Monday, July 12, 2010

MATUKIO YA SONGEA WEEKEND!!!


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma, Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Lizaboni mjini Songea wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Bw. Athuman Mhina. Jumuiya hiyo imeazimia kuhamasisha ujenzi wa mabweni katika shule zote za kata nchini ili kudhibiti mimba kwa watoto wa kike.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Bw. Athuman Mhina (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma, Stella Manyanya (kushoto) katika mkutano wa kuelelezea shughuli za Jumuiya hiyo kwa wananchi wa Kata ya Lizaboni mjini Songea jana. Katikati ni Mwenyekiti wa balaza la wazazi mkoa wa Ruvuma, Bw. Willy Kayomb



Baadhi ya noti za fedha zenye thamani ya zaidi ya Milioni moja za mkazi mmoja wa kijiji cha Mpitimbi, wilaya ya Songea, Bw. Mathias Kikolwe zikiwa zimeharibika vibaya kutokana na kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa miaka mitatu. Bw. Kikolwe ambaye hakutaka kupigwa picha alijikuta akiangua kilio kikubwa mbele za watu mara baada ya kujibiwa na mmoja wa wafanyabiashara kuwa fedha hizo haziwezi kutumika tena (Picha kwa hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment