Sunday, February 7, 2010

MANCHESTER UNITED YAFANYA MAUAJI!!!


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England Manchester United wameendeleza mbio zao za kuusaka ubingwa kwa mara ya nne kwa kasi baada ya kuifumua Portsmouth kwa magoli matano kwa buyu.

Mashetani hao Wekundu wakiwa katika Dimba lao la nyumbani la Old Trafford wamejikuta wakitoa kisago hicho kwa Portsmouth ambayo inaburuza mkia katika mchezo wa ligi ambao ulitawaliwa na mabingwa hao watetezi.

Magoli ya Manchester United wamekwamishwa nyauni na Wayne Rooney, Michael Carrick, Dimtry Berbato huku mengine mawili wakijifunga Portsmouth wenyewe na Anthony Vanden Borre na Marc Wilson.

Barclays Premier League
Bolton 0-0 Fulham
Burnley 2-1 West Ham
Hull 2-1 Man City
Liverpool 1-0 Everton
Man Utd 5-0 Portsmouth
Stoke 3-0 Blackburn
Sunderland 1-1 Wigan
Tottenham 0-0 Aston Villa

No comments:

Post a Comment