Saturday, July 3, 2010

MATUKIO MBALIMBALI MIKOA YA KUSINI!!!!


Wananchi wa mtaa wa Mahenge mjini Songea wakichangishana fedha kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu hivi karibuni wakati wa mkutano wa kuunda kamati ya kusimamia mfuko wa kusaidia watoto hao katika mtaa huo

Wanafunzi wa mwaka wa Tatu, Semista ya Sita wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha St. Joseph kilichopo mjini Songea mkoa wa Ruvuma, Bi. Olivia Masange (kulia) na Bi. Sophia Kalinga wakisoma vitabu kupitia mtandao katika maktaba ya chuo hicho mara baada ya kuzinduliwa juzi na mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bi. Christine Ishengoma

Suala la utunzaji wa mazingira katika halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma linaonekana kukosa mwamko miongoni mwa wananchi walio wengi kama inavyoonekana pichani wananchi wakiendelea kutupa takataka eneo ambalo kuna kibao kilichopiga marufuku kutupa takataka

Mdau wa Blogu hii Emmanuel Msigwa (kulia) akizungumza na Ofisa mtendaji wa kijiji cha Ilungu, kata ya Ipepo wilayani Makete, Lumeo Sanga juu ya kudorora kwa elimu katika kijiji hicho kutokana na kukithiri kwa imani za kishirikina miongoni mwa wananchi

No comments:

Post a Comment