Monday, May 24, 2010

CUF WALISEMEA SUALA LA KUJIUZULU KWA MASAUNI!!!

Kufuatia Sakata ndani ya Umoja wa Vijana CCM linalohusu mambo kadhaa likiwemo suala la Mwenyekiti wa Umoja huo Hamad Y.Masauni kuhusishwa na suala la kughushi cheti cha kuzaliwa,Sekretarieti ya Vijana CUF tunatoa pongezi kwa uamuzi wa kujiuzulu bwana Masauni kufuatia kashfa hiyo.

Tunampongeza Masauni kwa kufanya hivyo kwani ameonyesha ujasiri ukilinganisha na wanachama wengine wa chama hicho wanapotuhumiwa,alichofanya Masauni ni miongoni mwa sifa za kiongozi,tunampongeza kwani kitendo alichofanya si akatika utamaduni wa CCM pale wanapokumbwa na kashfa kuchukua uamuzi wa kuwajibika kwa staili hii.

Kitendo kilichofanywa na Masauni cha kughushi cheti si cha ajabu ndani ya CCM,wapo lukuki ila yeye ni kama kondoo tu wa kafara hivyo tunawakumbusha wana CCM kutomkalia kooni Masauni peke yake labda kama kuna agenda ya siri juu ya hili hasa ikizingatiwa kuna machafu mengi ndani ya chama hicho lakini hayajashikiwa bango kitu kinachopelekea wahusika wa mabaya hayo kama vile ufisadi na kughushi vyeti mbalimbali kuendelea kubaki madarakani na hata kutochukuliwa hatua zozote kama wanachama.

Cha kushangaza kama kweli Masauni kaghushi vyeti kwanini walimhifadhi muda wote huo? Kwanini Rais Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama naye alizidiwa na ujanja huu na hata akashabikia kuwa Uenyekiti wa Umoja huo apewe Masauni? Katika hili makosa yapo pande zote mbili(Chama na Masauni) hivyo kama ni hatua za kisheria zichukuliwe na zikate pande zote.

No comments:

Post a Comment