Friday, August 20, 2010

WALIMU WATAKIWA KUACHA TABIA YA UMAMLUKI!!


NAIBU katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Ezekiel Oluoch, akiongea na walimu wa shule za msingi na sekondari katika ukumbi wa Songea Club mjini hapa huku akiwataka walimu hao kuacha mara moja kuwa vibaraka wa wanasiasa kama wengi wao walivyogeuka kuwa makampeni meneja wa wagombea katika mchakato wa upigaji kura za maoni uliofanyika hivi karibuni. (Picha zote na Emmanuel Msigwa, Songea)

BALOTELLI AIBEBA MAN CITY, COLE AKIKOSA PENALTY!!



Michezo ya kusaka nafasi ya kushiriki katika hatua ya Makundi ya Mashindano ya Europa imeendelea na kushuhudia Manchester City ikichomoza na ushindi wa goli moja kwa nunge dhidi ya FC Timisoara kwa goli la Super Mario Balotelli. Vijogoo vya Jiji, Liverpool vimevuna ushindi wa goli moja kwa buyu mbele ya Trabzonspor huku Joe Cole akikosa mkwaju wa penalty!!!

GALLAS ATUA TOTTENHAM!!


Nahodha wa zamani wa Washika Bunduki wa Jiji la London, Arsenal, William Gallas amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Tottenham Hotspur akiwa mchezaji huru. Gallas alikuwa anawaniwa na Kibibi Kizee cha Turin, Juventus na Panathinaikos ya Uguriki!!!

Thursday, August 19, 2010

MAN CITY KUUZA WACHEZAJI WATATU!!





Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester City, Roberto Mancini ametangaza kuwa tayari kuwauza wachezaji watatu wa timu hiyo. Golikipa Shay Given baada ya Joe Hart kuonesha uwezo mkubwa, Mshambuliaji Roque Santa Cruz ambaye hana uhakika wa namba pamoja na Robinho ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo katika Klabu ya Santos!!!

MASCHERANO KUONDOKA KWA ADA KUBWA YA UHAMISHO!!


Kocha wa Vijogoo vya Jiji Klabu ya Liverpool, Roy Hodgson amesema atamuuza kiungo ambaye hajatulia wa timu hiyo Javier Mascherano iwapo klabu ambazo zinamtaka zitatoa fungu kubwa kuweza kumnunua. Mascherano amemwambia Hodgson anataka kuondoka Anfield kwa sababu zake binafsi huku Inter Milan na Barcelona zikimwania!!!

Wednesday, August 18, 2010

JAMES MILNER AKAMILISHA USAJILI WAKE MAN CITY!!!



Kiungo wa Kimataifa wa Uingereza, James Milner amekamlisha usajili wake wa kujiunga na Manchester City akitokea Aston Villa kwa kitita cha Pauni milioni 26 sambamba na mchezaji Stephen Ireland!!!

YANGA YATWAA NGAO YA HISANI!!!


Timu ya Yanga ilifanikiwa kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuwafunga Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kwa changamoto ya mikwaju ya penalty. Yanga iliibuka mbabe kwa mikwaju mitatu dhidi ya mmoja wa Simba!!!

ANELKA AUDHIKI UAMUZI WA FFF KUMFUNGIA!!!


Mshambuliaji wa Klabu ya Chelsea, Nicolas Anelka ameudhiaki uamuzi wa Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Kabumbu nchini Ufaransa FFF kumfungia michezo kumi na nane ya kimataifa baada ya kuwa chanzo cha kuzuka mtafaruku wakati wa fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Anelka amesema vyote vinavyofanyika havina maana na vimekuja kwa sababu Kocha Mpya Laurent Blanc aweze kufanya kazi zake kwa amani!!!

ANELKA, EVRA, RIBERY NA TOULALAN WAFUNGIWA TIMU YA TAIFA!!!






Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Ufaransa FFF limewafungiwa wachezaji ambao waanaelezwa kuwa chanzo cha kutokea mgomo! Nicolas Anelka amefungiwa michezo kumi na nane, Nahodha wa Kikosi hicho Patrice Evra michezo mitano, Franck Ribery michezo mitatu na Jeremy Toulalan mchezo mmoja!!!

Tuesday, August 17, 2010

SIMBA vs YANGA!!!



Watani wa Jadi Simba na Yanga leo wanashuka dimbani katika mchezo wao wa Ngao ya Hisani ikiwa ni ufunguzi wa Ligi katika Msimu ujao ambao unataraji kuanza mwishoni mwa juma hili. Mpambano huo unapigwa katika Dimba la Taifa huku Simba akiwa bingwa mtetezi!!

CUF YABADILI TAREHE YA KUMSINDIKIZA MGOMBEA WAO WA URAIS!!

CUF - Chama Cha Wananchi kinawatangazia Wananchi wote kuwa kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya tarehe ya kurudisha fomu ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo basi Mgombea wa Urais Profesa Ibrahim Haruna Lipumba atarudisha fomu tarehe 19/08/2010.

Msafara huo utaanzia Ofisi ya Wilaya ya Ilala iliyopo Buguruni Shell saa 4.00 asubuhi na msafara huo utapitia barabara za Uhuru hadi Mnazi mmoja, Bibi Titi, Ohio, Ghana na kuingia Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Taifa.

CUF - Chama Cha Wananchi tunawaomba wanachama wote wanaopenda mabadiliko kujitokeza kwa wingi kumsindikiza Prof. Ibrahim Lipumba.

Aidha tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya na hii imekuwa nje ya uwezo wetu.

MAN UTD YAICHAKAZA NEWCASTLE UNITED!!!








Timu ya Manchester United imeanza ligi kwa ushindi baada ya kuichakaza Newcastle United kwa magoli 3-0 katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi uliopigwa katika Dimba la Old Trafford!!!

Sunday, August 15, 2010

MRITHI WA FABIO CAPELLO ATAKUWA MZAWA!!!


Chama Cha Soka nchini England FA kimesema kocha ambaye atakuja baada ya Fabio Capello kumaliza mkataba wake atakuwa mzawa na si kutoka taifa jingine. Mkurugenzi Mtendaji wa FA amethibitisha Kocha ambaye atafuata baada ya 2012 atakuwa Muingereza!!!

MAMADOU NIANG B 52 AIHAMA MARSEILLE!!





Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal na nahodha wa zamani wa Olympique De Marseille Mamadou Niang maarufu kama B 52 ameihama klabu hiyo na kutimkia Fenerbahce ya Uturuki!!!

JIONEE MWENYEWE MAMBO YALIVYO!!!


Kutokana na miundombinu ya stendi kuu ya mabasi Songea kuwa mibovu imekuwa vigumu kwa magari makubwa kuingia na kutoka katika stendi hiyo kama inavyoonekana gari lenye namba za usajiri T 439 AJQ mali ya kampuni ya CocaCola likishindwa kutoka katika stendi hiyo na kusababisha adha kubwa kwa wengine.

Uuzaji wa mafuta ya kula wa mtindo huu umekuwa ukifananishwa na uchakachuaji wa mafuta ya Dizeli na Petroli ulioshamiri katika siku za hivi usoni kwani wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia ubora wa mafuta hayo kupungua kutokana na kuuziwa ndani ya makopo

Watoto kutoka Shirika la Masista wa Maria Immaculata kutoka India (DMI) mkoa wa Ruvuma wakionesha umahili wa kucheza ngoma ya ukakamavu ya mganda katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa DMI iliyofanyika katika viwanja vya makumbusho ya Vita vya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea mwishoni mwa wiki.

Askofu mkuu jimbo Katoliki la Songea, Mhashamu Norbert Mtega akicheza na watoto wimbo wa kuliombea Taifa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa DMI iliyofanyika katika viwanja vya makumbusho ya Vita vya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea mwishoni mwa wiki.

Mama mkuu wa Shirika la Masista wa Maria Immaculata kutoka India (DMI) Afrika, Sista Thianes (kushoto) akiteta jambo na Askofu mkuu jimbo Katoliki la Songea, Mhashamu Norbert Mtega katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa DMI iliyofanyika katika viwanja vya makumbusho ya Vita vya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea mwishoni mwa wiki.(Picha zote na Emmanuel Msigwa, Songea)

MANCINI AMTAKA GIVEN ASALIE MAN CITY!!


Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester City, Robert Mancini amemtaka Mlindamlango wa timu hiyo Shay Given kuendelea kusalia licha ya kukira kwamba chaguo lake la kwanza kwa sasa ni Joe Hart ambaye aliisaidia kuambulia sare dhidi ya Tottenham Hotspurs!!!

LIVERPOOL NA ARSENAL HAKUNA MBABE!!!








Mechi ya kwanza ya Big Four nchini England imeshuhudia Vijogoo vya Jiji Liverpool vikigawana pointi na Washika Mitutu wa Jiji la London, Arsenal baada ya dakika tisini za mchezo wao kumalizika kwa sare ya goli 1-1!!!

Friday, August 13, 2010

UGONJWA WA AJABU WAWAKUMBA WANAFUNZI!!!


Baadhi ya wanafunzi wa darasa la Saba katika shule ya msingi ya Ilembula, wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe waliokumbwa na ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu wakiwa wamehifadhiwa katika moja ya darasa la shule hiyo kusubiri kurejea kwa fahamu zao baada ya kuanguka

Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Ilembula, wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe aliyekumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kupoteza fahamu akibebwa na wanafunzi wenzie kwa kushirikiana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bi. Betty Simon (kulia) mara baada ya kuanguka na kumpeleka katika darasa lililotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi waliokumbwa na ugonjwa huo.

Mwalimu mkuu wa shule ya Ilembula, wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Bi. Betty Simon (kushoto) akijaribu kumdaka mmoja wa wanafunzi wa darasa la Saba wa shule hiyo aliyekumbwa na ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu kabla hajaanguka chini.

Mmoja wa wanafunzi wa kike wa darasa la Saba katika shule ya msingi ya Ilembula, wilaya mpya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe aliyekumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kupoteza fahamu akianguka mara baada ya kutoka chooni (kinachoonekena nyuma yake) kama alivyonaswa na mpiga picha wetu. (Picha kwa Hisani ya Emmanuel Msigwa)

Monday, August 2, 2010

BABU SONG ATANGAZA KUTUNDIKA DARUGA CAMEROON!!




Mkongwe Rigobert Song atangaza kutundika daruga katika Soka la Kimataifa baada ya kuitumikia Cameroon kwa michezo 137 na kufunga magoli 4 tu. Hatua hiyo inakuja baada ya kucheza fainal nne za Kombe la Dunia na kuwa mchezaji ambaye amepata mafanikio makubwa akiwa na Kikosi cha Simba wasiofugika.