Monday, July 19, 2010

CUF WALIA NA ONGEZEKO LA UMASKINI NCHINI!!!

CUF – Chama cha Wananchi tumeshangazwa na kauli kuwa ongezeko la foleni za magari katika jiji la Dar es Salaam ni kipimo cha kuinua maisha bora kwa kila Mtanzania kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Vyombo vya Habari Rais Kikwete aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano huo wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais kwa asililmia 99.16, Dkt, Ali Mohamed Shein kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais Zanzibar na Dkt, Mohamed Gharib Bilal kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

CUF – Tumeshangazwa na propaganda aliyoitumia Rais Kikwete kwa kuwalaghai Wananchi ambao wengi wao ndio wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na umasikini unaoongezeka siku hadi siku, huku wakati huo huo mazingira ya ongezeko la kiuchumi yakiimarika zaidi kwa walionacho, mafisadi, wala rushwa na viongozi wa serikali wanaosaini mikataba hewa na waliojilimbikizia posho kubwa kubwa na ziara nyingi za nje na ndani ya nchi ambao ndio wanaosababisha ongezeko kubwa la magari nchini pamoja na wenye vipato halali wachache sana wenye uwezo huo.

CUF – Tunatambua kuwa wakati walionacho wakiongeza magari, mipango mingi ya serikali pamoja na utekelezaji wa sera mbovu za CCM zinaendelea kumdumaza mwananchi wa kipato cha chini kushindwa hata kuongeza baiskeli moja, baada ya ile ya zamani kuchakaa na kubaki kuishi kwa pato la chini ya dola moja kwa siku.

CUF – Tunawatanabaisha Watanzania wote kuwa makini na kauli za propaganda za Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, watakuja na vigezo vingi vya kuzusha ili kuonyesha ufanisi hewa wa utekelezaji wa sera zao, hivyo ni wajibu kuwapa fundisho kuwa wakati wa Watanzania kudanganyika umekwisha kwa kuhakikisha mnachagua viongozi wapya kutoka chama chenu cha Wananchi (CUF) kitakacho jali maslahi na haki za raia wote kwa usawa.

No comments:

Post a Comment