Thursday, July 1, 2010

MATUKIO YA WILAYANI MBINGA!!!


Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, mkoa wa Ruvuma, Kepteni John Komba akiwaambia wananchi wa kijiji cha Kingerikiti wilayani Mbinga (Hawapo pichani) kuwa haoni shida kufilisiwa fedha zote katika kutatua matatizo yao. Alisema bado ana kiu ya kutaka kuendelea kuwasaidia wananchi wa jimbo la Mbinga Magharibi lililopo katika wilaya ya Ziwa Nyasa ili waweze kuondokana na umaskin

Ukistaajabu ya Musa, Utayaona ya Filauni: Mwananchi huyu aliyejitambulisha kwa jina la Frank Sanga, akitumia ndoo ya lita 20 kunywa pombe ya kienyeji aina ya ‘Komoni’ kama alivyokutwa na kamera yetu katika kijiji cha Ilungu wilayani Makete hivi karibuni. Ofisa mtendaji wa kijiji cha Ilungu, Bw. Lumeo Sanga alisema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wazazi kuthamini sana pombe kuliko elimu kwa watoto wao.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Kanali mstaafu Edmund Mjengwa akipiga picha kikundi cha ngoma cha wanawake cha kioda katika kijiji cha Liparamba wilayani Ziwa Nyasa wakati kikitumbuiza katika mkutano wa serikali kuitambulisha wilaya mpya ya Ziwa Nyasa iliyotengwa kutoka wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma hivi karibuni

Mafuta ya Petrol yameanza kuuzwa kwenye makopo katika Kijiji cha Tingi Wilayani Mbinga ambapo lita moja inauzwa kwa shilingi 2,300/ (Picha na Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment