Saturday, September 18, 2010

MHANGA WA UBUNGE AUKWAA UKUU WA WILAYA!!!


Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM Nape Moses Nnauye ameteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi. Hii inaweza kuwa njia moja wapo ya kumfuta "JASHO" baada ya kushindwa kupata nafasi ya kuwa mgombea Ubunge katika Jimbo la Ubungo!!!

Thursday, September 16, 2010

TAKUKURU YATAKIWA KUUNGWA MKONO KWENYE SHUGHULI ZAKE!!!

Katibu Mkuu Ikulu, Bwana Michael Mwanda amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Lindi, viongozi, Asasi Zisizo za Kiserikali pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani humo, kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa vile jukumu la kupambana na rushwa ni la Watanzania wote.

“Jukumu la kupambana na rushwa ni letu sote na ndiyo maana kwa kutambua hilo, nipo hapa leo kuwaunga mkono katika mapambano dhidi ya rushwa. Napenda nitumie nafasi hii pia kuwahamasisha wananchi wote wa Mkoa wa Lindi pamoja na viongozi wenzangu kuwaunga mkono TAKUKURU katika mapambano haya mazito”, amesema.

Bwana Mwanda amebainisha hayo mjini Lindi 16 Septemba, 2010 akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi za TAKUKURU mkoani humo, iliyohudhuriwa pia na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Asasi Zisizo za Kiserikali.

Katika hotuba yake, Bwana Mwanda amesema hatua ya TAKUKURU kujenga jengo la ofisi katika Mkoa wa Lindi, inatokana na dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Nne katika kuimarisha utawala bora na kuboresha utendaji wa kazi wa taasisi hiyo, kwa vile siku zote lengo la Serikali ni kupeleka huduma karibu na wananchi.

“…lengo la Serikali yetu siku zote limekuwa ni kupeleka huduma karibu na wananchi ili waweze kufanya shughuli zao za kimaendeleo kwa ufanisi na kuhakikisha kwamba kero ya rushwa inadhibitiwa vilivyo katika kila kona ya nchi yetu”, amebainisha Bwana Mwanda.

Amesema vita ya kuzuia na kupambana na rushwa ni kubwa inayohitaji umakini, moyo wa kujitolea na kujituma, na wakati mwingine kukubali lawama, hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa TAKUKURU ili waweze kutoa huduma zilizo bora zaidi.

Bwana Mwanda amewatanabaisha viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuwaelimisha waumini wao na hasa vijana kuhusu ubaya wa rushwa, na amewashauri kutumia nafasi waliyo nayo kutoa elimu ya maadili mema kwa waumini ili waepukane na maovu, hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa kujenga jamii adilifu na inayochukia vitendo vya rushwa.

Katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31, 2010, Bwana Mwanda amewahimiza wananchi kuzingatia matakwa ya sheria zinazosimamia masuala ya rushwa katika uchaguzi, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo haugubikwi na vitendo vya rushwa.

Ili kuhakikisha kuwa TAKUKURU inapata mafanikio zaidi, Bwana Mwanda ameitaka Taasisi hiyo kuimarisha Kamati za Uadilifu zilizopo katika Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya, kuzishirikisha Asasi Zisizo za Kiserikali katika vita dhidi ya rushwa katika ngazi hizo, kuendelea kujenga uwezo wa watumishi wake, na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu rushwa.

SIMBA YAZOA POINTI TATU WAKATI YANGA IKICHECHEMEA!!!




Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea ambapo Bingwa Mtetezi Simba amefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Wakati Mtibwa wakiwalazimisha sare Yanga ya goli moja kwa moja huku Azam wakipata kichapo cha goli moja kwa nunge kutoka kwa Kagera Sugar!!!

CUF WALAANI KUPIGWA KWA MWANDISHI KWENYE KAMPENI!!!

CUF – Chama cha Wananchi tumesikitishwa na kitendo cha mwandishi wa gazeti la Mwananchi Fredrick Katulanda, kuvamiwa na kushambuliwa na kikosi cha “janjaweed” wa Chama cha Mapinduzi wanatambulika kama “Green Guard” na kumjeruhi, katika kampeni za Ubunge katika jimbo la Sumve, Kijiji cha Nyambiti.

Walinzi hao walimshambulia mwandishi huyo na kumjeruhi sehemu za puani na mdomoni wakati wakimtaka yeye na wanataaluma wengine wa fani ya uandishi waondoke kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo hilo la Sumve, wilayani Kwimba.

CUF – Chama cha Wananchi tunalaani, kitendo hicho kuwa siyo cha kiungwana hata kidogo, licha ya kuhatarisha amani ya nchi lakini pia ni ukiukwaji mkubwa wa maadili na haki za binadamu cha kuwapiga waandishi wakiwa kazini.

CUF – Chama cha Wananchi tunatambua kuwa, vitendo hivi vimefanywa na Chama cha Mapinduzi, kutokana na mazoea ya kubebwa kwa kuripotiwa habari zao kwa kupambwa zaidi kuliko uhalisia, hivyo pindi waandishi wanapofuata maadili ya taaluma yao na kuripoti habari kama zilivyo, inakuwa nongwa kwa CCM, na kupanda jazba hatimaye kujichukulia sheria mikononi mwao.

CUF – Tunaviomba vyombo vyote vinavyohusika, kuwachukulia hatua kali Chama cha Mapinduzi, kwa uvunjifu huu wa amani, ukiukwaji wa maadili wakati wa kampeni na kwa vile ni vitendo vya jinai, tunalisihi jeshi la Polisi kuhakikisha wale wote waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa Chama hicho.

CUF – Tunawatanabaisha Watanzania kuwa makini na chama hiki kinachoashiria uvunjivu wa amani iliyoasisiwa na wazee wetu, kwani hata ukiangalia baadhi ya mabango yao ya kampeni yanatoa vitisho kwenu wapiga kura ili msichague chama kingine iwapo kama mnataka amani, hii ina maana kuwa wapo tayari kuvunja amani iliyopo iwapo hawatachaguliwa.

HAKI SAWA KWA WOTE

RAFAEL NADAL AENDELEA KUSHEREHEKEA TAJI LA US OPEN!!!


Mchezaji ambaye anaorodheshwa katika nafasi ya kwanza upande wa wanaume kwa Mchezo wa Tennis na Bingwa wa US Open Rafael Nadal ameendelea kusherehekea ubingwa wake na hapa ilikuwa katika Uwanja wa Sabtiago Bernabeu kabla ya kuchezwa kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madrid na Ajax Amsterdam.

MAUAJI YAFANYIKA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA!!!










Uefa Champions League
AC Milan 2-0 Auxerre
Arsenal 6-0 Braga
Bayern Munich 2-0 Roma
CFR 1907 Cluj-Napoca 2-1 Basle
Marseille 0-1 Spartak Moscow
MSK Zilina 1-4 Chelsea
Real Madrid 2-0 Ajax
Shakhtar Donetsk 1-0 Partizan Belgrade

CUF NA MATOKEO YA UTAFITI YA SYNOVTE!!!

CUF – Chama cha Wananchi tumefarijika kwa taarifa iliyosahihi inayoelezea hali halisi ya utolewaji wa Habari za kampeni katika vyombo vya Habari, iliyoripotiwa na Meneja taasisi ya Synovate Bi. Jane Meela jana Jumanne, Septemba 14, jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ambayo imeripotiwa katika vyombo vya Habari imebainisha kwamba, katika utafiti wao wa pili Taasisi ya Synovate imegundua kuwa katika kampeni zinazoendelea Magazeti yameegemea kuripoti zaidi Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufuatiwa na Chama cha Demokrasia Makini (CHADEMA) na kuviacha vyama vingine pasipo kupewa kipaumbele.

Taarifa hiyo imesema kuwa vyombo vya televisheni havikulalia upande wowote, taarifa zao wanazozitoa zinatoa kipaumbele kwa vyama mbalimbali (neutral) tofauti na vyombo vya magazeti, na isitoshe suala la amani limekuwa likizungumziwa zaidi katika kampeni zilizoripotiwa, halikadhalika Chama cha CHADEMA kilimepata kipaumbele mara baada ya kumtangaza mgombea wake wa Urais.

CUF – Chama cha Wananchi pamoja na kufarijika kwa ripoti hii ya Synovate ambayo inausahihi ndani yake, lakini pia tunamasikitiko kwa vyombo hivyo vya habari kwani pamoja na nia nzuri ya kuongozana na baadhi ya waandishi wao katika ziara za kampeni zetu za mgombea Urais na mgombea mwenza, lakini bado kipaumbele kimeelekezwa zaidi kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia Makini (CHADEMA).

CUF – Tunawatanabaisha Watanzania kuwa dhamira ya makusudi inayofanywa na vyombo vingi vya habari (ukiacha vichache), hususani magazeti ni kujaribu kuonyesha kuwa upinzani uliopo katika uchaguzi mwaka huu kwa Tanzania Bara, ni baina ya CCM na CHADEMA, na kwa upande wa Zanzibar ni baina ya CCM na CUF, jambo ambalo halina ukweli kabisa.

CUF – Tunatambua kuwa harakati hizi hazikuanza leo, kwani waandishi walidiriki kulitamka hili bayana katika mikutano yetu na waandishi wa habari mapema mwaka jana 2009, kabla ya kuumbuliwa na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji zilizofanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka jana, ambapo pamoja na taarifa halisi za matokeo hayo kutotangazwa na wizara ya TAMISEMI (kwa kuchelea kuumbuka), bado chama chetu kilifanya zizuri kuliko chama kingine chochote cha upinzani.

Ikiwa hata mwaka haujatimia tangu uchaguzi huo kufanyika, hayamkiniki kigezo kinachotumika na baadhi ya vyombo hivi vya habari kukipa kipaumbele chama ambacho kiliambulia mitaa saba tu, katika jiji hili la Dar es Salaam, na chama chetu kufanikiwa kuchukua mitaa 34, ambapo maeneo yaliyokuwa ni ngome zetu kuu ambayo ni wastani wa robo tatu wa wagombea wetu walienguliwa.

CUF – Tunavisihi vyombo vya Habari pamoja na kuifanyia kazi kamilifu ripoti ya Synovate, wazingatie maadili ya uandishi wa habari, jambo ambalo wamekuwa wakiliahidi na kujivuna nalo, hatupendi matukio ya mwaka 2005 ya wananchi wenye hasira kali kukosa imani na vyombo hivyo, yakajirudia katika uchaguzi huu.

HAKI SAWA KWA WOTE

Wednesday, September 15, 2010

MAMBO YALIVYOKUWA CHAMPIONS LEAGUE!!!












Uefa Champions League
Barcelona 5-1 Panathinaikos
Benfica 2-0 Hapoel Tel-Aviv
Bursaspor 0-4 Valencia
FC Copenhagen 1-0 Rubin Kazan
FC Twente 2-2 Inter Milan
Lyon 1-0 Schalke 04
Man Utd 0-0 Rangers
Werder Bremen 2-2 Tottenham

VALENCIA NJE MSIMU WOTE!!




Kiungo wa Pembeni wa Klabu ya Manchester United Antonio Valnecia huenda akawa nje ya Dimba kwa kipindi chote cha msimu kutokana na kuumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Rangers uliopigwa kwenye Dimba la Old Trafford. Kocha Mkuu wa Man Utd Sir Alex Ferguson amethibitisha huenda mchezji huyo asipatikane hadi mwishoni mwa msimu!!!

Wednesday, September 1, 2010

AJALI ZA BARABARANI BADO NI TATIZO SUGU!!!!


Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakipima ajali ya gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajiri T 544 AFY inayofanya safari zake kati ya Mtyangimbole na mjini Songea mara baada kufeli breki na dereva kulazimika kukata kona ya ghafla na kisha kuparamia ukuta wa hotel ya kufikia wageni ya Safina Lodge mjini Songea. Zaidi ya abiria 20 wamenusurika kifo katika ajali hiyo

Crista Komba mkazi wa mjini Songea mkoa wa Ruvuma, akipata matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Songea baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajiri T 544 AFY inayofanya safari zake kati ya Mtyangimbole na mjini Songea mara baada gari hilo kufeli breki na dereva kulazimika kukata kona ya ghafla na kisha kumgonga. Zaidi ya abiria 20 wamenusurika kifo katika ajali hiyo. (Picha zote na Emmanuel Msigwa, Songea)