuaji kwa madaktari bingwa.

Sunday, March 14, 2010

LANGA LANGA YAANZA KWA KASI!!!


Driver Race Time
1 Spain F Alonso 1:39:20.396
2 Brazil F Massa 1:39:36.495
3 Great Britain L Hamilton 1:39:43.578
4 Germany S Vettel 1:39:59.195
5 Germany N Rosberg 1:40:00.609
6 Germany M Schumacher 1:40:04.559
7 Great Britain J Button 1:40:05.676
8 Australia M Webber 1:40:06.756
9 Italy V Liuzzi 1:40:13.404
10 Brazil R Barrichello 1:40:22.885
Mashindano ya kwanza ya Msimu wa Formula One maarufu kama Langa Langa umeanza na kushuhudia Fernando Alonso akiibuka kidedea katika Behrain Grand Prix. Huku mkongwe Michael Schumacher ambaye ni bingwa mara saba liyerejea tena katika mchuano akiangukia nafasi ya sita.

PACQUIAO AMCHAKAZA CLOTTEY!!!


Bingwa wa WBO Manny Pacquiao amefanikiwa kutetea taji lake baada ya kumchakaza Bondia wa Ghana Joshua Clottey kwa pointi baada ya raundi kumi na mbili kumalizika bila ya kuwepo mbabe!!