Tuesday, July 6, 2010

SEMENYA HURU KUSHIRIKI MASHINDANO!!!


Mfukuza Upepo kutoka nchini Afrika Kusini Caster Semenya ameruhusiwa kushiriki katika mashindano ya riadhaa duniani baada ya uchunguzi aliofanyiwa kubaini kuwa jinsi yake ni ya kike na si ya kiume kama ambavyo ilikuwa inadaiwa awali!!!

WOZA 2010-HOLLAND YATINGA FAINAL!!!










Timu ya Taifa ya Holland imefanikiwa kukata tiketi ya kutinga Soccer City kwa ajili ya Fainal baada ya kuichabanga Uruguay kwa magoli 3-2. Holland sasa inasubiri mpinzani wake kwa ajili ya mchezo wa fainal utakaopigwa Jumapili!!!

Monday, July 5, 2010

MARADONA KUKACHA KIBARUA CHAKE ARGENTINA!!!


Kocha Mkuu wa Argentina Diego Armando Maradona amesema atatangaza msimamo wake iwapo ataendelea kuifundisha Timu hiyo baada ya kutolewa katika hatua ya Robo Fainal kwa kupata kichapo kizito cha magoli 4-0!!!

NADAL ALIVYOTWAA UBINGWA WA WIMBLEDON!!!








Mchezaji nambari moja Duniani kwa mchezo wa Tennis upande wa Wanaume Rafael Nadal amefanikiwa kutwaa ubingwa w wimbledon baada ya kumchakaza Tomas Berdych kwa seti tatu kwa bila. Matokeo yalikuwa 6-3 7-5 na 6-4!!!

DUNGA ATIMULIWA KUINOA BRAZIL!!


Shirikisho la Soka nchini Brazil CBF limetangaza kumtimua kazi Kocha wa Kikosi hicho ambacho alikuwa anakiongoza kwenye mchuano wa Kombe la Dunia na kutolewa kwenye hatua ya Robo Fainali Carlos Dunga. CBF imesema Kocha mpya atatajwa mwezi ujao na kuchukua jukumu la kukinoa kikosi hicho.

Saturday, July 3, 2010

MKUU WA WILAYA YA MBINGA ATAKA WANAWAKE WAWE WAKALI KWA WAUME ZAO!!!

Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Kanali mstaafu Edmund Mjengwa amewataka wanawake wilayani humo kuwa wakali kwa waume zao katika kipindi cha mavuno na mauzo ya Kahawa kwa madai kuwa wengi wao wamekuwa wakithubutu kuongeza wanawake baada ya mauzo ya Kahawa.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha Tingi, wilayani hiyo Mjengwa amesema katika wilaya hiyo wanawake ndiyo wanaoonekana kujituma zaidi katika kazi za shambani hususani katika kilimo cha zao la Kahawa lakini wanaume hujitokeza nyakati za mavuno na mauzo pekee.

Amesema tabia hiyo ya wanaume kujitokeza na kujifanya wao ndiyo wapangaji wakubwa wa mauzo nyakati hizo kumekuwa kukisababisha familia zao kuendelea kuishi maisha duni kutokana na wengi wao kutumia fedha zote za mauzo ya Kahawa kwa kuongeza wanawake na kupenda anasa zilizokithiri.

Kanali Mjengwa amesema endapo wanawake hao wakiwa wakali kwa wanaume zao juu ya suala hilo litasaidia pia katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuzifanya familia zao kuwa na maisha bora zaidi.

Ameeleza kuwa tabia hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuleta msukumo mkubwa kwa baadhi ya wanawake wenye tabia ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini kuja katika wilaya hiyo kuvuna fedha kwa wanaume wapenda anasa.

Baadhi ya wananchi waliiomba serikali kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kufanya hivyo kwa madai kuwa licha ya kuingilia uhuru wao binafsi lakini unawanyanyasa wanawake na watoto wasio na hatia kukosa haki zao za msingi ikiwemo kupata matibabu bora na elimu. (Habari na Emmanuel Msigwa)

SPAIN YATINGA NUSU FAINAL WOZA 2010!!!









Timu ya taifa ya Spain imetinga hatua ya nusu fainal baada ya kuichabanga Paraguay kwa goli moja kwa nunge. Goli hilo pekee la Spain limekwamishwa nyavuni na David Villa na hivyo sasa timu hiyo itakuwa na kibarua dhidi ya German!!!

SERENA ATWAA UBINGWA WA WIMBLEDON!!!





Mchezaji ambaye anaorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwa ubora wa Tennis upande wa wanawake Serena Williams amefanikiwa kutwaa taji la Wimbledon baada ya Vera Zvonareva kwa mbili za 6-3 na 6-2.

MATUKIO MBALIMBALI MIKOA YA KUSINI!!!!


Wananchi wa mtaa wa Mahenge mjini Songea wakichangishana fedha kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu hivi karibuni wakati wa mkutano wa kuunda kamati ya kusimamia mfuko wa kusaidia watoto hao katika mtaa huo

Wanafunzi wa mwaka wa Tatu, Semista ya Sita wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha St. Joseph kilichopo mjini Songea mkoa wa Ruvuma, Bi. Olivia Masange (kulia) na Bi. Sophia Kalinga wakisoma vitabu kupitia mtandao katika maktaba ya chuo hicho mara baada ya kuzinduliwa juzi na mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bi. Christine Ishengoma

Suala la utunzaji wa mazingira katika halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma linaonekana kukosa mwamko miongoni mwa wananchi walio wengi kama inavyoonekana pichani wananchi wakiendelea kutupa takataka eneo ambalo kuna kibao kilichopiga marufuku kutupa takataka

Mdau wa Blogu hii Emmanuel Msigwa (kulia) akizungumza na Ofisa mtendaji wa kijiji cha Ilungu, kata ya Ipepo wilayani Makete, Lumeo Sanga juu ya kudorora kwa elimu katika kijiji hicho kutokana na kukithiri kwa imani za kishirikina miongoni mwa wananchi

WOZA 2010- ARGENTINA NJE!!!




Friday, July 2, 2010

BRAZIL YAONDOLEWA WOZA 2010!!!












Timu ya Taifa ya Brazil imeondolewa katika kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia baada ya kufungwa magoli 2-1 na Uholanzi!!!