Tuesday, July 20, 2010

HARAKATI ZA KUWANIA UBUNGE SONGEA!!!


Wagombea wa kiti cha ubunge jimbo la Songea mjini, Bw. Oliver Mhaiki (kulia) akisalimiana na mgombea mwenza Bw. Hassan Moyo nje ya ofisi ya CCM mjini Songea mara baada ya kutoka kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Kaimu katibu wa CCM Songea mjini, Bw. Zongo Lobezongo (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Songea mjini, Bw. Hassan Moyo baada ya kukidhi masharti ya kutoa kiasi cha sh. 100,000 kwa ajili ya fomu hiyo

Katibu wa CCM wilaya ya Songea vijijini Bi. Lydia Gunda (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Peramiho Bw. Joseph Mhagama baada ya kukidhi masharti ya kutoa kiasi cha sh. 100,000 kwa ajili ya fomu hiyo huku akitoa ahadi ya kulipa kiasi kingine cha sh. Milioni Moja kesho yake.

Mgombea wa ubunge jimbo la Songea mjini Bw. Oliver Mhaiki akimueleza Kaimu Katibu wa CCM Songea mjini Bw. Zongo Lobezongo kuwa hawezi kuchangia kiasi cha sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya kuimarisha chama na kusaidia kampeni kutokana na kupewa taarifa hiyo ghafla

Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini, Bw. Hassan Moyo akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa wananchi wa Songea mjini mara baada ya kutoka kuchukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Songea mjini (Picha kwa Hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment