Monday, January 18, 2010

RAIS KIKWETE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA!!!

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Jumatatu, Januari 18, 2010, amewapatia wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, gari la wagonjwa, ili kupunguza shida ya usafiri wa wagonjwa katika eneo hilo.

Katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Mheshimiwa Kikwete amekabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Mbozi, Bwana Levison Jeremiah Chilewa.

Mheshimiwa Kikwete aliwaahidi wananchi wa Kamsamba gari hilo wakati alipotembelea eneo hilo mwishoni mwa mwaka jana.

MASHAMBULIZI NCHINI AFGHANISTAN!!!


Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul umekumbwa na mashambulizi mapema ya siku ya jumatatu mara baada ya Wanamgambo wa Kundi la Taliban kufanya shambulizi lililolenga Wizara za nchi hiyo. Taarifa za Wanamgambo wa Taliban zimethibitisha kuhusika kwao na kuongeza nia yao ilikuwa ni kushambulia Makazi ya Rais ya nchi hiyo. Jumla ya watu watano wanasemekana kuuawa huku wengine zaidi ya thelathini wakijeruhiwa.

HENRY KUKUTANA NA RUNGU LA FIFA!!!!


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ufaransa na Barcelona, Thiery Henry ameitwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA kwa ajili ya sakata la kushika mpira katika mechi yao ya kusaka nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia. Henry alishika mpira mara mbili katika mechi dhidi ya Jamhuri ya Ireland kabla hajapiga krosi iliyowekwa kimiani na William Gallas. Sakata la Henry kushika mpira kabla ya kufungwa kwa goli lilizua utata na kutaka kutia dosari mashindano ya mwaka yatakayofanyika nchini South Africa.

ESSIEN AONDOLEWA KIKOSI CHA GHANA!!!!


Kiungo wa Kimataifa wa Ghana ambaye anakipiga katika Klabu ya Chelsea, Michael Essien ameondolewa katika Kikosi cha timu hiyo kutokana na kuumia goti katika mzoezi ya Timu hiyo. Kiungo huyo wa Black Stars amepata maumivu hayo akiwa katika Mji wa Cabinda kwenye mazoezi ya kawaida. Essien kuumia kwake kutakuwa pigo kwa timu hiyo kutokana na mchezaji huyo kucheza kipindi kimoja katika mechi na Ivory Coast.
Kwa sasa Ghana itamkosa Essien katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Burkina Faso.

Sunday, January 17, 2010

NCCR MAGEUZI KUIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI!!!

Chama Cha NCCR Mageuzi kimetangaza nia yake ya kuiburuza serikali Mahakamani iwapo itashindwa kufanya marekebisho kwenye miswada miwili ya sehria ya uchaguzi ambayo itapelekwa bunge katika Mkutano wa Kumi na Nane. Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Samweli Ruhuza ametangaza nia ya Chama chake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Chama hicho Ilala Dar Es Salaam.

CHEMICAL ALLY AHUKUMIWA KIFO!!!!


Ali Hassan al-Majid maarufu kama Chemical Ali mmoja wa watuhumiwa walioshiriki katika mauaji ya Wakurdi zaidi ya laki moja na elfu themanini amehukumiwa adhabu ya kifo. Chemical Ali alikuwa mshirika wa karibu wa Rais wa zamani wa Iraq Marehemu Saddam Hussein

TAMASHA LA ELIMIKA NA BONGO FLAVOUR!!!




MACHATA YA NGUO ZA KIBONGO!!!!





Siku hizi fulana na Tshirt ambazo zinamaneno ya kiswahili zimekuwa maarufu sana kwa Vijana. Kila sehemu unakutana na watu wakiwa wamevaa fulanazz zenye maneno mbalimbali mathalani Umefulia, Kaza Buti na mfano wa hivyo. Lakini chata hizi ni za makundi ya muziki hapa nchini. Huree Tz nasi tunaweza!!

MAPHARAO WATINGA ROBO FAINAL, SUPER EAGLES WASHINDA!!!





Mchuano wa Dimba la Mataifa ya Afrika umeendelea kutimua vumbi nchini Angola na kushuhudia Mabingwa watetezi Misri "Pharaos" wakitinga hatua y Robo Fainal wakati Nigeria "Super Eagles" wakishindwa kwa tabu goli 1-0.

YANGA YAANZA KWA USHINDI MZUNGUKO WA PILI, LEO ZAMU YA SIMBA!!!



Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa lala kwa buriani umeanza jana na kushuhudia Mabingwa watetezi Yanga wakivuna ushindi wa magoli mawili kwa nunge mbele ya African Lyon kwa magoli ya Jerryson Tegete na Mrisho Ngasa. Leo ni zamu ya vinara wa ligi hiyo Simba ambao wanakibarua dhidi ya Majimaji ya Songea

CHELSEA YAUA, MAN UTD YACHOMOZA NA USHINDI!!!







Vinara wa Ligi Kuu Nchini England Matajiri wa kutupwa wa Jiji la London, Chelsea wameendelea kujiimarisha kileleni baada ya kuvuna ushindi wa magoli 7-2. Mashetani Wekundu Manchester United wenyewe wameshinda 3-0. Manchester City wamekumbana na shubiri chini ya Kocha wao mpya Roberto Mancini baada ya kufungwa magoli 2-0 na Everton.

Barclays Premier League
Chelsea 7-2 Sunderland
Everton 2-0 Man City
Man Utd 3-0 Burnley
Stoke 1-1 Liverpool
Tottenham 0-0 Hull
Wolverhampton 0-2 Wigan

Saturday, January 16, 2010

LIVERPOOL MWAKA WA SHETANI!!!!



Bwawa La Maini mambo yanazidi kuwaelemea kwani katika mchezo wake dhidi ya Stoke City wameambulia sare. Liverpool ambo walikuwa wakwanza kupata goli wamejikuta wakiruhusu goli la kusawazisha katika dakika ya 90 ya hivyo matokeo kuwa 1-1. Kweli kisicho riziki hakiliki waswahili wamesema

IVORY COAST YAFUZU ROBO FAINALI - AFCON!!!









Kikosi cha Tembo wa Africa Ivory Coast imekuwa timu ya kwanza kutinga katika hatua ya robo fainali baada ya kuvuna ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Ghana Black Stars. Magoli ya Ivory Coast yamefungwa na Gervinho, Siaka Tiene na Didier Drogba wakati la Ghana limepachikwa nyavuni na Asamoah Gyan.

Friday, January 15, 2010

CAMPBELL ASAJILIWA TENA ARSENAL!!!


Klabu ya Arsenal haitimaye imemsajili tena beki wake wa zamani Mkongwe Sol Campbell mwenye umri wa miaka 35. Campbell ambaye almanusra ajiunge na Manchester United amekamilisha usajili wake na Kujiunga na Washika Bunduki wa Jiji la London. Campbell amekuwa hana klabu ya kuchezea tangu mwezi December baada ya kuachwa na Notts County

BENITEZ AOMBA RADHI MASHABIKI!!!!


Kocha Mkuu wa Liverpool Rafael Benitez amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kushuhudia wakitolewa kwenye Kombe la Chama Cha Soka Nchini England FA kunako raundi ya tatu. Liverpool imeondolewa katika FA baada ya kupigwa magoli 2-1 na Reading

WAKALI WA MLIMANI TV WAKIWA KAZINI!!!!!




Hawa ni baadhi tu ya wale ambao wanakisimamisha kituo cha Mlimani Tv kwenye kazi. Anuary Mkama Mkuu wa kazi akifanya interview na Nahodha wa Malindi ya Zanzibar. Saleh Masoud maarufu kama Jecha akiwa amekamata Kamera yake. Juu ni Sylvia Mwehozi akiwa na Mama Nyerere. Ninavyomjua huyu binti hii picha itakuwa imebandikwa sebuleni kwao.

LIGI MZUNGUKO WA PILI KUANZA KESHO!!



Mabingwa watetezi Yanga wanatarajiwa kuanza mzunguko wa Pili wa ligi kesho kwa kucheza na wabaya wao African Lyon. Yanga watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare na African Lyon katika mzunguko wa kwanza. Vijana hao wanaonolewa na Kostadin Papic maarufu kama Clinton watakuwa na kibarua cha kuanza vizuri hatua hii ya lala kwa buriani.

MISAADA YAANZA KUWASILI NCHINI HAITI!!!!



Mashirika mbalimbali ya Misaada yameanza kupeleka misaada nchini Haiti kuwasaidia manusuru wa janga la Tetemeko la Ardhi ambalo limepiga nchi hiyo. Manusura wengi wanahitaji maji, chakula, malazi pamoja na msaada wa matibabu wa haraka.
Takwimu za Shirika la Msalaba Mwekundu zinaonesha watu zaidi ya elfu 50 wamepoteza maisha huku majeruhi wakiwa milioni 3.
Miili imeendelea kuzagaa katika mitaa ya nchi hiyo kutokana na zoezi la kuikosanya kwenda taratibu kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kutosha na vya uhakika.

Thursday, January 14, 2010

ANGOLA YAWEKA HAI MATUMAINI YA KUTINGA ROBO FAINALI




Wenyeji wa Michuano ya AFCON Angola wameweka hai matumaini ya kutinga katika hatua ya Robo Fainali baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Malawi. Angola ambao katika mchezo wa kwanza waliambulia sare ya magoli 4-4 dhidi ya Mali wameshinda mchezo wao dhidi ya Malawi kwa 2-0. Magoli ya Angola yamefungwa na washambuliaji wake hatari Flavio na Manucho.

MALI HOI MBELE YA ALGERIA - AFCON!!!



Hatimaye Algeria inakuwa Timu ya kwanza miongoni mwa tano ambazo zitaiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia kupata ushindi. Algeria wamefanikiwa kuvuna ushindi baada ya kuifunga Mali kwa goli moja kwa buyu. Goli hilo la Wawakilishi hao wa Bara la Afrika kwenye Dimba la Kombe la Dunia limefungwa na Rafik Halliche akiunga mpira wa faulo uliopigwa na Karim Ziani

TASWIRA MAKINI!!!!










Mmmh!! Mambo ya sherehe ya kuukaribisha mwaka 2010 kwa Wafanyakazi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC). Matukio yalikuwa mengi kwa hiyo nitaendelea kukushushia kidogo kidogo!! Lakini nimependa sana watu walivyoshow love!