Tuesday, July 27, 2010

BALOZI WA JUMUIYA YA ULAYA AKIWA ZIARANI MBINGA!!!


BALOZI wa Jumuiya ya nchi za Ulaya Tanzania (EU), Bw. Timothy Clarke (kushoto) na Katibu mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushiria, Bw. Mohamed Muya (katikati) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Kanali mstaafu Edmund Mjengwa wakati wakitembelea shamba la mfano la Kituo cha utafiti wa kahawa cha TaCRI-Ugano wilayani Mbinga

Mkulima Bi. Alfeda Mapunda mkazi wa kijiji cha Myangayanga wilayani Mbinga, mkoa wa Ruvuma akitoa maelekezo ya uzalishaji wa kahawa ya vikonyo kwa Balozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya Tanzania (EU), Bw. Timothy Clarke (wa mwisho kushoto) mara alipomtembelea mkulima huyo kuona shughuli zake za kilimo cha Kahawa baada ya kupata mafunzo kutoka Kituo cha TaCRI-Ugano cha Mbinga (Picha na Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment