Monday, July 26, 2010

MATUKIO YA KANDA YA KUSINI!!!


Mgombea ubunge jimbo la Songea mjini kupitia CCM, Bw. Oliver Mhaiki akiongea na wananchi na wanachama wa kata ya Ruvuma mjini hapa kwa lengo la kuomba kura ili aweze kuchaguliwa katika kinyang'anyiro cha kiti hicho Agosti Mosi mwaka huu

Jumla ya wagombea Wanne wanaowania nafasi ya ubunge katika jimbo la Songea mjini, mkoa wa Ruvuma kupitia tiketi ya CCM wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Chama hicho Songea mjini kikiwapitisha kwa wananchi na wanachama kwa lengo la kuwanadi na kusikiliza sera zao. Kutoka kushoto ni Bw, Renatus Mkinga, Bw. Oliver Mhaiki, Bw. Emmanuel Nchimbi na Bw. Mohamed Slim

Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini (CCM), Bw. Renatus Mkinga akiomba kura kwa wanachama wa kata ya Mateka mjini hapa huku akiahidi kutatua tatizo sugu la umeme mjini Songea ili kuvuia wawekezaji na kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali

Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini (CCM), Bw. Emmanuel Nchimbi akiomba kupewa kura za kuendelea kuongoza jimbo hilo kwa wanachama wa kata ya Ruvuma mjini hapa huku akionesha kitabu kilichoandikwa mambo aliyotekeleza katika kipindi chake cha ubunge cha miaka Mitano

Mjasiliamali ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akijaribu kumshawishi mteja kununua ndizi katika eneo la Mkongo wilayani Namtumbo, mkoa wa Ruvuma. Wanawake wa eneo hilo wanasifika kwa kujituma katika shughuli za biashara ndogo ndogo katika kujikwamua na umaskini

Gari ikiwa imebeba shehena ya mzigo wa Tumbaku kuipeleka katika maghala ya kiwanda cha Songea na Namtumbo (SONAMCU) kilichopo Songea mjini baada ya kukusanywa kutoka kwa wakulima wa Wilaya ya Namtumbo, mkoa wa Ruvuma tayari kuisafirisha kwenda mikoa ya Morogoro na Tabora inakosindikwa (Shukran Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment