Monday, August 2, 2010

MATUKIO MBALIMBALI MWISHONI MWA JUMA!!!


Mwenge wa Uhuru ukivushwa katika Mto Ruhuhu kutoka wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma kuingia katika wilaya ya Ludewa mkoa wa Iringa kwa kutumia kivuko cha Mv Ruhuhu baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Ruvuma

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma, Anselm Tarimo (kulia) akimkabidhi mwenge wa uhuru Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka (kushoto) mpakani mwa wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma na Ludewa mkoa wa Iringa baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake katika mkoa wa Ruvuma

Mkazi huyu ambaye jina lake halikupatikana akiwa amelewa chakali huku akiwa na chupa zingine za bia zaidi ya Nne ambazo hazijafunguliwa katika mkesha wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa uliokesha katika kijiji cha Ruanda wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa, Nassoro Matuzya akimfariji mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Emmanuel Mapunda mwanafunzi wa shule ya msingi Lukarasi wilayani Mbinga na kulazimika kuendesha harambee ya kumchangia mtoto huyo ambapo zilipatikana fedha zaidi ya 350,000 ili ziweze kumsaidia

Kasto Turuka (aliyeshika usukani) mkazi wa Mbinga mjini akitoa maelekezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa, Nassoro Matuzya namna anavyotengeneza pikipiki ya miguu Minne kwa kutumia mabati, vyuma chakavu na injini ya pikipiki. Matuzya alimuomba mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anamsaidia kijana huyo kupata namba za usajili wa vyombo vyao ili viweze kutumika na kufanya kazi kisheria

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa, Nassoro Matuzya (kulia) akitoa ujumbe wa mbio za mwenge huo katika kijiji cha Miembeni wilayani Mbinga wakati wa makabidhiano ya mwenge kutoka wilaya ya Songea vijijini kwenda wilayani humo. Kushoto aliyeshika kidevu ni Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa akisikiliza kwa makini ujumbe huo

Mkulima Gabriel Mbano mkazi wa kijiji cha Myangayanga, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma, akikagua miti ya kahawa katika shamba lake na kuifanyia usafi ili iweze kuzalisha kahawa bora na nyingi zaidi (Mambo yote na Mdau Emmanuel Msigwa)

No comments:

Post a Comment