Tuesday, July 27, 2010
BALOZI WA JUMUIYA YA ULAYA AKIWA ZIARANI MBINGA!!!
BALOZI wa Jumuiya ya nchi za Ulaya Tanzania (EU), Bw. Timothy Clarke (kushoto) na Katibu mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushiria, Bw. Mohamed Muya (katikati) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Kanali mstaafu Edmund Mjengwa wakati wakitembelea shamba la mfano la Kituo cha utafiti wa kahawa cha TaCRI-Ugano wilayani Mbinga
Mkulima Bi. Alfeda Mapunda mkazi wa kijiji cha Myangayanga wilayani Mbinga, mkoa wa Ruvuma akitoa maelekezo ya uzalishaji wa kahawa ya vikonyo kwa Balozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya Tanzania (EU), Bw. Timothy Clarke (wa mwisho kushoto) mara alipomtembelea mkulima huyo kuona shughuli zake za kilimo cha Kahawa baada ya kupata mafunzo kutoka Kituo cha TaCRI-Ugano cha Mbinga (Picha na Mdau Emmanuel Msigwa)
Monday, July 26, 2010
MATUKIO YA KANDA YA KUSINI!!!
Mgombea ubunge jimbo la Songea mjini kupitia CCM, Bw. Oliver Mhaiki akiongea na wananchi na wanachama wa kata ya Ruvuma mjini hapa kwa lengo la kuomba kura ili aweze kuchaguliwa katika kinyang'anyiro cha kiti hicho Agosti Mosi mwaka huu
Jumla ya wagombea Wanne wanaowania nafasi ya ubunge katika jimbo la Songea mjini, mkoa wa Ruvuma kupitia tiketi ya CCM wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Chama hicho Songea mjini kikiwapitisha kwa wananchi na wanachama kwa lengo la kuwanadi na kusikiliza sera zao. Kutoka kushoto ni Bw, Renatus Mkinga, Bw. Oliver Mhaiki, Bw. Emmanuel Nchimbi na Bw. Mohamed Slim
Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini (CCM), Bw. Renatus Mkinga akiomba kura kwa wanachama wa kata ya Mateka mjini hapa huku akiahidi kutatua tatizo sugu la umeme mjini Songea ili kuvuia wawekezaji na kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali
Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini (CCM), Bw. Emmanuel Nchimbi akiomba kupewa kura za kuendelea kuongoza jimbo hilo kwa wanachama wa kata ya Ruvuma mjini hapa huku akionesha kitabu kilichoandikwa mambo aliyotekeleza katika kipindi chake cha ubunge cha miaka Mitano
Mjasiliamali ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akijaribu kumshawishi mteja kununua ndizi katika eneo la Mkongo wilayani Namtumbo, mkoa wa Ruvuma. Wanawake wa eneo hilo wanasifika kwa kujituma katika shughuli za biashara ndogo ndogo katika kujikwamua na umaskini
Gari ikiwa imebeba shehena ya mzigo wa Tumbaku kuipeleka katika maghala ya kiwanda cha Songea na Namtumbo (SONAMCU) kilichopo Songea mjini baada ya kukusanywa kutoka kwa wakulima wa Wilaya ya Namtumbo, mkoa wa Ruvuma tayari kuisafirisha kwenda mikoa ya Morogoro na Tabora inakosindikwa (Shukran Mdau Emmanuel Msigwa)
Tuesday, July 20, 2010
HARAKATI ZA KUWANIA UBUNGE SONGEA!!!
Wagombea wa kiti cha ubunge jimbo la Songea mjini, Bw. Oliver Mhaiki (kulia) akisalimiana na mgombea mwenza Bw. Hassan Moyo nje ya ofisi ya CCM mjini Songea mara baada ya kutoka kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Kaimu katibu wa CCM Songea mjini, Bw. Zongo Lobezongo (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Songea mjini, Bw. Hassan Moyo baada ya kukidhi masharti ya kutoa kiasi cha sh. 100,000 kwa ajili ya fomu hiyo
Katibu wa CCM wilaya ya Songea vijijini Bi. Lydia Gunda (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Peramiho Bw. Joseph Mhagama baada ya kukidhi masharti ya kutoa kiasi cha sh. 100,000 kwa ajili ya fomu hiyo huku akitoa ahadi ya kulipa kiasi kingine cha sh. Milioni Moja kesho yake.
Mgombea wa ubunge jimbo la Songea mjini Bw. Oliver Mhaiki akimueleza Kaimu Katibu wa CCM Songea mjini Bw. Zongo Lobezongo kuwa hawezi kuchangia kiasi cha sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya kuimarisha chama na kusaidia kampeni kutokana na kupewa taarifa hiyo ghafla
Mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini, Bw. Hassan Moyo akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa wananchi wa Songea mjini mara baada ya kutoka kuchukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Songea mjini (Picha kwa Hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)
Monday, July 19, 2010
CUF WALIA NA ONGEZEKO LA UMASKINI NCHINI!!!
CUF – Chama cha Wananchi tumeshangazwa na kauli kuwa ongezeko la foleni za magari katika jiji la Dar es Salaam ni kipimo cha kuinua maisha bora kwa kila Mtanzania kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Vyombo vya Habari Rais Kikwete aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano huo wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais kwa asililmia 99.16, Dkt, Ali Mohamed Shein kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais Zanzibar na Dkt, Mohamed Gharib Bilal kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
CUF – Tumeshangazwa na propaganda aliyoitumia Rais Kikwete kwa kuwalaghai Wananchi ambao wengi wao ndio wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na umasikini unaoongezeka siku hadi siku, huku wakati huo huo mazingira ya ongezeko la kiuchumi yakiimarika zaidi kwa walionacho, mafisadi, wala rushwa na viongozi wa serikali wanaosaini mikataba hewa na waliojilimbikizia posho kubwa kubwa na ziara nyingi za nje na ndani ya nchi ambao ndio wanaosababisha ongezeko kubwa la magari nchini pamoja na wenye vipato halali wachache sana wenye uwezo huo.
CUF – Tunatambua kuwa wakati walionacho wakiongeza magari, mipango mingi ya serikali pamoja na utekelezaji wa sera mbovu za CCM zinaendelea kumdumaza mwananchi wa kipato cha chini kushindwa hata kuongeza baiskeli moja, baada ya ile ya zamani kuchakaa na kubaki kuishi kwa pato la chini ya dola moja kwa siku.
CUF – Tunawatanabaisha Watanzania wote kuwa makini na kauli za propaganda za Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, watakuja na vigezo vingi vya kuzusha ili kuonyesha ufanisi hewa wa utekelezaji wa sera zao, hivyo ni wajibu kuwapa fundisho kuwa wakati wa Watanzania kudanganyika umekwisha kwa kuhakikisha mnachagua viongozi wapya kutoka chama chenu cha Wananchi (CUF) kitakacho jali maslahi na haki za raia wote kwa usawa.

HARAKATI ZA KUSAKA UBUNGE ZAZIDI KUPAMBA MOTO!!!
Mkurugenzi wa shirika la Wanaharakati wanaojishughulisha na masuala ya Utawala bora, Maendeleo na Haki za binadamu (AFDF), Renatus Mkinga (kushoto) akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Songea Mjini huku akionesha moja ya karatasi yenye sifa za mbunge alizodai ni bandia na kuahidi kuwapelea mahakamani wabunge wote wenye vyeti bandia endapo atachaguliwa. Kulia na Makamu mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Ruvuma , Muhidin Amri. (Picha na Mdau Emmanuel Msigwa)
Monday, July 12, 2010
RAIS MUSEVENI ATEMBELEA MAJERUHI!!!
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ametembelea Hospital kuwaangalia majeruhi waliotokana na mashambulizi mawili ya milipuko ya mabomu iliyotokea nchini humo na kuhusishwa na Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab kutoka Somalia. Watu sabini na nne wameelezwa kupoteza maisha na wengine sabini wakijeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyotokea katika Klabu ya Raga na Mgahawa wa Ethiopia!!!
SPAIN WATUA KWAO WAKIWA MASHUJAA!!!
MIKONO IKIWA IMESHIKA KOMBE- WOZA 2010!!!
PICHA BORA YA WOZA 2010 NA WALA SI KARATE!!!
JUMUIYA YA WAZAZI SONGEA YALIVALIA NJUGA SUALA LA MIMBA!!!
JUMUIYA ya wazazi nchini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), imejipanga kufufua jumuiya hiyo inayodaiwa kuanza kufa kwa kuhakikisha kuwa inajenga mabweni ya wanafunzi katika shule zote za sekondari za kata ili kutokomeza mimba kwa watoto wa kike.
Aidha, Jumuiya hiyo imejipanga kuzunguka nchi nzima kuelezea na kuweka wazi shughuli zake kwa wananchi ili waitambue na kuweza kujiunga kwa wingi zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanachama.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Bw. Athumani Mhina wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati maalumu ya wazazi mkoani Ruvuma pamoja na wananchi wa kata ya Lizaboni mjini Songea.
Amesema kasi ya wanafunzi kupata ujauzito Tanzania kwa sasa ni kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma hali ambayo inatishia kuwa na kizazi kisicho na elimu na kwamba wazazi wenyewe ndiyo wenye jukumu la kwanza kutokomeza hali hiyo kwa kujenga mabweni ya wanafunzi hao katika shule zote za kata.
Ameeleza kuwa kitendo kuwaachia watoto hao kutembea umbali mrefu kwenda shule kila siku ni kuwapa nafasi kubwa mafataki kuwaingiza katika vishawishi mbalimbali na hatimaye kuwajaza mimba na kisha kuwatelekeza na kuwaacha wakihangaika peke yao.
Mhina pia ameoneshwa kusikitishwa na baadhi ya tabia ya wazazi ambao wameshindwa kuheshimu watoto wa wenzao na kuamua kufanya nao mapenzi na kuwaingiza katika matatizo makubwa badala ya wao kuwa walimu na walinzi wa watoto hao.
Mbali na hayo, pia Mhina amewaomba wazazi nchini kuhakikisha ujenzi wa mabweni hayo ya wanafunzi yaende sambamba na ujenzi wa nyumba za walimu ili kuwafanya walimu hao kudumu na kuipenda kazi yao.
Amesema walimu wengi wanashindwa kufanya kazi yao na kulazimika kuacha kazi hiyo ama kuhamia maeneo mengine yenye unafuu kutokana na kufanya kazi katika mazingira mabovu yasiyovumilika. (Habari kwa hisani ya Emmanuel Msigwa)

MATUKIO YA SONGEA WEEKEND!!!
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma, Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Lizaboni mjini Songea wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Bw. Athuman Mhina. Jumuiya hiyo imeazimia kuhamasisha ujenzi wa mabweni katika shule zote za kata nchini ili kudhibiti mimba kwa watoto wa kike.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa, Bw. Athuman Mhina (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma, Stella Manyanya (kushoto) katika mkutano wa kuelelezea shughuli za Jumuiya hiyo kwa wananchi wa Kata ya Lizaboni mjini Songea jana. Katikati ni Mwenyekiti wa balaza la wazazi mkoa wa Ruvuma, Bw. Willy Kayomb
Baadhi ya noti za fedha zenye thamani ya zaidi ya Milioni moja za mkazi mmoja wa kijiji cha Mpitimbi, wilaya ya Songea, Bw. Mathias Kikolwe zikiwa zimeharibika vibaya kutokana na kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa miaka mitatu. Bw. Kikolwe ambaye hakutaka kupigwa picha alijikuta akiangua kilio kikubwa mbele za watu mara baada ya kujibiwa na mmoja wa wafanyabiashara kuwa fedha hizo haziwezi kutumika tena (Picha kwa hisani ya Mdau Emmanuel Msigwa)
WACHEZAJI BORA WOZA 2010!!
SPAIN BINGWA WOZA 2010!!!
Timu ya Taifa ya Spain imefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuifunga Holland katika mchezo wa fainal kwa goli moja kwa nunge. Goli hilo limefungwa na kiungo Andrea Iniesta ambaye pia alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo. Kwa matokeo hayo Spain inafanikiwa kuwa bingwa na kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa ikiwa na magoli machache, kufungwa mechi ya kwanza ya mashindano na pia kuwa timu ya kwanza kutoka bara la Ulaya kutwaa ubingwa nje ya bara hilo!!!
Friday, July 9, 2010
BELHADJ ATIMKIA QATAR!!!!
LE BRON JAMES AITWA MSALITI NA MASHABIKI WA CLEVELAND!!!
Thursday, July 8, 2010
HOWARD WEBB KUCHEZESHA FAINAL WOZA 2010!!!
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limemtangaza Mwamuzi kutoka nchini Uingereza Howard Webb kuchezasha mchezo wa fainal wa Kombe la Dunia utakaopigwa siku ya jumapili kwenye Dimba la Soccer City. FIFA imemtangaza mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 38 akisaidiwa na Michael Mullarkey na mwenzake Darren Cann na kuwa mwamuzi wa kwanza kutoka Uingereza tangu mwaka 1974. Mchezo huo wa jumapili unatarajiwa kuwakutanisha Holland dhidi ya Spain!!!
FIFA KUFANYA MABADILIKO YA WAAMUZI!!!
Wednesday, July 7, 2010
BARCELONA YASHINDWA KUWALIPA WACHEZAJI MSHAHARA WA JUNE!!!
WOZA 2010-SPAIN YAIFUATA HOLLAND SOCCER CITY KWA FAINAL!!
Subscribe to:
Posts (Atom)