Monday, May 31, 2010

UTAMU WA SOKA HATA KWA VIONGOZI WA JUU DUNIANI!!


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon naye kumbe yumo kwenye usakataji wa kabumbu hapa akimuinua Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuzidiwa na shughuli ya usakataji wa kabumbu!!

BP YAENDELEA KUWA KATIKA WAKATI MGUMU!!


Hali bado ngumu kwa Kampuni ya Mafuta nchini Uingereza ya BP kutokana na kusema ina mpango wa kusitisha mpango wake wa kudhibiti uvujaji wa mafuta ambao unaendelea katika Ghuba ya Mexico. Hatua hiyo imekuja baada ya eneo la Amerika ya Kati kukumbwa na kimbunga cha Agatha ambacho kimefanya kazi iwe ngumu!!

Monday, May 24, 2010

LIYUMBA AHUKUMIWA MIAKA MIWILI!!




Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Amatus Liyumba amehukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya kuhusika katika matumizi mabaya ya fedha katika Ujenzi wa majengo pacha ya BOT!!!

JAMAICA KWA WAKA MOTO!!!




Mji Mkuu wa Jamaica Kingston umetawaliwa na machafuko baada ya serikali ya nchi hiyo kumshikilia Christopher Coke. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bruce Golding amesema jeshi lake lipo mbioni kudhibiti hali hiyo ili irejee kwenye utulivu kama awali!!!

UCHAGUZI ETHIOPIA!!!


Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia umekamilika huku Waziri Mkuu wa sasa Meles Zenawi akipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi. Tayari wapinzani nchini Ethiopia wameituhumu serikali ya kwamba imefanya wizi wa kura. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanataraji kutangazwa siku ya Jumanne!!!

WANANCHI SONGEA WATAKIWA KUCHANGAMKIA NAFASI ZA MASOMO!!!

Askofu mkuu wa Jimbo Katoliki la Songea, Mkoa wa Ruvuma , Mhashamu Norbert Mtega, amewataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za masomo zinazojitokeza humo.

Askofu Mtega amewataka wazazi kuhakikisha wanakuwa na mwamko wa elimu kwa kuwapeleka watoto wao shule badala ya fedha zao kuishia katika pombe na michango ya harusi.

Askofu Mtega ametoa mwito huo wakati akitoa ekaristi takatifu ya Kipaimara kwa waumini 100 wa kanisa hilo katika kanisa la Mtakatifu Agness lililopo Chipole Songea vijijini.

Amesema kumekuwa na fursa nyingi za masomo zinazojitokeza lakini mwamko wa wananchi wa wana-Ruvuma kujitokeza kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo ni mdogo mno.

Ametoa mfano na kusema kuwa Songea imebahatika kupata chuo cha Computer Science cha Mtakatifu Joseph ambacho kinasimamiwa na Mabinti wa Maria Imakulata (DMI) kutoka India lakini watu waliojiunga na chuo hicho wengi wao wanatoka Arusha, Moshi, Mbeya na kwingineko.

Anasema yeye ni Mwenyekiti wa bodi ya shule ya St. Joseph ambayo kwa bahati nzuri inachukua hata wanafunzi wa kidato cha Nne waliopata daraja la Tatu na Nne na kisha kuwaendeleza kwa miezi sita katika somo la Hesabu na Kiingereza ambapo wakifaulu wanaendelea na masomo hadi kupata Diploma na Digrii kwa gharama za serikali. (Habari kwa hisani ya Emmanuel Msingwa)

Amesema katika hali ya kushangaza akiwa Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ameshuhudia kuona wanafunzi wengi wanaokuja kujiunga na shule hiyo wanatokea katika mikoa mingine bila kuelewa sababu inayochangia hali hiyo.

CUF WALISEMEA SUALA LA KUJIUZULU KWA MASAUNI!!!

Kufuatia Sakata ndani ya Umoja wa Vijana CCM linalohusu mambo kadhaa likiwemo suala la Mwenyekiti wa Umoja huo Hamad Y.Masauni kuhusishwa na suala la kughushi cheti cha kuzaliwa,Sekretarieti ya Vijana CUF tunatoa pongezi kwa uamuzi wa kujiuzulu bwana Masauni kufuatia kashfa hiyo.

Tunampongeza Masauni kwa kufanya hivyo kwani ameonyesha ujasiri ukilinganisha na wanachama wengine wa chama hicho wanapotuhumiwa,alichofanya Masauni ni miongoni mwa sifa za kiongozi,tunampongeza kwani kitendo alichofanya si akatika utamaduni wa CCM pale wanapokumbwa na kashfa kuchukua uamuzi wa kuwajibika kwa staili hii.

Kitendo kilichofanywa na Masauni cha kughushi cheti si cha ajabu ndani ya CCM,wapo lukuki ila yeye ni kama kondoo tu wa kafara hivyo tunawakumbusha wana CCM kutomkalia kooni Masauni peke yake labda kama kuna agenda ya siri juu ya hili hasa ikizingatiwa kuna machafu mengi ndani ya chama hicho lakini hayajashikiwa bango kitu kinachopelekea wahusika wa mabaya hayo kama vile ufisadi na kughushi vyeti mbalimbali kuendelea kubaki madarakani na hata kutochukuliwa hatua zozote kama wanachama.

Cha kushangaza kama kweli Masauni kaghushi vyeti kwanini walimhifadhi muda wote huo? Kwanini Rais Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama naye alizidiwa na ujanja huu na hata akashabikia kuwa Uenyekiti wa Umoja huo apewe Masauni? Katika hili makosa yapo pande zote mbili(Chama na Masauni) hivyo kama ni hatua za kisheria zichukuliwe na zikate pande zote.

SNEIJDER KUREJEA REAL DE MADRID!!!


Kiungo wa Kimataifa wa Uholanzi anayesukuma gozi katika Klabu ya Inter Milan Wesley Sneijder amesema atarejea katika Klabu yake ya zamani ya Real De Madrid baada ya kupata mafanikio ya kutwaa mataji matatu akiwa katika Ligi ya Serie A kwenye msimu wake wa kwanza!!

Sunday, May 23, 2010

VITA YA INTER MILAN vs BAYERN MUNICH!!!














Mambo yalivyokuwa katika Uga wa Santiago Bernabeu wakati wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya. Inter Milan walifanikiwa kubeba mwali baada ya kuifunga Bayern Munich magoli 2-0!!!

MOURINHO SAFARI REAL DE MADRID!!


Kocha mwenye mbwembwe na tambo nyingi Jose Antonio Mourinho maarufuf kama Special One ametangaza nia yake ya kutaka kukinoa kikosi cha Real De Madrid baada ya kuipa ndoo tatu Inter Milan ikiwepo na ile ya Champions League. Mourinho amesema kama haujafundisha Real De Madrid utakuwa haujakamilika. Mourinho amesema ana uchungu sana kuona mechi dhidi ya Bayern Munich imekuwa ya mwihso kwake akiwa Inter Milan. Special One amesema kwa sasa ananyumba Stanford Bridge na San Siro na sasa anataka kuongeza Santiago Bernabeu.

Saturday, May 22, 2010

CHAMAKH ATUA RASMI ARSENAL!!


Klabu ya Arsenal imethibitisha kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco Marouane Chamakh kwa mkataba wa muda mrefu baada ya kumalizana na timu yake ya Bordeuax ya Ufaransa. Huu ni usajili wa kwanza Arsene Wenger kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi!!!

SAA CHACHE ZIMESALIA KABLA YA KUPATIKANA BINGWA!!!


Saa chache zimesalia kabla ya Bingwa wa mwaka huu wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya hajapatikana. Miamba Inter Milan inatarajiwa kuumana na Bayern Munich. Na tayari Kocha wa Inter Milan Jose Mourinho ameendelea kukataa kuongelea future yake hasa kutokana na kuhusishwa na kujiunga na Real Madrid!!!

AJALI YA NDEGE INDIA!!!



Takriban watu 158 ambao ni abiria wa Air India wamefariki dunia baada ya ndege waliyokuwa wanasafiria kuanguka katika Mji wa Mangalore wakati taarifa zikisema watu nane wamenusurika!!!

Friday, May 21, 2010

VITA YA DUNIA INTER MILAN vs BAYERN MUNICH!!



Vita ya Dunia inasubiri kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ambayo kwa mara ya kwanza inachezwa siku ya jumamosi tofauti na ilivyozoeleka huwa usiku wa Jumatano. Mchezo huo unawakutanisha Inter Milan wanaonolewa na Jose Antonio Mourinho dhidi ya Bayern Munich iliyochini ya Louis Van Gaal. J e nani kuibuka mbabe kati ya Special One Mourinho au Van Gaal??

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA CCM WILAYANI KYELA!!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Nawab Mullah kutokana na kifo cha Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kyela, Marehemu Japhet Mwakasumi, aliyefariki tarehe 19 Mei, 2010 Jijini Dar es Salaam.

Katika salamu zake hizo, Rais Jakaya Kikwete amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Marehemu Mwakasumi kilichotokea nyumbani kwake Ukonga – Banana, Jijini Dar es Salaam.

“Ninatambua vema mchango wa Marehemu Mwakasumi wakati wa uhai wake katika Wilaya ya Kyela hususan katika Chama Cha Mapinduzi kutokana na uhodari na uchapakazi wake ambao umeiwezesha CCM kuimarika zaidi, “amesema Rais Kikwete na kuongeza, “Kwa hakika kifo chake ni pigo kubwa kwa familia yake, wana – CCM na wananchi wote wa Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla”

Katika rambirambi zake kwa familia ya Marehemu Japhet Mwakasumi, Rais Kikwete amesema familia hiyo imepoteza kiongozi muhimu. Amewataka ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu Mwakasumi kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, na amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu Japhet Mwakasumi.

KIKOSI CHA SPAIN WORLD CUP!!

Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Jose Manuel 'Pepe' Reina (Liverpool), Victor Valdes (Barcelona).

Defenders: Raul Albiol (Real Madrid), Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Joan Capdevila (Villarreal), Carlos Marchena (Valencia), Gerard Pique (Barcelona), Carles Puyol (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).

Midfielders: Xabier Alonso (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), Cesc Fabregas (Arsenal), Andres Iniesta (Barcelona), Javier Martinez (Athletic Bilbao), David Silva (Valencia), Xavi Hernandez (Barcelona).

Forwards: Jesus Navas (Sevilla), Juan Manuel Mata (Valencia), Pedro Rodriguez (Barcelona), Fernando Llorente (Athletic Bilbao), Fernando Torres (Liverpool), David Villa (Valencia).

GRANT ABWAGA MANYANGA PORTSMOUTH!!



Kocha Mkuu wa Klabu ya Portsmouth Avram Grant ambaye ni raia wa Israel ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya kushindwa kuibakisha Timu huyo Ligi Kuu Nchini England. Grant amethibitisha kubwaga kwake manyanga baada ya hapo awali kuwepo uvumi!!

CUF WATOA KAULI MAUAJI YA KATIBU CCM MWANZA!!

CUF – Chama cha Wananchi tunawasihi Wagombea na Viongozi wa Vyama vya Siasa vya upinzani kwa ngazi zote kuwa makini juu ya usalama wao kuelekea uchaguzi mkuu ujao kutokana na dalili mbaya ya mauaji ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Isamilo mkoani Mwanza, Bahati Stephano yaliyofanyika wiki iliyopita,.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mauaji hayo yanahusishwa na tetesi za kisiasa na tayari watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo wamekamatwa akiwemo Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwani wa Kata hiyohiyo ya Isamilo, Bandiho Bihondo (64).

CUF – Chama cha Wananchi tumeshitushwa na mauaji hayo kufanyika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, na hasa ikizingatiwa kuwa aliyeuliwa alikuwa ni kiongozi wa chama cha siasa kilichoko madarakani na wanaotuhumiwa wanahusika kwa njia moja au nyingine ni wanachama wa chama hicho.

CUF – Kutokana na mazingira ya kifo hicho tunazidi kusisitiza na kuwaasa Wagombea na Viongozi wa vyama vya Siasa vya upinzani kwa ngazi zote kuwa macho na maisha yao, na waichukulie kuwa hii ni dalili ya hali ya hatari, kwa wale wagombea wa upinzani wanaokubalika katika maeneo yao, na viongozi waliomstari wa mbele katika ujenzi wa chama kiasi cha kuwa tishio katika maeneo yatakayogombewa hususani kwa wanaotaka kutetea nafasi zao.

CUF – Tunawasihi Wananchi wa Tanzania hususani wapiga kura wote kuwa makini na wagombea ambao wanaona nafasi walizonazo wanahati miliki nazo, kutoa fundisho kwa wagombea hao na chama chao cha CCM ili watambue kuwa nchi hii ni yetu sote na wananchi (wapiga kura) ndio wenye hati miliki ya nani ndie mstahiki wa kuongoza nchi kwa kipindi husika.

VILLA AKAMILISHA USAJILI BARCELONA!!



Mshambuliaji wa Kimataifa wa Spain David Villa amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Mabingwa wa La Liga Barcelona kitokea Valencia! Villa amesajiliwa kwa kitita cha pauni 34.2 na kusaini mkataba wa miaka minne kwa vijana hao wa Catalan!!!

Sunday, May 16, 2010

BAYERN MUNICH YATWAA TAJI LA PILI!!!


Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kutwaa ubingwa wake wa pili mwaka huu baada ya kushinda taji la Chama Cha Soka nchini Ujerumani kwa kuichakaza Werder Bremen kwa magoli manne bila ya jibu!! Magoli ya washindi wamefungwa na Arjen Robben, Ivica Olic, Franck Ribery na Bastian Schweinsteiger. Bayern wametinga pia fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya wakiwa na kibarua dhidi ya Inter Milan!!

BALLACK KUFANYIWA SCAN YA ENKA!!



Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack anafanyiwa scan ya kifundo chake cha mguu ambacho ameumia kwenye mchezo wa fainali ya FA dhidi ya Portsmouth. Ballack alipigwa daruga na Kevin Prince Boateng na hivyo yupo mashakani kushiriki fainali za Kombe la Dunia zinazoanza mwezi ujao nchini Afrika Kusini!!!

CHELSEA BINGWA FA!!








Klabu ya Chelsea maarufu kama The Blues wamefanikiwa kutwaa taji lao la pili msimu huu baada ya kuifunga Portsmouth maarufu The Pompey kwenye fainali ya FA kwa goli moja kwa nunge!! Hongereni Wazee wa Darajani kwa kuwa na mwaka wa mafanikio!!

Wednesday, May 12, 2010

NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA LIBYA!!


Watu zaidi ya mia moja wamepoteza maisha baada ya ndege ya Afriqiyah ya nchini Libya kuanguka katika Mji wa Tripoli! Mtoto wa miaka minane pekee ndiye ambaye amesalimika kwenye ajali hiyo! Ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ikitokea nchini Afrika Kusini!!

Sunday, May 9, 2010

SHERIA YA WALEMAVU YALILIWA!!!

Mkuu wa Kitengo Cha Walimu wenye ulemavu wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT Peter Mlimahadala amemuomba Rais Jakaya Kikwete kusaini haraka sheria ya Walemavu iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni ili ianze kutumika na kuwanusuru walemavu wengi ambao haki zao zinapotea.

Mwalimu Peter Mlimahadala ambaye alikuwa akikabidhi Msaada Baiskeli Mbili za walemavu kwa wanafunzi Wilayani Songea Mkoani Ruvuma pia ametaka Serikali ichukue hatua za haraka kuondoa kodi na kuweka ruzuku kwa vifaa vya walemavu ambavyo kwa sasa havinunuliki kutokana na kuuzwa bei kubwa.

Pamoja na kuomba kusainiwa haraka kwa sheria ya Walemavu ya mwaka 2010, Mlimahadala pia ameomba serikali kutafuta ufumbuzi wa tatizo la vifaa vya walemavu kuuzwa kwa bei ya juu akipendekeza Serikali itoe ruzuku kwa vifaa hivyo.

Aidha Amependkeza Vifaa vya walemavu ambavyo huingizwa hapa nchini kutoka nje ya nchi visitozwe kodi, ili viwafikie walemavu kwa bei nafuu.

Akiwa Mjini Songea Mwalimu Peter Mlimahadala amekabidhi Baiskeli mbili za walemavu zenye thamani ya zaidi shilingi milioni moja zilizotolewa na CWT ambacho ni chama pekee cha wafanyakazi chenye kitengo cha Walemavu. (Habari kwa Hisani ya Gerson Msigwa)

Saturday, May 8, 2010

KIKOSI CHA GHANA KWA WORLD CUP!!!


Goalkeepers: Richard Kingston (Wigan, England) Daniel Adjei (Liberty Professionals), Stephen Ahorlu (Hearts of Lions) , Stephen Adams (Aduana Stars)

Defenders: Samuel Inkoom (Basle, Switzerland), Hans Sarpei (Bayer Leverkusen, Germnay) Lee Addy (Bechem Chelsea), John Mensah (Sunderland, England), Rahim Ayew (Zamalek, Egypt), Isaac Vorsah (Hoffenheim, Germany), John Pantsil (Fulham, England), Jonathan Mensah (Granada, Spain) Eric Addo (Roda JC, Holland)

Midfielders: Dede Ayew (Arlese Avignon, France) Michael Essien (Chelsea, England) Kwadwo Asamoah (Udinese, Italy) Agyemang Badu (Udinese, Italy) Stephen Appiah (Bologna, Italy) Anthony Annan (Rosenborg, Norway) Haminu Dramani (Lokomotiv Moscow, Russia), Sulley Muntari (Inter Milan, Italy) Quincy Owusu-Abeyie (Al Sadd, Qatar), Derek Boateng (Getafe, Spain) Bernard Kumordzi (Panionios, Greece) , Laryea Kingston (Hearts, Scotland), Kevin-Prince Boateng (Portsmouth, England)

Strikers: Prince Tagoe (Hoffenheim, Germany) Asamoah Gyan (Rennes, France), Dominic Adiyiah (AC Milan, Italy), Matthew Amoah (NAC Breda, Holland)

MAGARI YA MASTAA WA ULAYA NA MAREKANI!!!








Haya ni baadhi ya magari ambayo yanatumiwa na Mastaa wa Ulaya na hata Marekani ambao wanayanunua kwa fedha nyingi sana. Sijui lini Mastaa wa hapa kwetu nao watafikia hapa na kuachana na kutamba na Vinadia vyao!!